Lulu (Elizabeth Michael) kuachiwa kwa dhamana

Lulu (Elizabeth Michael) kuachiwa kwa dhamana

We are learning thru mistakes.Kama ni somo limeingia kchwani.Chezea maabusu weweee...
 
Jamani nina kaswali kamoja tu, mlijuaje ameua bila kukusudia ili hali walikuwa peke yao chumbani?
nani atuhakikishie kuwa akiwa bila kukusudia? Je angekuwa kabwela wa huko vijijini sitimbi hii kesi ingesomeka hivo?
 
Huyu mtoto naamini sasa amejifunza maisha ,namshauri amrudie Mungu na ikiwezekana sasa aanze kufanya kazi zitakazompa Mungu utukufu na awe na ushuhuda wa maisha yake alivyokuwa mahabusu ili jamii itambue hali ya magereza yetu ilivyo,Swla
la hukumu naiachia mahakama lakini pia naamini mahakama itamtendea haki kwa vile shitaka lake siyo na kukusudia na vile vile inawezekana umri wake ulichangia yote yaliyotokea.
 
Enyi mawakili mliomtetea Lulu sidhani kama kazi hiyo mumeifanya kwa moyo wa uzalendo kama hakuna kilicho nyuma ya pazia,kwanini nasema hivyo,wako wengi sana wanapata shida,wanasota kwa kukosa msaada na wana kesi kama hiyo ya Lulu kuna matabaka ya watu hapa Tanzania ambao wako juu ya sheria,tumeona mfano wa Lulu na Ditopile wao kesi zao zimeshughulikiwa kwa haraka na suluhisho kupatikana wakati wako watu ambao wanayo zaidi ya miaka 5 hawana dalili ya kutoka huko gerezani simply hawana fedha au hawana wa kuwasemea kwenye jamii inayotuzunguka,tuna create matabaka kati ya watanzania nna dhambi hiyo haitatuacha itatutafuna sana kwani tayari kuna pengo la walio nacho na wasiokuwa nacho na ambao wako juu ya sheria na walio chini ya sheria ambao kesi zao ni rahisi kubadilishwa kutoka kuua na kuua bila kukusudia sababu wanauwezo,Ole wao masikini na wasiokuwa na kitu Tanzania utakoma
 
Jamani nina kaswali kamoja tu, mlijuaje ameua bila kukusudia ili hali walikuwa peke yao chumbani?
nani atuhakikishie kuwa aliua bila kukusudia? Je angekuwa kabwela wa huko vijijini sitimbi hii kesi ingesomeka hivo?

hapa wanasheria naomba watusaidie 7bu hii nilidhani inanisumbua mimi mwenyewe! Pia majibu ya hospitali (postmortem) yanambeba huyu mtoto!
 
Haiwezi kuwa mali ya mahakama ashinde asishinde anarudishiwa.Hiyo inakuwa mahakamani kama endapo akitoroka ndiyo inakuwa sehemu ya malipo ya mlalamikaji/mahakama.

725-800x600.jpg
196381_603336873014068_845533663_n.jpg

MKATA KIU ukisikia kuwekewa dhamana mahakamani kwa kumdhamini Mtuhumiwa akae nje kwa dhamana ni kuwa hiyo Hela haitolewi hapohapo ila km akishindwa kutokea mahakamani ndipo Mdhamini itabidi atoe hizo milioni 20 ili zikamtafute Mshtakiwa (LULU) na wala sio malipo kwa Mlalamikaji au Mahakama
Na huenda wewe Mdhamini ukafungwa miezi 6 km hiyo hela huna au huna hiyo nyumba mpaka mtuhumiwa aletwe
Navyofahamu hela inayotolewa Mahakamani ni zile za madai na faini, lakini hela za dhamana zinawekwa na kesi ikiisha unarudishiwa du sijakutana nayo labda Mahakama za mwanzo
 
Last edited by a moderator:
Nimepata bahati ya kuona clip ya mahojiano mafupi kati ya msanii Elizabeth Michael (Lulu) na waandishi wa habari yaliyofanyika leo mahakamani alipokuja kujua hatma ya dhamana yake.
Kilichonikera na kunishangaza sana ni maneno aliyoyatumia huyu binti. Eti anasema amemiss red capet. Kauli hii imenikera sana kwani kwa mambo yaliyojitokeza na mazingira yanayomzunguka sikutegemea aseme kitu kama hiki.
Nilitegemea amshukuru Mungu kwa kumsaidia na aoneshe kuumizwa na kilichotokea, lakini wapi, haka katoto kanawaza starehe tu.
She hasnt learnt anything at all!
 
Hako kana pepo la ngono hakawezi acha. Hawa mawakili wamekuja kuchafua hali ya hewa tena kaue mwingine.
 
dah nilimsikia anaongea na waandishi wa habari nikasema hapa hakuna mtu.eti haaa red carpet nitashindwa sijapita muda mrefu kwenye mared carpet ..nikajisemea hapa kwisha habari yake..labda tuendelee kumuombea
 
Namuombea Lulu aweze kuepushiwa Kikombe Hicho. Bado ni mdogo na hakika nadhani kama ni bahati mbaya ambayo hatasahau ni hili tukio la 2012. Bila shaka mahakama inatenda haki kwani hapo ilipofikia wameona ukweli, namuombea Lulu aweze kuwa huru jamani.
 
Haruhusiwi kusafiri kwenda kokote, hata mkuranga tu haruhusiwi, yeye ni wa dar tu hadi kesi itakapoisha

Akina Ruge na Shigongo washapata dili.

Watatulipisha viingilio kwenda kumuona Dar live na ziara za mikoani.
 
Haruhusiwi kusafiri kwenda kokote, hata mkuranga tu haruhusiwi, yeye ni wa dar tu hadi kesi itakapoisha

Basi andaa kiingilio cha dar live na mlimani city siku ya miss tz.
 
Back
Top Bottom