Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ninahisi huko mahabusu alikuwa salama zaidi kuliko atakavyokuwa uraiani...
Just thinking....
Ni Kanumba, sio Manumba. RekebishaLulu hakuua ni udhaifu wa hayati manumba kutojua mbinu za upelelezi.
Namaanisha yule mukubwa wa wapelelezi hapa mujini bongo mkuuNi Kanumba, sio Manumba. Rekebisha
Mimi naona wagambo gambo wa magereza wanauza sura tu hapa!![]()
Habari zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa Mahakama kuu ya Tanzania imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael aka Lulu aliyekuwa mahabusu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.
Wiki iliyopita mawakili wa muigizaji huyo waliwasilisha maombi ya dhamana kwa mahakama hiyo kuu ya Tanzania.
Wanasheria hao Peter Kibatala, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe waliomba dhamana hiyo itolewe haraka kwakuwa muombaji amekaa mahabusu kwa zaidi ya miezi saba na kwamba kosa lake linaweza kupewa dhamana.
Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia Steven Kanumba April 7, 2012, huko Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam.
Kanumba alidaiwa kuwa kwenye ugomvi na Lulu aliyekuwa mpenzi wake nyumbani kwake Sinza.
SOURCE: ITV
UPDATES:
- Sasa ndio wanakagua documents za wadhamini mahakamani...
- Kuna mambo hayajakamilika hivyo anarudi jela, hadi kesho...
FINAL UPDATE (03:00 PM, 28, Jan, 2013)
Lulu hajaachiwa, atarudishwa mahakamani kesho kwakuwa Msajili wa Mahakama Kuu hakuwepo na hii ilikuwa ni kesi ya 'Kuua bila kukusudia'.
Kesho wadhamini watawasilisha nyaraka zao mbele ya msajili ndipo anaweza kuachiwa...
Tutawafahamisha kitachojiri mahakamani kesho
![]()
It will take her only three months to forget, and she will go back to square one.
yuko sahihi wewe ndio hujui mpelelezi anaitwa manumba hahahahahahani kanumba, sio manumba. Rekebisha