sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,687
- 1,111
Lukuvi ana tatizo gani na mh. Samia rais wa JMT!! Alipomtoa kwenye uwaziri alisema anataka awe mshauri wake, lakini hakufafanua mshauri wa nini, watu wakapaza sauti kuwa Mama kavunja katiba kwa kumteua, likasemwa sana likapita.
Lukuvi kagombea U-NEC nao kaangukia pua, si ajabu kwa giant kama Lukuvi, nguli wa siasa za nyanda za juu kusini kudondoka, ila kina stusha ni ghafla mno. Shida iko wapi au kuna sehemu alikosea!!!
Kubwa nalo liona wanasiasa wengi hawajui kusoma alama za nyakati, hii hugharimu sana maisha yao ya kisiasa kuishia pabaya. Hawataki kung'atuka mpaka wajumbe waonekane siyo watu wazuri!!!
Mh Lukuvi mbio za farasi huishia ukingoni, rudi kwa mzee mwenzio Mzindakaya muulize aliona nini ambacho wewe umeshindwa kukiona!! Kwa heshima uliyojijengea ni wakati sasa wa kuachia vijana wewe ubaki kuwa mshauri, mbona Mark Mwandosya kaweza wewe na timu ya kina Wassira inashindwa nini!!!