Lukuvi, mbio za sakafuni huishia ukingoni; jitafakari

Lukuvi, mbio za sakafuni huishia ukingoni; jitafakari

Lukuvi ana tatizo gani na mh. Samia rais wa JMT!! Alipomtoa kwenye uwaziri alisema anataka awe mshauri wake, lakini hakufafanua mshauri wa nini, watu wakapaza sauti kuwa Mama kavunja katiba kwa kumteua, likasemwa sana likapita.

Lukuvi kagombea U-NEC nao kaangukia pua, si ajabu kwa giant kama Lukuvi, nguli wa siasa za nyanda za juu kusini kudondoka, ila kina stusha ni ghafla mno. Shida iko wapi au kuna sehemu alikosea!!!

Kubwa nalo liona wanasiasa wengi hawajui kusoma alama za nyakati, hii hugharimu sana maisha yao ya kisiasa kuishia pabaya. Hawataki kung'atuka mpaka wajumbe waonekane siyo watu wazuri!!!

Mh Lukuvi mbio za farasi huishia ukingoni, rudi kwa mzee mwenzio Mzindakaya muulize aliona nini ambacho wewe umeshindwa kukiona!! Kwa heshima uliyojijengea ni wakati sasa wa kuachia vijana wewe ubaki kuwa mshauri, mbona Mark Mwandosya kaweza wewe na timu ya kina Wassira inashindwa nini!!!
Woote hao wana majina makubwa lakini hawana uwezo binafsi nje ya kubebwa.

Lukuvi alikuwa anawika kwa kubebwa tu lakini Uwezo wa kushindana hana.

Na atapotea mazima kama sio kuonewa huruma japo akabaki baki level za juu
 
Kila nikikumbuka Bilioni 7 za royal tour na deni la taifa lilivyopaa na mnasema bila haya mtaendelea kopa.. Haki tena mtu kama Lukuvi ni wa muhimu sana kwa sasa..
Ana umuhimu gani?
 
Na unatakiwa ujitoe akili kuamini Magu hakushinda kihalali. Nyie si kila siku mnatupa idadi ya watu wanaojiandikisha kupitia ile kampeni maarufu ya chadema kidigitali ambayo kwa sasa hatukusikii tena humu ukiipigia chapuo.? Au lengo la ile kampeni ni nini? Kutafuta watu wa kuandamana barabarani?

Sasa wenzenu wakisema wana mtaji wa kura hizo we unaumia, ila we ukisema ni sawa.

Nakusisitizia tena, upinzani hawashindi bila kupata kura za wanaccm, na ili kupata kura za wanaccm ni lazima kwanza itokee mipasuko ya kimakundi. Ombeeni hilo litokee kila chaguzi, utanishukuru badae.
Ndiyo maana ya uchaguzi,ukiona wamepata kura za ccm ujue wame pave to the success
 
Woote hao wana majina makubwa lakini hawana uwezo binafsi nje ya kubebwa.

Lukuvi alikuwa anawika kwa kubebwa tu lakini Uwezo wa kushindana hana.

Na atapotea mazima kama sio kuonewa huruma japo akabaki baki level za juu
Hajawahi kutokea mtia nia kwa nafasi ya urais kama Edward Lowassa,alikitikisa chama, serikali na organs zake,very strategically,wengine ni wakina tuooombe,tupige magotiiii
 
Na unatakiwa ujitoe akili kuamini Magu hakushinda kihalali. Nyie si kila siku mnatupa idadi ya watu wanaojiandikisha kupitia ile kampeni maarufu ya chadema kidigitali ambayo kwa sasa hatukusikii tena humu ukiipigia chapuo.? Au lengo la ile kampeni ni nini? Kutafuta watu wa kuandamana barabarani?

Sasa wenzenu wakisema wana mtaji wa kura hizo we unaumia, ila we ukisema ni sawa.

