Isikilize video iliyopo kwenye post #1 ina majibu ya maswali yako karibu yote. Yanini unaandikia mate na wino upo?
Uislaam ni mbele ya kitu chochote kile, na hapa tunauonesha mfumo kristo ulivyo na haupo CCM tu. Ni maradhi yaliyopandikizwa na Nyerere kwa muda wa miaka 26 mfululizo, ni gonjwa zito linawaathiri Watanzania wote si Waislaam pekee.
Huu ugonjwa alionao Lukuvi wa hofu kwa Uislaam unaliathiri taifa na si yeye tu mwenye gonjwa hilo, ni wengi sana.
ndugu zangu wanajf ninawaomba kwa heshima na taadhima wakati huu si wakuangalia dini hebu tujitahidi kwa pamoja tudai tanganyika yetu atakae kuwa mkristo au muislam ni imani yake kwa manufaa yake na anachotaka kufanya lukuvi na hao wasakatonge wenzake ni kuvuruga mada ili tugeukie dini tusitetee wala kupigania nchi yetu
Mimi ni mtetezi wa CCM daima. Kumbuka, mtoto akikunyea huukati mkono, unauosha unausafisha unaendelea na maisha.
Na hapa tupo katika kuusafisha mkono kwa kuudhihirisha mfumo kristo tunaouongea kila siku. Huu ni ushahidi kamili kuwa hatulalamiki kwa kupenda kulalamika tu. Yapo, toka kwa waziri mkuu mpaka kwa akina Lukuvi. Ni wengi tu wapo. lakini ukweli ukidhihiri uongo hujitenga.
Ka Lukuvi kamewakera Waislaam wengi wa CCM leo, na hata wale wasio wa CCM. Hukumsikiliza Lipumba hapo kwenye post #1 au unatumia kamchina hakaoni video?
Huwezi mkuu sababu ya hawa ccm,na wamefanya makusudi kudivert attention kwa kuwatumia mapandikizi yao kuingiza issue ya udini wakijua kuna akili ndogo zitaacha kujadili hoja at hand na kuzungumzia personality Lukuva lukuva,tuachane na habari ya katiba
Ana tofauti gani na Lukuvi?
Amandla.......
Hii lugha si muwaachie wenye nayo?
Amandla.....
Kwani wewe ulijiunga Chadema kumfuata Padre Slaa au Mchungaji Msigwa?
Mimi sijaelewa bado
Nimeusikiliza vizuri sana ,nimependa alivyopangilia hoja na kuhitimisha kwa nguvu za hoja. Sasa naona Intarahamwe mmeanza kushikana mashati wenyewe kwa wenyewe , kwani naona wa kuwabagua wameshaisha.
Mimi sijauona huo mfumo kristo hapo , nimeichukulia hiyo kauli kama kauli zingine za vitisho na ubaguzi kutoka kwa viongozi wa ccm, mbona huzungumzii kauli kama nchi itatawaliwa kijeshi ,Zanziba imepatikana kwa mapinduzi na serikali ya mapinduzi haiwezi kuchukuliwa kwa karatasi n.k.
Usitake kuugeuza huu mjadala uwe wa kidini , wakati hapa chanzo cha matatizo yote haya inafahamika ni ccm.
Kwa taarifa yako huwezi kutenganisha ccm na unacholalamikia hapa , chagua moja huwezi kutetea mabwana wawili kwa wakati mmoja kwenye hili suala.
"VUA GAMBA JIUNGE NA UKAWA UPINGE UBAGUZI NA VITISHO"
Faiza Foxy dada yangu kipenzi busara yashinda utumwa!
Hivi utasemaje wakristo wanausema Uislam wakati Lukuvi pale kanisani hakuenda kuhubiri kama mchungaji bali alipeleka salam za serikali? Mbona kajisemea mwenyewe alimwakilisha waziri mkuu?
I am a christian na kwa imani yangu ni dhambi tena ya mauti kumtendea mwenzangu nisichopenda mm kutendewa; hii ni amri kuu katika ukristo yaani kumpenda jirani kama ninavyojipenda mwenyewe.
Mkristo wa ukweli hawezi tumia mbinu yoyote ile kumnyima ibaada mwenzake kwa kitu anachokiamini. Dini ya ukristo haihitaji mtetezi maana Mungu wa ukristo anauwezo wa kugeuza nia ya mtu yeyote bila nguvu! Ni dhambi kwa ukristo kumkataza mtu kuchagua akipendacho. So tofautisha ukristo na individuals' selfishness!
