Lulu amtusi mama yake Kanumba, amuita KUBWA JINGA

Lulu amtusi mama yake Kanumba, amuita KUBWA JINGA

Hajafanya vizuri Lulu, ila mama Kanumba pia aachane tu na hako katoto maisha yaendelee
 
Mimi sio shabiki wa huyo Lulu. Kwa nini huyo mama kila siku ni kulalamika tu? Au alitaka Lulu awe anamnyenyekea kwa kila kitu? Kuishi kwa kutegemea posho za magazeti ya Shigongo ni ujinga
 
Ila Tanzania ina maboya wengi sana, mpaka leo hii mnaamini magazeti ya Shigongo? Au mpaka siku waje waandikwe wazazi wenu ndio mtaona wanatunga ili wauze?

Wakiandika lulu anautajiri wa bilioni moja itapingwa vikali sana kuwa ni uongo, ila habari ya kimbea namna hii inaaminika kirahisi sana...

71%
Asilani sitaki kusikia magazeti ya Shigongo wala Shibangi.
 
Diana-Elizabeth-Michael-Lulu2.jpg

KITENDO cha muigizaji wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, kutoa maneno ya kumtusi mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa, ni dalili za msichana huyo kuitafuta laana.

Hivi karibuni, mama Kanumba aliliambia gazeti moja nchini kuwa tabia ya mpenzi huyo wa zamani wa mwanaye imebadilika sana na kukosa maadili, kiasi cha kumuita yeye kuwa ni kubwa jinga.

“Sielewi jambo gani limemtokea huyo binti mpaka kufikia hatua ya kuniita mimi kubwa jinga, lakini yote namwachia Mungu maana anajua anachokifanya,” alisema mama huyo huku akionekana kulengwa na machozi.

Kwa upande wake, alipoulizwa kuhusu kutoa kauli nzito kwa mama huyo, Lulu alijibu kwa nyodo na kusema hapendi kumzungumzia chochote kwani siyo staili yake kuzungumzia mambo ya wengine katika vyombo vya habari.

“Kama yeye amesema hivyo kwenye vyombo vya habari ni staili yake, mimi staili yangu ni ya kukaa kimya, sitaki kabisa kumzungumzia huyo mama,” alisema Lulu.

Naona huyu dogo umaarufu unaanza kumpa kichwa, anaanza kuvuka redline.

Source: Gazeti letu pendwa
Ila haka kabinti ni kiburi, kiburi kitupu hata uso wake unaonyesha hivyo.
 
wakati lulu ana mahusiano ya kimapenzi na kanumba ilikuwa siri kiasi kwamba ht mama kanumba hakujua ila baada ya lulu kutoka rumande ushoga ghafla ukaibuka kati ya lulu na huyo mama nilikuwa najiuliza wanazungumza nini mtu na mjukuu wake!!kitu km hicho nilikitegemea
 
Huyo mama nae arudi kijijini tu, huku mjini hapamtoshi
Nakumbuka alivyokuwa anagida mayi kipindi kileee wakati ndo mwanaye amefari na kumtolea maneno ya kashfa Baba Kanumba, ila ni kweli alitegemea Lulu atamsaidia kimaisha lakini Lulu anamkwepa.
 
Walimtumia huyu mama kumsafisha lulu kipindi ambacho kila mtu alikua na hasira nae ila yameisha leo anamuita huyo mama, lazima mama wa watu aumie katumika na kuachwa
 
Hivi kesi yake imeishaje bado mtuhumiwa huyu mtoto asie na nidham
 
Bado natutafuta kosa la Lulu sijaliona mtu akiliona anishtue
 
Diana-Elizabeth-Michael-Lulu2.jpg

KITENDO cha muigizaji wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, kutoa maneno ya kumtusi mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa, ni dalili za msichana huyo kuitafuta laana.

Hivi karibuni, mama Kanumba aliliambia gazeti moja nchini kuwa tabia ya mpenzi huyo wa zamani wa mwanaye imebadilika sana na kukosa maadili, kiasi cha kumuita yeye kuwa ni kubwa jinga.

“Sielewi jambo gani limemtokea huyo binti mpaka kufikia hatua ya kuniita mimi kubwa jinga, lakini yote namwachia Mungu maana anajua anachokifanya,” alisema mama huyo huku akionekana kulengwa na machozi.

Kwa upande wake, alipoulizwa kuhusu kutoa kauli nzito kwa mama huyo, Lulu alijibu kwa nyodo na kusema hapendi kumzungumzia chochote kwani siyo staili yake kuzungumzia mambo ya wengine katika vyombo vya habari.

“Kama yeye amesema hivyo kwenye vyombo vya habari ni staili yake, mimi staili yangu ni ya kukaa kimya, sitaki kabisa kumzungumzia huyo mama,” alisema Lulu.

Naona huyu dogo umaarufu unaanza kumpa kichwa, anaanza kuvuka redline.
Hivyo ile kesi iliishaje?
 
Mpaka leoo najiulizagaa Kanumbaa Alitelezaaa alisukumwaa au alikufaa kwa wivuu Wa kimapenziii..turudii nyumaa Kanumba kutembeaa Na Katotoo ni kosa..Mungu Akamwadhibuuu kwa kufichuaa yaliyokuwaaa mafichoni...tungejuajeeee
 
Waandishi wanaume wa magazeti ya Shigongo wanakilisha wanaume wa Dar. Ila hii mbona ni story tu kama story zingine za Wema kununua nyumba ya mil 400. Huyo mama mbona hajatoa ushahidi wowote kwa waandishi..? Na waandishi wanaandikaje bila kuwa na ushahidi..?
 
Mimi ningekua mama Kanumba Lulu nisingemuacha nisingeweza kua mnafiki huku moyo unauma
Hata mimi aisee yani, alitakiwa ale nae sahani moja ili apate haki ya mwanawe, nina uhakika hata hajui what happened in that room, on that day, yaani eti akawa urafiki na mtu anayehusika na kifo cha mwanae, hapo alibuug step.Aangekomaa lazima lulu angekula miaka kadhaa jela.
 
Back
Top Bottom