Historia inaonesha toka aingie madarakani huwa hahudhirii misiba na majanga makubwa ya kitaifa. Huwa anaenda baada ya siku kadhaa nyingi kupita.
Mfano, msiba wa watoto wa shule kule Arusha mwaka jana, hakwenda kabisa.
Janga la tetemeko la ardhi lililosababisha uharibifu mkubwa mikoa ya kanda ya ziwa hususani mkoa wa Kagera, hakwenda kwa wakati. Alikwenda baada ya siku kadhaa na mnaokumbuka aliishia kutoa maneno ya kashfa kwa wahanga.
Mwenendo na tabia hii ya Rais Magufuli, ilipelekea watu kuanza kuumiza kichwa na hata kuhoji, kulikoni? Maana haikuwa ya kawaida tofauti na watangulizi wake.
Hata hili kama mzee huyu atazikwa pasipo uwepo wake, ndiyo litachochea zaidi shauku ya watu kutaka kujua kulikoni?
Sababu haiwezi kuwa ya "kuumia au kujisikia machungu ya kifo ya mzee huyu". Mimi nakataa mpaka kesho. Ipo sababu nyingine tena ikiwa na uhusiano na imani za kichawi, kiuaguzi, matambiko na ushirikina.
Huyu mzee hata kutosafiri nje ya nchi mara kwa mara, lina connection na hisia hizi. Iwe isiwe, tutajua tu hata wajifiche vipi!