Mimi ningetamani Zanzibar ikawa nchi ya kiislam ili mimi nitakapopiga magoti yangu chumbani kwangu, na kulituma neno Zanzibar injili ingehubiriwa bila mm kwenda Zanzibar na kwa jinsi hiyo Mungu wangu atakuwa amedhihirisha nguvu zake!
My father was a muslim ndugu zake wote walikuwa waislam. Baba yangu alibadili dini na alikuwa mkristo wa kwanza huko nitokako. Lakini aliweka sheria nyumbani kwetu asilazimishwe ndugu yake yeyote kubadili ama kuishi maisha kinyume na dini yao ya uislam. Chakushangaza hakuna ndugu yake hata mmoja leo aliye mwisilamu wote walibadili kwa hiari yao. Haikuwa abrupt ilichukua miaka zaidi ya 60. Zaidi ni kuwa kanisa alililianzisha leo jamii ile ya hiyo sehemu asilimia 90 ni wakristo.
Hivyo ninauhakika dini ya ukristo haihitaji nguvu bali kuna evidence wapo watu wanakubali kuifia tena kwa hiari siyo kwa manipulation.
So what I mean kwangu inakuwa heri sana kama Zanzibar ingeachwa na kuwa nchi ya uislam ili kwa huduma yetu Mungu ajitukuze mwenyewe Zanzibar bila maguvu wala shuruti!
So hao watu wanaoutumia ukristo kwa nia zao siyo wakristo ni wasaka tonge tu!
Professor Lipumba leo amesema anakwenda Zanzibar kuwaelezea wananchi kinachoendelea, nna uhakika mada kuu haitoliwacha hili la Lukuvi. Au unasemaje?
Anakwenda kushitaki kwa wananchi wa Zanzibar.
Mkuu,
Nimekusoma na nimependa kiduchu hiyo personal experience yako, uliyoamua ku-share nasi Watanzania wanzio!
I must admit it's so interesting!
Ahsanta sana!
Faiza Foxy dada yangu kipenzi busara yashinda utumwa!
Hivi utasemaje wakristo wanausema Uislam wakati Lukuvi pale kanisani hakuenda kuhubiri kama mchungaji bali alipeleka salam za serikali? Mbona kajisemea mwenyewe alimwakilisha waziri mkuu?
I am a christian na kwa imani yangu ni dhambi tena ya mauti kumtendea mwenzangu nisichopenda mm kutendewa; hii ni amri kuu katika ukristo yaani kumpenda jirani kama ninavyojipenda mwenyewe.
Mkristo wa ukweli hawezi tumia mbinu yoyote ile kumnyima ibaada mwenzake kwa kitu anachokiamini. Dini ya ukristo haihitaji mtetezi maana Mungu wa ukristo anauwezo wa kugeuza nia ya mtu yeyote bila nguvu! Ni dhambi kwa ukristo kumkataza mtu kuchagua akipendacho. So tofautisha ukristo na individuals' selfishness!
Mimi ningetamani Zanzibar ikawa nchi ya kiislam ili mimi nitakapopiga magoti yangu chumbani kwangu, na kulituma neno Zanzibar injili ingehubiriwa bila mm kwenda Zanzibar na kwa jinsi hiyo Mungu wangu atakuwa amedhihirisha nguvu zake!
My father was a muslim ndugu zake wote walikuwa waislam. Baba yangu alibadili dini na alikuwa mkristo wa kwanza huko nitokako. Lakini aliweka sheria nyumbani kwetu asilazimishwe ndugu yake yeyote kubadili ama kuishi maisha kinyume na dini yao ya uislam. Chakushangaza hakuna ndugu yake hata mmoja leo aliye mwisilamu wote walibadili kwa hiari yao. Haikuwa abrupt ilichukua miaka zaidi ya 60. Zaidi ni kuwa kanisa alililianzisha leo jamii ile ya hiyo sehemu asilimia 90 ni wakristo.
Hivyo ninauhakika dini ya ukristo haihitaji nguvu bali kuna evidence wapo watu wanakubali kuifia tena kwa hiari siyo kwa manipulation.
So what I mean kwangu inakuwa heri sana kama Zanzibar ingeachwa na kuwa nchi ya uislam ili kwa huduma yetu Mungu ajitukuze mwenyewe Zanzibar bila maguvu wala shuruti!
