Lukuvi, mbio za sakafuni huishia ukingoni; jitafakari

Lukuvi ana tatizo gani na mh. Samia rais wa JMT!! Alipomtoa kwenye uwaziri alisema anataka awe mshauri wake, lakini hakufafanua mshauri wa nini, watu wakapaza sauti kuwa Mama kavunja katiba kwa kumteua, likasemwa sana likapita.

Lukuvi kagombea U-NEC nao kaangukia pua, si ajabu kwa giant kama Lukuvi, nguli wa siasa za nyanda za juu kusini kudondoka, ila kina stusha ni ghafla mno. Shida iko wapi au kuna sehemu alikosea!!!

Kubwa nalo liona wanasiasa wengi hawajui kusoma alama za nyakati, hii hugharimu sana maisha yao ya kisiasa kuishia pabaya. Hawataki kung'atuka mpaka wajumbe waonekane siyo watu wazuri!!!

Mh Lukuvi mbio za farasi huishia ukingoni, rudi kwa mzee mwenzio Mzindakaya muulize aliona nini ambacho wewe umeshindwa kukiona!! Kwa heshima uliyojijengea ni wakati sasa wa kuachia vijana wewe ubaki kuwa mshauri, mbona Mark Mwandosya kaweza wewe na timu ya kina Wassira inashindwa nini!!!
Hawa wakongwe na CCM wajifunze kuwa kuku mzee hatagi yai😅😅
 
Kila nikikumbuka Bilioni 7 za royal tour na deni la taifa lilivyopaa na mnasema bila haya mtaendelea kopa.. Haki tena mtu kama Lukuvi ni wa muhimu sana kwa sasa..
Maccm yote yaliyosalia kuanzia bosi wenu mkulu hakuna mwenye UWEZO WA lukuvi
 
Waziri Kivuli Assistant to the Assisting Prime Minister katika Ofisi ya Raisi President Special Chapa Wadogo Mnyooshaji Mkubwa.

Cheo Kigumu sana

Waziri Mkuu Plenipotential

Mpeni haki
 
Lukuvi ana tatizo gani na mh. Samia rais wa JMT!! Alipomtoa kwenye uwaziri alisema anataka awe mshauri wake, lakini hakufafanua mshauri wa nini, watu wakapaza sauti kuwa Mama kavunja katiba kwa kumteua, likasemwa sana likapita.

Lukuvi kagombea U-NEC nao kaangukia pua, si ajabu kwa giant kama Lukuvi, nguli wa siasa za nyanda za juu kusini kudondoka, ila kina stusha ni ghafla mno. Shida iko wapi au kuna sehemu alikosea!!!

Kubwa nalo liona wanasiasa wengi hawajui kusoma alama za nyakati, hii hugharimu sana maisha yao ya kisiasa kuishia pabaya. Hawataki kung'atuka mpaka wajumbe waonekane siyo watu wazuri!!!

Mh Lukuvi mbio za farasi huishia ukingoni, rudi kwa mzee mwenzio Mzindakaya muulize aliona nini ambacho wewe umeshindwa kukiona!! Kwa heshima uliyojijengea ni wakati sasa wa kuachia vijana wewe ubaki kuwa mshauri, mbona Mark Mwandosya kaweza wewe na timu ya kina Wassira inashindwa nini!!!
Kapumzike kama kina mzee pinda hawana pressure wanaendesha maisha yao kilaini hawabughudhi mtu wala hawabugudhiwi na mtu, katafute shamba Isimani, mzee wetu
 
Lukuvi, Moja ya Mzee Makini sana na Tunu Kwa Taifa.

Kwa Taifa hili lenye Vijana wajinga waimbao mapambio Kila uchwao.

Mzee anahitajika sana ,tumuombee uzima, 2025 sio mbali.
Kama mzee makini kawaulize tembo wa maeneo ya makatapola ng'ambo ya migoli mlazo,mapela mengi au waulize watu wa migoli.
 
Back
Top Bottom