Boa tarde camaradas.
Tembea uyaone, zunguka ujifunze.
Hivyo ndivyo ninavyoanza kwa leo.
Mara nyingi nimekua msomaji tu humu ndani, ila leo kuna topic nimeisoma humu ndani iliyo nishawishi na mimi leo niandike.
Katika harakati zangu za kutafuta maisha nilijikuta naangukia Mocambique. Mocambique sikwenda kuajiriwa bali ni kuchimba madini (Ruby).
Nakumbuka huku nilikutana na Rafiki yangu anaeitwa Carlos. Mshikaji tulijuana kutokana na kufanya nae kazi (kuchimba) mara kwa mara.
Katika harakati zetu mara nyingi tulikuwa watu wa kuporora (hatupati madini)
Siku moja Carlos akanishauri twende kijijini kwao Shapa (wilaya ya Mueda, mkoa Cabo del Gado) kuna mzee ni mganga anaweza kutusaidia katika haraka zetu. Carlos yeye ni Mmakonde chale.
Baada ya kufika kijijini Shapa, Carlos akinichukua mpaka nyumbani kwa mganga (Mzee LUPATU)
Tulifika kwa mzee, tukamueleza shida yetu, na mzee akakubali kutupa dawa (ya madini). Siku ya tatu tukageuka kurudi mgodini (Nanhupo, wilaya ya Montepuez, mkoa Cabo del Gado)
Hatukumaliza wiki mbili, tukapata Gram moja na point saba (Ruby) tukaenda kulitikisa (kuuza) kwa Mtailendi.
Tukapata mgao kila mtu $17,500. US dollar. Kwa muda huo nilijikuta na Milioni thalathini sita na usheee hivi.
Baada ya mgao wetu, tukaamua kwenda kumpa shukrani yake mzee wetu (Mzee LUPATU) tena ukizingatia kutoka Mueda kwenda Namatili (boda) sio mbali, na ndio njia ambayo ninaitumia kuvuka kutoka Mocambique kuja Tanzania.
Tulifika kwa mzee LUPATU tukampa shukrani, na kila mtu akampa yule mzee 50,000 miticaish.
Baada ya shukrani, yule mzee akatuomba tulale pale kwake kisha kesho tuondoke, maana kuna kinga anataka kutupa.
Hakuna aliekataa, tulibaki pale kama alivyotaka babu yetu.
Kilipoingia kiza babu alikuja na ndoo iliyo jaa maji yenye dawa (niliona mizizi na majani ndani ya yale maji) akatuogesha kisha tukaingia kilingeni kwake. Akatoa vibao vidogo viwili, vye pembe nne, mfano wa kibiriti.
Vibao vile upande mmoja wa kibao kulikua kama kimechorwa msalaba kwa kuchongwa. Tukaamuliwa tuchanjwe damu, then damu ile ilipitishwa mule kwenye mistari iliyo chongwa kama msalaba.
Tulipomaliza zoezi lile, kila mtu akapewa kibao chake na kuruhusiwa kwenda kulala.
Kabla ya kwenda kulala mzee alitupa masharti ya dawa ile, akatuambia hii ndio LUPATU Wajukuu zangu, hamtarogwa na mtu yoyote kwenye dunia hii. Akatuambia lakini dawa hii ina masharti.
1 Usiende nayo kwenye shughuli yoyote ile, iwe harusi ama maziko.
2 Ukifika popote (ugenini) unatakiwa uwaambie wenyeji kuwa una kinga dhidi ya uchawi, hivyo hairuhusiwi kwa mtu yeyote kugusa uchawi mpaka utakapo ondoka.
3 Ukitaka kulala na mwanamke, iache nje (nje ya mlango)
Chengine, alituambia kuwa, hiyo dawa inafanya kazi umbali wa nyumba kumi kutoka kushoto, nyumba kumi kulia, nyumba kumi mbele ya nyumba, nyumba kumi nyuma ya nyumba.
Siku iliyo fuata mimi na Carlos tukaondoka, kila mtu akielekea kwao.
Carlos nilimuacha kwao Mueda, mimi nikavuka boda nikaingia nyumbani Tanzania. Nilipofika home, nikawaambia ndugu zangu hasa watu wazima. Pale home, mzee kuliko wote ni mama yangu mkubwa.
Hii ni nyumba ya familia (akina mama wamerithi nyumba ya baba yao) Kuna watu wengi sana.
Basi baada ya mapokezi, uchovu wa safari ilinibidi nipumzike kidogo (nililala)
Nilivyoamka jua lilikua limeshazama, hivyo jioni ilisha ingia.
Nikatumia muda huo kuwaambia wale waliokuwepo siku hiyo.
Nakumbuka alikua Mama mkubwa, dada yangu wa kwanza kuzaliwa, Mjomba pamoja na madogo walio kuwepo hapo.
Nilinza kwa kuwaambia kuwa nina dawa ya uchawi, hivyo kama kuna mchawi basi asichezee uchawi wake mpaka mimi nitakapoondoka.
Niliongea kimasihara kwakua nilitegemea nyumbani hakuna mchawi.
Mama yangu mkubwa akaomba nimuoneshe hiyo kinga (dawa).
Nikaingia mfukoni nikakitoa kile kibao. Kila mtu alicheka na kusema Mocambique wanaamini sana uchawi.
Usiku uliingia na kila mmoja akaenda zake kulala.
Siku ya pili palipokucha nikaelekea zangu Karikoo, kwenda kuchenji Dollar zangu. (Kariakoo Bazar )
Siku hiyo nakumbuka nilikula sana mtungi, nikarudi home usiku sana kama mida ya saa sita hivi usiku.
Nilipo fika home, kwa uchovu wa pombe nikajilaza kitandani, mara hazikupita dakika nyingi nikaanza kuona chumba kina mwekua mwekua, yani kama mtu kashika kioo anakizungusha mule ndani.
Nikaamka, mara ya kwanza nilidhani ni pombe labda, lakini jinsi muda ulivyokua unaenda ile hali ndio ilikua inazidi.
Ilipita kama dakika 20 hivi huku ile hali ya kumulika ikiendelea, mara nikasikia Pah! Yani kama mtu kapasua chupa ya bia vile.
Baada ya ule mlio, ule mwanga wa kioo mule ndani ukapotea.
Usingizi ulinichuka mpaka asubuhi.
Cha ajabu naamka asubuhi nakuta watu pale home wamejawa na huzuni, nilivyouliza naambiwa mama yako mkubwa kaanguka jana usiku mlangoni kwake akitokea chooni, hivyo kawaishwa hospital Temeke.
Samahani ndugu zangu.
Hii story nilipanga kuimaliza leo leo, ila kuna hudhuru imenikuta, hivyo nitaimalizia baadae ama kesho.
Naomba munisamehe.
Kwakua chenji nilikua