Lupatu: Kinga dhidi ya wachawi na uchawi

Binafsi naamini kitu nachokiona

Nimeshashuhudia vitu vya ajabu kweli
Unaruhusiwa kuamini chochote. Lakini ukweli si lazima uendane na unachoamini.

Hata unachokiona, au unachodhani unakiona, si lazima kiwe kweli.

Mathalani, unaweza kumuona Bob Marley anaimba kwenye concert, kwenye TV, ukasema huyu mtu yupo anaimba.

Kumbe alishafariki siku nyingi.

Kwa mtu asiyeelewa TV inavyofanya kazi, kumuelezea kwamba mtu aliyefariki miaka mingi anaweza kuonekana anaimba mbele yake ni kama uchawi.

Ukienda jangwani, kuna sehemu huko katikati ya jangwa ambako hakuna maji, kutokana na mwanga unavyoakisiwa, panaonekqna kutoka mbali kama pana chemchemi ya maji (mirage).

Unaona kabisa pale pana maji, unayakimbilia. Ukifika unakuta hakuna kitu.

Kwa hiyo hata unachoona hakihakikishi kwamba kitu kipo, unaweza kuona kitu ambacho hakipo.

Na unaweza kuona kitu cha ajabu, kwa sababu hukijui tu, ukasema uchawi.

Kama yule babu ambaye hajui TV inafanya kazi vipi anashangaa watu wanaongea kwenye kibox, anaona uchawi tu.

Kumbe kuna maelezo ambayo hayahusishi uchawi.

Muandishi wa riwaya za kisayansi wa Kiingereza Arthur C. Clarke, aliandika "Any sufficiently advanced technology is indistinguishable from magic".

Babu zetu walioishi miaka 200 iliyopita ungewaonesha ndege zinavyoruka leo, na tunavyowasiliana kwenye internet, wangesema ni uchawi.

Kumbe physics tu.

Unajuaje unachofikiri wewe kuwa ni uchawi leo ni uchawi kweli na si kukosa maarifa kwako tu?
 
Umeandika marefu lakini matupu

Ukweli ni kwamba unaweza kuona na kisiwepo lakini unaweza kuona na kikawepo

Umechagua kuamini nilichokiona hakipo nimechagua kuamini nilichokiona kipo

Unataka urogwe ili uamini?

Maana kwa mtazamo wako unataka ushahidi usio na chembe ya mashaka
 
Sitaki kuamini, nataka kujua.

Hapo ndipo ilipo tofauti yangu mimi na wewe.

Unaweza kuthibitisha uchawi upo, watu wajue?

Kuamini ni haki yako ya kikatiba, unaruhusiwa kuamini vya kweli na uongo.

Tuongelee ukweli, facts, vitu vinavyothibitishika.

Si hadithi za kuaminika.

Uchawi ni nini?

Unajuaje huu ni uchawi, na hii hapa michezo ya kisaikolojia ya karata tatu tu?

Unaweza kuthibitisha uchawi upo?
 
Sio lazima uamini au ujue

Kuamini au kutoamini kwako hakuna athari yoyote

Kwani wewe si Kiranga tu au mwenzetu unajionaje[emoji3][emoji3]
 
Sio lazima uamini au ujue

Kuamini au kutoamini kwako hakuna athari yoyote

Kwani wewe si Kiranga tu au mwenzetu unajionaje[emoji3][emoji3]
Issue hapa si mimi au wewe.

Issue ni, ukweli uko wapi na njozi tupu ziko wapi.

Na hili linajibiwa kwa uthibitisho.

Na hujathibitisha kwamba uchawi upo kweli.

In fact, hata huja define uchawi ni nini.
 
ngoja niisceenshot hii coment, maana wamezidi manina hawa watu hatulai mchana tuhangaike na mikazi migumu, usiku tunataka tupumzike wao nao wanakuja kutupumzikia sisi. Funkeeee
 
Issue hapa si mimi au wewe.

Issue ni, ukweli uko wapi na njozi tupu ziko wapi.

Na hili linajibiwa kwa uthibitisho.

Na hujathibitisha kwamba uchawi upo kweli.

In fact, hata huja define uchawi ni nini.
Elimu magharibi imekuharibu

Definition za kazi gani hapa?

Wachawi wana uwezo huo wa kukufafanulia lakini kwa kuwa ilishachukuliwa kwa mtazamo hasi hakuna mtu atajitokeza akwambie

Uthibitisho uliobaki urogwe tu

Mbona hili unalikwepa?

Sema tukuroge acha mboyoyo[emoji3]
 
Hujathibitisha uchawi upo.

Kwa njia yoyote.

Niroge nishindwe ku type hapa sasa hivi uthibitishe uchawi upo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…