Kutoka jasho ni njia mojawapo ambayo Mungu ameiweka ili mwili uwe unatoa sumu mwilini na kuweka mifumo ya mwili sawasawa! Sasa kwanini upake makemikali ya kuzuia jasho isitoke? Je unajua kufanya hivyo Kwa muda muda mrefu huwa kuna madhara? Tafakali na uchukue hatua! Njia nzuri ya kufanya ili kuepuka jasho lenye harufu ni kuoga vizuri, kupaka sabuni na kujisugua vizuri makwapani na kuhakikisha unasugua makwapani Kwa povu la sabuni na kujisuuza kisha paka tena sabuni sugua na kujisuuza nakwambia Hata jasho itoke vipi haitakuwa na harufu ya ajabu! Hata mapafyumu siyo mazuri ni kemikali zile, Hata manukato ya kuweka Kwenye Magari na spray za bafuni na Ofisini zote hazifai Kwa wenye uelewa na wenye kujali! Yani nikaanza kijadili kiundani wengi watanishangaa na kuniuliza Kwa hiyo inakuwaje [emoji87][emoji87][emoji87] kila Mtu afanye anavyoona ni vyema!