So hao watu wanaoutumia ukristo kwa nia zao siyo wakristo ni wasaka tonge tu!
Hapa kinacho leta tabu sana sio maneno tuu ya Lukuvi.Bali ni mahala alipo kwenda kuyatolea maneno hayo. Ukisikiliza maneno yenyewe ni ya uchechezi wa dini mbili kubwa ktk Jamhuri yetu .
Mbaya zaidi amekwenda kumuwakilisha PM kwahiyo hakwenda pale kama Lukuvi tu na hakuenda pale binafsi kaenda akiwa anaiwakilisha Serikali ya Jamhuri. Laiti maneno yale angeyatamka pale mjengoni tungesema anawachonganisha waislam na vyombo vya usalama na wanao taka muundo tofauti na muundo wa serikali 2.
Mm namuona Lukuvi ni mtu anae uchukia uislam ingawa chuki zake sio kwa faida na maslahi ya ukiristo nathubutu kusema chuki zake ni kwa maslahi na utashi wake binafsi.nataka niamini hana imani na chama chake kushinda ktk muundo wa muungano wa ainayeyote tofauti na huu uliopo. Ndio maana anajaribi kutuchonganisha kwa kutumia dini zetu.chakusikitisha huyo mchungaji aliekuwa anapewa uaaskofu mdu mfupi tu ameamini maneno ya Lukuvi na akatoa jibu hapo hapo.
Kabla ya kutoka bungeni baadhi ya wabunge wa UKAWA jana, Professor Lipumba aliweka wazi aliyoyaongea kanisani waziri mmoja wa Serikali ya Muungano. Lipumba alisema kuna waziri kaenda kuhutubia kanisani kuwa "ikiwa Zanzibar itapewa mamlaka kamili basi mjuwe itaanzisha dola ya Kiislam".
Jana nikauliza ni waziri gani huyo? sikupata jibu humu JF.
Lakini kwa kuwa Mungu hamfichi mnafik, huyo waziri kajitokeza mwenyewe bungeni leo hii na kwanza kukiri kuwa katumwa na Waziri Mkuu na kusema kuwa hiyo ni hofu, "phobia" yake na akaendelea kusema "hakuna yeyote wa kunizuia hofu yangu hii".
Akazunguka wee na maneno lakini akashindwa kukisema kile alichokieleza Lipumba.
Kwa uchache, Lukuvi ameudhihirishia umma kuwa ana "Islamophobia" au hofu ya Uislaam.
Kiongozi unaefikia kutangaza Kanisani na Bungeni kuwa hutaki kuwapa mamlaka kamili Zanzibar kwa ajili ya dini yao, kweli hiyo si Serikali ya Mfumo Kristo tunayoilalamikia siku zote humu?
Na leo Lukuvi kahitimisha kwa kuniunga mkono yale ninayoyasema humu kila siku kuwa huu Muungano upo kwa ajili ya Kanisa. Na unaongozwa na Kanisa. Huwa mnajifanya hamnielewi lakini leo yamebainika bayana.
Wanaonisikitisha zaidi ni wale Wazanzibari waliobaki kuipigia makofi hoja hii ya Lukuvi, halafu wanajiita wao Waislaam. Waislaam mnaambiwa hampewi nchi yenu kwa kuwa Lukuvi ana hofu mkipewa mtaifanya dola ya Kiislaam na nyinyi mnashangilia? Yaani Lukuvi anawaambia kinaga ubaga kuwa mtabaki ndani ya mfuko Kristo mkitaka msitake na mkikataa basi ni bora nchi hii ishikwe na jeshi na akafikia mpaka kuwapa mfano wa Islamic Brotherhood ya Egypt.
Kinachonishangaza hii hofu yanini kwa Lukuvi? ikiwa nchi anayoiongelea ni Zanzibar na Wazanzibari 99% ni Waislaam ikiwa
wataamuwa nchi yao kuwa ya Kiislaam yeye anapatwa na hofu ya nini?
[video=youtube_share;PIAPAAd3Dck]http://youtu.be/PIAPAAd3Dck[/video]
cc Ritz, gombesugu, kahtaan, THE BIG SHOW, CHAMVIGA
Moderator tafadhali usiiunganishe hii na nyuzi nyingine hii maudhui yake inajitegemea.