HII NI KWA WENYE AKILI TU!
KUNA tofauti kubwa kati ya kuitikia wito wa kuhojiwa kwenye Kamati ya Nidhamu na kuitikia wito wa kuzungumza ili kuyamaliza kiutu uzima.
Komredi Abdulrahman Kinana na Mwalimu Yusuf Makamba waliitikia wito leo, Lumumba, Dar es Salaam kwenye ofisi ndogo ya Makao Makuu CCM.
Ni baada ya Ijumaa kutokwenda kwenye kikao cha Kamati ya Nidhamu ili kusomewa tuhuma zao na kujieleza, Makao Makuu, Dodoma.
Swali 1; kwa nini hawakwenda Dodoma Ijumaa?
Swali 2; kwa nini kikao cha leo kimefanyika Dar?
Swali 3; Makamba na Kinana waliona Dodoma mbali?
Swali 4; Nini kimewashawishi kuitikia wito leo baada ya kugoma Ijumaa?
Swali 5; Lugha gani ilitumika kujenga wito wa Ijumaa ambao ulifeli na maneno yapi yaliyotumika kufanikisha wito wa leo?
Swali 6; Makamba na Kinana waliitikia wito kama watuhumiwa wanaomhujumu na kumteta Rais Magufuli, au waliitikia wito kama wastaafu wenye hasira baada ya kuchafuliwa?
Swali 7; Agenda ya kikao cha leo ilikuwa nini? Je, tuhuma za kumhujumu Rais au kuzungumza ili kuyamaliza kiutu uzima?
Swali 8; Mbona picha hazizungumzi kikao? Kinana anaonekana kwenye kikao na Mangula, Dk Bashiru na wajumbe wengine wawili lakini Makamba yeye kwenye gari, Dk Bashiru akizungumza naye dirishani?
Swali 9; Picha ya Makamba akiwa kikaoni mbona haijaoneshwa? Picha ya Kinana akiwa anaongea (kuagwa) na Dk Bashiru kwenye gari mbona haipo? Au mpigapicha alichagua kila mmoja ampige na location yake?
Swali 10; Makamba na Kinana waliingia kwenye kikao kimoja au kila mmoja alikuwa na cha kwake?
Swali 11; ni marudio, je, agenda ya kikao ilikuwa tuhuma za kumhujumu na kumsengenya Rais kama walivyodukuliwa kwenye simu zao au ilikuwa kukutana na kuzungumza ili kuyamaliza kiutu uzima?
Zingatia; kuna tofauti kubwa kati ya kuitikia wito wa kuhojiwa kwenye Kamati ya Nidhamu na kuitikia wito wa kukutana kuzungumza ili kuyamaliza kiutu uzima.
Nasisitiza; hii ni kwa wenye akili tu. Kama unajiona huna akili, tafadhali, yapo mambo mengi yanakuhusu lakini sio hii post.
Ameandika Luqman MALOTO
Sent using
Jamii Forums mobile app