Lukuvi, mbio za sakafuni huishia ukingoni; jitafakari

Lukuvi, mbio za sakafuni huishia ukingoni; jitafakari

Lukuvi ana tatizo gani na mh. Samia rais wa JMT!! Alipomtoa kwenye uwaziri alisema anataka awe mshauri wake,lakini hakufafanua mshauri wa nini,watu wakapaza sauti kuwa Mama kavunja katiba kwa kumteua,likasemwa sana likapita.

Lukuvi kagombea U-NEC nao kaangukia pua,si ajabu kwa giant kama Lukuvi,nguli wa siasa za nyanda za juu kusini kudondoka,ila kina stusha ni ghafla mno. Shida iko wapi au kuna sehemu alikosea!!!

Kubwa nalo liona wanasiasa wengi hawajui kusoma alama za nyakati,hii hugharimu sana maisha yao ya kisiasa kuishia pabaya. Hawataki kung'atuka mpaka wajumbe waonekane siyo watu wazuri!!!

Mh Lukuvi mbio za farasi huishia ukingoni,rudi kwa mzee mwenzio Mzindakaya muulize aliona nini ambacho wewe umeshindwa kukiona!! Kwa heshima uliyojijengea ni wakati sasa wa kuachia vijana wewe ubaki kuwa mshauri, mbona Mark Mwandosya kaweza wewe na timu ya kina Wassira inashindwa nini!!!
Mzindakaya yupi au yule aliye kaburini?
 
..Lukuvi si alikuwa ktk genge la Magufuli?

..sasa kwanini ameshindwa wakati tuliambiwa watu wa Magufuli ndio walioongoza kwa kura ktk uchaguzi wa Nec?

..au Lukuvi ameshindwa kwasababu sio mwenyeji wa kanda ya ziwa?
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Lukuvi ana tatizo gani na mh. Samia rais wa JMT!! Alipomtoa kwenye uwaziri alisema anataka awe mshauri wake, lakini hakufafanua mshauri wa nini, watu wakapaza sauti kuwa Mama kavunja katiba kwa kumteua, likasemwa sana likapita.

Lukuvi kagombea U-NEC nao kaangukia pua, si ajabu kwa giant kama Lukuvi, nguli wa siasa za nyanda za juu kusini kudondoka, ila kina stusha ni ghafla mno. Shida iko wapi au kuna sehemu alikosea!!!

Kubwa nalo liona wanasiasa wengi hawajui kusoma alama za nyakati, hii hugharimu sana maisha yao ya kisiasa kuishia pabaya. Hawataki kung'atuka mpaka wajumbe waonekane siyo watu wazuri!!!

Mh Lukuvi mbio za farasi huishia ukingoni, rudi kwa mzee mwenzio Mzindakaya muulize aliona nini ambacho wewe umeshindwa kukiona!! Kwa heshima uliyojijengea ni wakati sasa wa kuachia vijana wewe ubaki kuwa mshauri, mbona Mark Mwandosya kaweza wewe na timu ya kina Wassira inashindwa nini!!!
Duh, mbona mada yako hii inachanganya mkuu 'sammonssee'!

Nilipoanza kukusoma, nilidhani unamtia moyo huyo Lukuvi, ili asibweteke, bali ajipime na kutafakari vyema historia ya utumishi wake na nafasi yake katika nchi hii, ili aone kama anafaa kuitumikia zaidi katika ngazi za juu zaidi kuliko alizozifikia kwa uteuzi.
Ajipime, katika utumishi wake, kama waTanzania waliweza kuona juhudi zake katika kuwatumikia, na arudi kwao kwa mipango maalum awaombe wamtazame tena kama anafaa kuendelea kuwatumikia..

Lakini, kwa mafadhaiko kwa wengi, Lukuvi nadhani amekuwa kama viongozi wengine wote walioko huko CCM, ambao inaonyesha wanapoachwa katika nafasi za uteuzi wanakuwa hawana mawazo mengine zaidi. Hii ni ishara kwamba utumishi wao katika nafasi wanazopewa, si kwa wananchi, bali kwa hao wanaowateua kwenye nafasi hizo.

Viongozi waliomo CCM, hawajui kujijenga kwa wananchi moja kwa moja, hata kama wanaonekana kufanya kazi vizuri, badala yake utumishi wao wanaukabidhi kwa hao wanaowateua, na mara wanapoachishwa hizo nafasi, hawajui pa kuanzia ili kuwaended wananchi.

Kwa maoni yangu, hili ndilo tatizo alilopata Lukuvi, na ni kwa bahati mbaya sana, kwani kwa utendaji wake alioonyesha, ingekuwa rahisi kukumbushia tu kwa wananchi wampime zaidi na kumwamini kuwafanyia kazi zaidi endapo wangeridhia. Yeye kaweka kila kitu kwa akina Samia!

Inasikitisha sana.
 
Lukuvi ana tatizo gani na mh. Samia rais wa JMT!! Alipomtoa kwenye uwaziri alisema anataka awe mshauri wake, lakini hakufafanua mshauri wa nini, watu wakapaza sauti kuwa Mama kavunja katiba kwa kumteua, likasemwa sana likapita.

Lukuvi kagombea U-NEC nao kaangukia pua, si ajabu kwa giant kama Lukuvi, nguli wa siasa za nyanda za juu kusini kudondoka, ila kina stusha ni ghafla mno. Shida iko wapi au kuna sehemu alikosea!!!

Kubwa nalo liona wanasiasa wengi hawajui kusoma alama za nyakati, hii hugharimu sana maisha yao ya kisiasa kuishia pabaya. Hawataki kung'atuka mpaka wajumbe waonekane siyo watu wazuri!!!

Mh Lukuvi mbio za farasi huishia ukingoni, rudi kwa mzee mwenzio Mzindakaya muulize aliona nini ambacho wewe umeshindwa kukiona!! Kwa heshima uliyojijengea ni wakati sasa wa kuachia vijana wewe ubaki kuwa mshauri, mbona Mark Mwandosya kaweza wewe na timu ya kina Wassira inashindwa nini!!!

Kuna kauli fulani aliitamka kuhusu zenji ndio inayomtafuna.
 
Laana ya kuhonga Wapiga kura Ulanzi na viberiti , kwao maendeleo 0 lakini kila uchaguzi anahonga ulanzi na kuzuia wagombea wengine
Vipi isimani nako mlihujumiwa nini? Maana we huwa unasema kila mahali mmehujumiwa.
 
Back
Top Bottom