Lulu sasa abadilishiwa mashtaka

chezeni na bustani ya eden inatisha sana. pili marehem huwa hana haki daima
 
Tanzania bado kuna utamaduni wa kuwabagua wanawake. Kama huyu dada angekuwa mwanaume wa yule Actor angekuwa mwanamke kusingekuwa na kesi na watu wangemuana kijana kama ni mdogo. Hatujui kilichotokea je kuna ulevi na kupigana ulikuwepo?, kama kuli kuwa na ulevi je nani alikuwa amelewa, kulikuwa kuna kupigana?,. Vitu vyote hivi ni vya msingi na kama kulikuwa na ulevi na kupigana itakuwa vigumu kusema msichana wa miaka 18 anaweza kupigana na kumpiga mwanaume wa miaka 26 au 27 labda awe amelewa. Vilevile labda huyu dada alitumia silaha kujihami kama kisu au gongo baada ya kupigwa vilevile kutakuwa hakuna kesi.
 
kanumba angekuwa ndugu yenu mngejadili kwa utulivu huu,hapa hakuna hata mmoja anayejua ukweli,lulu aweza kuwa na hatia au asiwe nayo.

Hujui kazi za mahakama wala waendesha mashitaka..
Kujaribu kukuelimisha,ni kujitafutia sononi na jioni mbaya ya leo..
 
Ni ajabu sana kwa uzi huu kukaa hapa ukiwa unaelezea sheria bila hata kutaja kifungu kimoja cha sheria na element za offence, soma PENAL CODE vilevile kasome vizuri CRIMINAL PROCEDUREA ACT pamoja na National Prosecution Act. labda kwa kukusaidia tuu soma section 195 na 196 of the PENAL CODE CAP 16. Ukitaka kumulamu mwanasheria tumia vifungu vya sheria ambavyo amekiuka.

kama unasema DPP haruhusiwi kuinstitute case ya manaslaughter tupe kifungu au precedent(cases) za kufuata.
 
Una uhakika na hilo?

Kuna kesi nyingi tu za manslaughter kwa TZ. Hiyo kuua bila kukusudia inaweza ikawasilishwa na DPP kama kwenye hii au wakati wanasikiliza kesi ya kuua, upande wa mshitakiwa unaweza kuamua kukana kosa la kuua lakini kukubali kosa la kuua bila kukusudia. Upande wa mwanasheria mkuu wakikubaliana na hilo basi inakuwa kesi ya kuua bila kukusudia.

Haiwezekani DPP akashitaki kesi kama murder halafu eti hakimu baadaye aseme sio murder ila ni manslaughter. Ukishindwa ku prove murder mshitakiwa anaachiwa.
mkuu, hakuna shitaka la kuua bila kukusudia! Ila mahakama baada ya kupelekewa kesi ya mauaji. Hupunguza kosa 'mudder' kuwa 'manslaughter'. Huwezi kupeleka 'manslaughter' km kosa mahakamani. Sijawahi ona zaidi ya kesi ya uncle Dito na hii hapa.
 

Prosecutorial discretion!
 
Hivi nayo hii ni siasa au kichwa changu kimefeli kuchanganua au sipo jukwaa la siasa
 
Don-Oba,

Upo NAÏVE sana na inawezekana hata sheria moja ya nchi hii hujui.

Lipo shitaka la kuua bila kusudia. Manslaughter.

Ukimshtaki mtu mahakamani kwa kosa la kuua kwa kusudia, Murder, ikagundulika aliua bila kukusudia, manslaughter ina maana anaachiwa huru.

Mahakama haiwezi kutunga shitaka.
Kama DPP hana ushahidi hawezi kukushtaki.

Mfano, umeshitakiwa kwa kosa la kuiba. Ushaidi ukaonyesha kua haukuiba bali ULIPIGA, ingawa kupiga mtu ni kosa, mahakama haiwezi kukuhukumu kwa kosa ambalo haukushtakiwa nalo. Hivyo inakuacha huru.

Ndio hilo alilofanya DPP.

Wabongo muwe mnasoma na msiwe wavivu wa kufikiri na mbilikimo wa mawazo.

Je umewahi kujiuliza kwanini marehemu alikua anatembea na mtoto chini ya miaka 18?. Marehemu alikua akimbaka. Ndio maana yake.
 
Lulu. Mmm! Mara miaka 18 mara 17. Usikute hata gerezani hayupo
 

Mkuu FairPlayer,
Hawa vijana wa fasta fasta huwa hawataki kusema hawajui na wakaamua kujifunza. Badala yake wanapasiana ujinga na mwisho jamii yote inajaa wajinga tu.

Hili jambo hata uki google tu unapata ukweli haraka na kuna mifano mingi lakini Mungu wangu vijana wanakuja na hitimisho utafikiri wanajua ukweli kumbe wako nje ile mbaya.
 
Kuuwa bila kukusudia kuna mpa mtu dhamana ya kuwa nje ya mahabusu, next visit ya Lulu mahakamani ni dhamana tu, mambo mengine baadae.
 
Hivi Director of Public Prosecuter (DPP) si ni yule nanihii, Elieza Feleshi? au tayari JK kambadilisha maana hachelewi kufanya yajukanayo kama maamuzi magumu"maamuzi magumu"[QUOTE=don-oba;5247041]Vichwa vya magazeti habari kubwa ya leo ni kwa msanii wa filamu nchini Lulu kubadilishiwa mashtaka kutoka kuua kwa kukusudia hadi kuua bila kukusudia.

Wanajamii, DPP kwa kufanya hivo tayari ameishatoa hukumu kwa mtuhumiwa. Hili suala lipo beyond judicial descretion power. Mahakama ndiyo yenye power ya kutafiti km mtuhumiwa aliua kwa kukusudia ama la.

Tunavyopeleka mashtaka mahakamani ya mauaji huwa hakuna shitaka la kuua bila kukusudia "manslaughter". Je ikitokea ushahidi ukapatikana mahakamani kwamba Lulu aliua kwa kukusudia! Sina haja hapa ya kumkandamiza Lulu ila napinga ukiukaji wa sheria alioufanya DPP. Huu ni ukiukwaji wa utawala wa sheria.

Ni ukiukwaji pia pale watendaji wa serikali wanapoingilia mamlaka za mahakama.[/QUOTE]
 
Tatizo ni sheria zetu tulizo rithi kutoka kwa mkoloni bila kujua madhara yake,
therefore is a gud chance that tupo kwenye mchakato wa katiba mpya so
tunahitaji mabadiliko ya kisheria mpaka huko mahakamani.
 

Mkuu Mtanzania,

Hofu yangu ni jamii hii tulionao. Jamii isiojua kitu jamii inayofanya Tanzania iwe ilipo.

Ni hali mbaya sana kwa nchi. Hata mabadiliko ya kimaendeleo tunayotaka hayatapatikana daima tukiwa na watu kama mleta mada.

Hali ni mbaya. Na mbaya zaidi ana watu wanamsapoti. Vita vya internet tulivyoanza miaka mingi vya kuleta maendeleo Tanzania vinaharibiwa na wababaishaji kama mleta mada. We no longer speak the same language kaka.

Enzi zileee wenye access na NET walikua wana ueledi na waelewa. Sikuhizi hata mtoto wa Nusery kama mleta mada naye ana access!!

Taifa bovu linaendelea. Na ndio viongozi wetu hao wajao maana wazee tunaishia!!

Naonea huruma Tanzania yangu.
 
Nimeelewa hayo mawazo yako nami nayaunga mkono.kama unasema ni ukiukwaji basi nenda katupe ushahidi jinsi alivyomuua mwenzake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…