Lupatu: Kinga dhidi ya wachawi na uchawi

Na VIP umepata hayo madini(utajiri/hela) baada ya kufanya makufuru yote hayo mkuu.?..out of curiosity!
Madini nishapata sana.
Nikitaja migao niliyo wahi kugawana unaweza kuacha kazi yako ukani fuata.
Kuhusu mali ninazo miliki ni Nyumba, na kirikuu mbili (vigali vidogo vya mizigo) pia nina shamba la minanasi kijijini Hanga (njia ya nyamisati )
Lakini mpaka sasa bado nachimba.
WACHIMBAJI pesa tuna pata tatizo letu ni Bata. Tunatumia mpaka chenji ya mwisho.
 
Maana yangu inabaki pale pale hata kama ni maza!
 
Sio wote.
Wapo wanaochimba na kupata kwa bahati zao, ila wanachelewa kupata.

Ila kiukweli ili uishinde kesi ya madini lazima ukufuru.
Binafs nishalala makabulini, nishafukua maiti za watu, yote ni kutafuta madini tu.
Mungu anisameh.
Weee ishia hapohapo.
Ndani ya dakika 10 zijazo nikukute kituoni Central
 
Kaka Jabiri fanya urudi basi hapa nyumbani Mkuranga hali ya kimaisha si nzuri,anko anataabika.Huko Msumbiji umeenda mazima maana wachimbaji mna 'mambo majinga' sana.Unakumbuka ule mwaka uliopota ruby nyingi..wakakunyang'anya,wakakupiga.Kaka Jabiri rudi!
 
Ooohooooo
 
Naona hii HADITHI, inafanana na zile hadithi tamu za Said Bawji enzi zileeee za gazeti la SANI. Likitoka leo likiwa na hadithi ambayo haijaisha, na kuambiwa ITAENDELEA TOLEO LIJALO, basi unakaa na hamu ya kulisubiri TOLEO LIJALO kwa zaidi ya miezi miwili. Tofauti na hadithi za John Rutayisingwa tulizokuwa tukizisoma kwenye gazeti la Mzalendo,kila Jumapili, kabla hajahamia kwenye gazeti la Dimba na Rai.
Dunia imebadilika. Jiandae, malizia simulizi yako yote pembeni, kisha uilete hapa, yabaki maoni ya wasomaji. Na huko magazetini, kukatiza katiza simulizi, ni kwa ajili ya biashara, ili ununue tena gazeti lijalo. Sasa sijajua mleta simulizi hii, hii katiza katiza, zina lengo gani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…