Lulu sasa abadilishiwa mashtaka

Lulu sasa abadilishiwa mashtaka

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Msanii Elizabeth Michael, maarufu kama Lulu (Hot Lulu), ameepuka adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa tuhuma za kumuua msanii mwezake, R.I.P Steven Kanumba baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kumbadilishia mashtaka, ambapo sasa anatuhumiwa kuua bila kukusudia.

Kutokana na mabadiliko hayo, Lulu ameepuka adhabu hiyo ya kunyongwa hadi kufa, hata kama atapatikana na hatia, adhabu yake ni kifungo cha maisha au kuachiwa huru.

Source: Gazeti la Mwananchi la Jumanne 18, Desemba 2012
 
hajaepuka adhabu ya kunyongwa, hajawahi kuwa convicted.

Magazeti yetu yanatuandikia madudu.

Hajaepuka adhabu ya kunyongwa, kwa sababu hajawahi kuadhibiwa kunyongwa. Na wala hakuwa na nafasi ya nasibu kubwa ya kunyongwa.

Ameepuka mustakabali wa kunyongwa.

Sijui kama kuna kutanabahisha tofauti ya mustakabali na adhabu katika uandishi wetu.
 
Pole zake nyingi, hata akiachiwa atakuwa keshasota vya kutosha.
 
Ndiyo maana kuna baadhi ya wapinzani wanasema majaji wengi wa Kikwete ni vilaza. Utamfunguliaje mtu mashitaka kama hakuna ushahidi tosha? Bongo hii, tunaishi basi tu.
 
Wamwache mtoto akanyweshee jangwa. Jangwa limezidiwa na ukame town.
 
Sioni kufungwa mtu maisha au kunyongwa hapa.....I just feel
 
Sioni kufungwa mtu maisha au kunyongwa hapa.....I just feel
Kwa nchi za wenzetu nadhani angeachiwa huru kabisa , maana wenzetu huwa hawana muda wa kuendesha kesi za kusadikika zisizo na ushahidi kama hii ya Lulu ambayo mwisho wa kesi hii hukumu yake itakuwa Lulu kuachiwa huru.

Sasa hivi na swala la muda kujuwa Lulu ni lini ataachiwa na Mahakama Kuu, kwa mfumo wa Tanzania kuuwa bila kukusudia wala siyo kesi ndio maana Ditopile walimsevu kumpa hii hili baadaye ashinde wakati ukweli ni kwamba Ditopile aliuwa kwa kukusudia.
 
Japo namuonea huruma, lakini mnakumbuka wanajeshi watatu waliohukumiwa kifo kwa kuhisiwa wamemuua mtoto wa Fundikira kama mwezi umepita sasa? Walikuwa ni watu wa mwisho kuwa na marehemu na hakukuwa na evidence concrete zaidi ya hiyo. Mimi sio mwanasheria, lakini tunayaona sana hayo.
 
Pole sana Lulu,yaliyokukuta ni mazito ila shukuru Mungu ana makusudi kwa kila jambo!Mrudie Mungu wako nae atatenda!ndio lililobakia!
 
hajaepuka adhabu ya kunyongwa, hajawahi kuwa convicted.

Magazeti yetu yanatuandikia madudu.

tatizo hatuna waandishi waliobobea kwenye sheria hata akipatikana na hatia ya kuua bila kukusudia hawezi kufungwa maisha..nashauri wasome penal codes.
 
Japo namuonea huruma, lakini mnakumbuka wanajeshi watatu waliohukumiwa kifo kwa kuhisiwa wamemuua mtoto wa Fundikira kama mwezi umepita sasa? Walikuwa ni watu wa mwisho kuwa na marehemu na hakukuwa na evidence concrete zaidi ya hiyo. Mimi sio mwanasheria, lakini tunayaona sana hayo.

wewe naona ni bora ukae kimya maana inaonekana huna taarifa za kutosha au hukufatilia kwa makini sakata lenyewe wala kesi yenyewe!
 
Back
Top Bottom