Lupatu: Kinga dhidi ya wachawi na uchawi

Kuna mtu aliketa habari zake za uchawi hapa.

Akanitishia ataniroga.

Nikamwambia aniroge nishindwe kutype hapa JF.

Sijamsikia tena.
Uchawi una kanuni zake pia na miiko yake.Sio unaomba kurogwa tu bila kujua kuwa uchawi una namna yake ili ufanyike kwa ufanisi.
Vitu kama majina yako halisi,ya wazazi wako;musa maalumu,vifaa maalumu na baadhi ya vitu kutoka mwilini mwako au ulipogusa au kuacha uchafu wako n.k
Toeni ushirikiano,mtarogwa mpaka mshangae!
 
Kuna mtu aliketa habari zake za uchawi hapa.

Akanitishia ataniroga.

Nikamwambia aniroge nishindwe kutype hapa JF.

Sijamsikia tena.
Mkuu ujinga bado ni tatizo kubwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Sio ujinga wa kusoma na kua na haya mavyeti bali kuelewa.

Idadi kubwa ya watu bado wanaamini uchawi. Sio wasiosoma tu hata wasomi, juzi niko mkoa flani kikazi kuna nimakutana na brother wangu anamtuhumu brother mwingine kwa uchawi, anamtoa tuhuma ni mtu amesoma sana na ana nafasi kubwa sana serikalini halafu anaetuhumiwa ni mtu ambae hakwenda shule kivile, nilisikitika sana.

Kuna kipindi tuliwahi kupata misiba mfululizo kwenye familia, tuhuma za kurogana zitakamalaki, kidogo zisambaratishe ukoo, hakuto kama tulivyowahi kua, watu wengine hawasalimiani hadi tukutane kwenye matukio.

Hali iko hivyo kwenye kwenye jamii kubwa ya watanzania, watu wanaamini kitu ambacho hakipo. Uchawi haujawahi kuwepo.

Nimeshawaambia watu wengi tu live waniroge lakini sijawahi kuona narogwa.
 
Hujathibitisha uchawi upo.

Hujaniroga nishindwe ku type hapa.

Niroge nishindwe ku type hapa uthibitishe uchawi upo.
Nakufahamu kitambo sana Kiranga tutabishana sana[emoji3][emoji3]nafikiri hakuna tatizo hata ukiamini hakuna uchawi
 
Zamani nilifikiri kwamba tutatatua matatizo mengi ya ujinga kwa kuzidisha elimu (formal education).

Nikaja kugundua kwamba utamaduni una nguvu kuliko elimu.

Ndipo hapo unakuta mtu kasoma, lakini bado anaamini uchawi.

Inasikitisha sana.

Lakini inatia moyo kusikia kwamba kuna watu kama wewe.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Alete nguo, kucha, nywele ,mate na jina halisi.
 
Nakufahamu kitambo sana Kiranga tutabishana sana[emoji3][emoji3]nafikiri hakuna tatizo hata ukiamini hakuna uchawi
Siongelei imani.

Naongelea fact.

Hakuna ushahidi wa fact wa kuthibitisha uchawi upo.
 
Formal education haiwezi kupiku tamaduni za watu. Kuna vitu vya ajabu sana vinafanywa na hao wenye formal education kwa kisingizio cha utamaduni.
 
Siongelei imani.

Naongelea fact.

Hakuna ushahidi wa fact wa kuthibitisha uchawi upo.
Ningekuwa mchawi ningekuthibitishia lakini mimi nimeona masuala ya kichawi

Hapa hatutaelewana kamwe ni mpaka uthibitishe na mimi siwezi
 
Sasa akileta hivyo si unaweza hata kutumia Chemistry kumuua ukaita uchawi?

Unashindwa kuvipata hivyo vitu kwa uchawi?
Mkuu akileta akaondoka halafu pakawa na matokeo ya zoezi hiyo ni chemistry?

Yaani unipe mahitaji halafu urudi ulaya huko uwe kichaa tuseme ni chemistry?
 
Ningekuwa mchawi ningekuthibitishia lakini mimi nimeona masuala ya kichawi

Hapa hatutaelewana kamwe ni mpaka uthibitishe na mimi siwezi
Umeona nini ulichofikiri ni uchawi na kwa nini ni lazima kiwe uchawi tu na si kitu kingine chochote?

Uchawi ni nini?
 
Mkuu akileta akaondoka halafu pakawa na matokeo ya zoezi hiyo ni chemistry?

Yaani unipe mahitaji halafu urudi ulaya huko uwe kichaa tuseme ni chemistry?
Kitendo cha kukupa hivyo vitu kinaweza kukupa nafasi ya kunipa sumu, ukaita uchawi.

Nimekuuliza huwezi kuvipata hivyo vitu kutoka kwangu kwa uchawi?

Hujajibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…