Nakusisitizia tena, upinzani hawashindi bila kupata kura za wanaccm, na ili kupata kura za wanaccm ni lazima kwanza itokee mipasuko ya kimakundi. Ombeeni hilo litokee kila chaguzi, utanishukuru badae.
We jamaa una matatizo ya Akili. Organs zote za serikali na uchaguzi na vyombo vyake vinajua Magu hakushinda🤣🤣🤣
 
Lukuvi anagombea anaangukia pia. Yule mzee Wasira anagombea anapata. Wasira alikua mkuu wa mkoa miaka ya sabini ya mwanzo mwanzo kabisa, yaani wasira ana zaidi ya miaka 50 kwenye uongozi. Yaani Wasira ameteuliwa na Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete Hadi Samia. Yaani hana jipya lkn anamzidi kete Lukuvi. Lukuvi jitafakari, wenzio ndani ya CCM wamekuchoka.
 
Ndiyo maana ya uchaguzi,ukiona wamepata kura za ccm ujue wame pave to the success
Ukiona umepata mke kwa sababu tu amegombana na mumewe ujue huyo sio wako, akielewana na mumewe ujue utalea watoto wa mwanaume mwenzio.

Majimbo mengi upinzani huwa wanashikilia temporary, ndio maana kipigo cha 2020 hadi leo hawaamini. CCM wakiacha wizi,upuuzi,ubinafsi wa viongozi wao maana hadi wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama wanachukiana kwa wizi na ubadhirifu wa mali za chama ukitoa nchi, na wakiungana wanachukua majimbo mapema tu.

Vijana wengi kama kina erythroc... hawaielewi hii kitu, wao wanajua mbunge wa chadema akishinda jimboni basi ni kura za chadema wakati 70% ni kura za wanaccm.
 
Kinacho sahaulika hakuna mgombea anayeshinda kwa kura za chama chake na hapo ndiyo maana halisi ya democracy,wakati mwingine unachagua mtu badala ya chama
 
Alimchochea Jiwe afute hati miliki ya shamba la kigamboni, baadae akapewa bakhresa ajenge kiwanda Cha sukari.

Atakiona Cha moto. Malipo hapahapa.
Ni kigamboni au mimi ndo sijui,kwahiyo kigamboni itakuwa sugarcane estate
 
Kinacho sahaulika hakuna mgombea anayeshinda kwa kura za chama chake na hapo ndiyo maana halisi ya democracy,wakati mwingine unachagua mtu badala ya chama
Kuna wengine hata bila kura za chama kingine wanashinda tu. Hiyo ndio tofauti.
 
Mpumbavu huyu alitaka kuanza kudhulimu hata masikini viwanja vyao vilivyo maeneo mazuri....
Alishobokea sana viwanja vya watu kigamboni, mpaka nikaanza kuona atafikia na kwangu, nyang'au huyu akafie mbali na asirudi tena.....
 
Ale alivyovuna miaka yote ya maisha yake.
Acheze na wajukuu inatosha siasa awaachie mataga vijana.
Kwanini Kwa Lukuvi tu na siyo kwa Kinana kafata nini alicho kisahau kwenye chama au tamaa tu ya madaraka tu kwanini chama kisiwape nafasi vijana? Mbona nchi za wenzetu vijana wa miaka 40 wanapewa nafasi kubwa tu, kwanini kinana asiwape nafasi vijana kuliko kukataa kustaafu uongozi, Viongozi wa Afrika akili zao zinafanana hawa taki kuachia madaraka iwe kisheria au kwa kujiuzulu, Mbona Viongozi wa Ulaya wakistaafu wanaridhika na wanakubali wamestaafu huwezi kuwaona wakikataa kustaafu mfano Obama, Clinton, Bush, David Cameroon wote awa anafanya shughuli zao uwezi kuwasikia wakionyesha nia ya kutaka kutawala tena, mfano ata Shein, Amani karume uwezi kuwaona wakitamani kuongoza tena.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom