Lumumba, Dar: Mzee Kinana na Mzee Makamba waitikia wito Kamati ya Maadili ya CCM

Lumumba, Dar: Mzee Kinana na Mzee Makamba waitikia wito Kamati ya Maadili ya CCM

Mmoja yupo kwenye gari na mwingine kaingia ndani na wote wametupa mashati ya CCM. Halafu kamati gani ya maadili ya watu wanne? Walikuwa na mishemishe zao naona wakaamua kupitia hapo kunywa kahawa ila kimsingi mumefeli kwenye hii movie.


Unareason kama mtoto, jaribu kuishi umri wako ingawaje siujui lkn nina uhakika uko > 25!
 
johnthebaptist, Acha uongo wazee wameripoti Lumumba au White house ipo Dar
Screenshot_20200210-231621_Twitter.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Double Standard ni pale mtu (ambae hapendiwi au asiekua na madaraka) akifanya jambo fulani basi ni "KOSA", ila jambo hilo hilo likifanywa na mtu anaependwa/mwenye madaraka "SIO KOSA".

Mfano, Chama tawala kufanya kampeni kabla ya muda au kufanya vikao vya hadhara sio kosa, ila vyama vya upinzani kufanya hayo ni kosa.
SASA UME SAIDIA WALE WANA OTUMIA HILO NENO KIMAKOSA.
 
kumbe alienda kikaoni mwanajeshi ameacha msimamo wake?
Siasa zinaboa....
Leo mnamsifu hatoenda kesho wamezingua wanaenda
Picha inajieleza kuna tatizo. Mzee Makamba ni kama vile anasisitiza msimamo na kumwambia Bashiru "Nyie endeleeni na chama chenu" na Bashiru anaonekana kumsihi Makamba abadili msimamo na kubaki kwenye chama.
View attachment 1353738

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usikute bado posho zao za kikao walilipana!
Ni haki yao.Kikao kina posho kikatiba.Sitting Allowance.Mikono wamenyoosha wakapokea mshiko na kurudi nyumbani siku mbili bila kikao.Hii ni sawa sawa na kusubiri lift ambayo hujui itatokea wakati gani.
 
HII NI KWA WENYE AKILI TU!

KUNA tofauti kubwa kati ya kuitikia wito wa kuhojiwa kwenye Kamati ya Nidhamu na kuitikia wito wa kuzungumza ili kuyamaliza kiutu uzima.

Komredi Abdulrahman Kinana na Mwalimu Yusuf Makamba waliitikia wito leo, Lumumba, Dar es Salaam kwenye ofisi ndogo ya Makao Makuu CCM.

Ni baada ya Ijumaa kutokwenda kwenye kikao cha Kamati ya Nidhamu ili kusomewa tuhuma zao na kujieleza, Makao Makuu, Dodoma.

Swali 1; kwa nini hawakwenda Dodoma Ijumaa?

Swali 2; kwa nini kikao cha leo kimefanyika Dar?

Swali 3; Makamba na Kinana waliona Dodoma mbali?

Swali 4; Nini kimewashawishi kuitikia wito leo baada ya kugoma Ijumaa?

Swali 5; Lugha gani ilitumika kujenga wito wa Ijumaa ambao ulifeli na maneno yapi yaliyotumika kufanikisha wito wa leo?

Swali 6; Makamba na Kinana waliitikia wito kama watuhumiwa wanaomhujumu na kumteta Rais Magufuli, au waliitikia wito kama wastaafu wenye hasira baada ya kuchafuliwa?

Swali 7; Agenda ya kikao cha leo ilikuwa nini? Je, tuhuma za kumhujumu Rais au kuzungumza ili kuyamaliza kiutu uzima?

Swali 8; Mbona picha hazizungumzi kikao? Kinana anaonekana kwenye kikao na Mangula, Dk Bashiru na wajumbe wengine wawili lakini Makamba yeye kwenye gari, Dk Bashiru akizungumza naye dirishani?

Swali 9; Picha ya Makamba akiwa kikaoni mbona haijaoneshwa? Picha ya Kinana akiwa anaongea (kuagwa) na Dk Bashiru kwenye gari mbona haipo? Au mpigapicha alichagua kila mmoja ampige na location yake?

Swali 10; Makamba na Kinana waliingia kwenye kikao kimoja au kila mmoja alikuwa na cha kwake?

Swali 11; ni marudio, je, agenda ya kikao ilikuwa tuhuma za kumhujumu na kumsengenya Rais kama walivyodukuliwa kwenye simu zao au ilikuwa kukutana na kuzungumza ili kuyamaliza kiutu uzima?

Zingatia; kuna tofauti kubwa kati ya kuitikia wito wa kuhojiwa kwenye Kamati ya Nidhamu na kuitikia wito wa kukutana kuzungumza ili kuyamaliza kiutu uzima.

Nasisitiza; hii ni kwa wenye akili tu. Kama unajiona huna akili, tafadhali, yapo mambo mengi yanakuhusu lakini sio hii post.

Ameandika Luqman MALOTO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinana na Makamba wameitikia wito kutoka kwa Wazee wenzao akina Mangula-Busara ya juu kabisa.
Kuitikia wito kuliwapa nafasi ya kueleza ya moyoni tofauti na kudhalilishwa na vijana wa UVCCM Dodoma.

Kinana na Makamba wana hoja nzito. Walipochafuliwa Chama kinachowaita leo ''kuyamaliza'' kilikuwa kimya

Walikaa kimya wakitegemea wapo watakaojitokeza kuzungumzia kadhia zao kutoka ndani ya chama. Kimyaa
Wakaandika barua kueleza madhila yao kwa baraza la Wazee

Walifanya hivyo kwa kujua kuwa barua kwenda kwa uongozi wa Lumumba uliojaa uvccm ni kujidhalilisha na haitawasaidia katika tatizo lao. Wakaomba wazee wenzao wasaidie

Ghafla uvccm wakaiuchukua hoja na kupitisha azimio la kuwaita Dodoma ili kuwakaanga.
Hata kama wangekuwa na hoja mwisho wa siku wangepewa onyo jambo ambalo ni udhalilisha.

Wao kama walalamikaji wakageuzwa kuwa watuhumiwa

CCM wajiulize walikuwa wapi wakati wazee hao ''wakidhalilishwa''?
Nini kosa lao katika kadhia nzima ya suala hili?
Leo wanawahitaji kwa lipi ikiwa hawakuweza kusimama nao wakati wanachafuliwa?

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Nasisitiza; hii ni kwa wenye akili tu. Kama unajiona huna akili, tafadhali, yapo mambo mengi yanakuhusu lakini sio hii post.
Na ubaya ni kwamba michango kama huu wako ni wachache sana humu JF wanaoupa nafasi kuusoma na kuyafikiri yaliyoandikwa ndani yake kwa kina.

Kwa kuwaza kati ya hayo maswali uliyoweka hapa, ni wazi

- wazee waligoma kwenda Dodoma

- ni wazi juhudi kubwa zilifanywa kuwatafuta wazee popote walipo

- ikatengenezwa 'movie' angalao ionekane wazee wameitikia wito. Hii ni kuwachota akili wasiotaka kuzitumia akili hizo kufikiri
Lakini, hata makada waliomo humu ndani ya JF, naona kama 'movie' hii haikutosha kuwachota akili zao na kuanza kuwika.

Ukweli utakuwa kwamba hawa wazee ni tofauti sana na akina Lowassa na mwenzake Sumaye.
Na tatizo linabaki kuwa mda ndio huo unayoyoma kuelekea kwenye uchaguzi mkuu. Itakuwa kazi ngumu sasa kuwashawishi (kwa mbinu kama zile walizofanyiwa akina Lowassa) ili wazee walegeze kamba.

Kuwafungulia mashtaka ya 'uhujumu' wakati huu sio mwafaka hata kidogo.

Je, ni mbinu zipi zitakazofanyika hawa wazee, angalau wabaki kimya?
 
Mtu mwenye akili timamu alijua vizuri kuwa yaliyokuwa yanasemwa kuhusu hawa wazee ni uongo ambao ungejibiwa na muda.

Wazee wasingekataa kuitikia wito bali wanaweza kukataa yaliyojiri kwenye wito.

Tatizo la mitandao kwa sasa nchini ni uongo umekuwa ukitangulia kabla ya ukweli!


Ni kweli hata yale makontena 70 ni uongo wa slow slow
 
Finally agreed

Jr[emoji769]
Agreed to what?
Tunasema siku ya sabato ni Jumamosi/Jumapili. Sasa siku ya Jumatano ukienda uwanja wa Taifa kuangalia mechi ya Simba vs Yanga na mtu akuone huko atakuwa sahihi kusema amekuona kanisani kwenye ibada siku ya Sabato?
 
Back
Top Bottom