Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
EmamaUsitutishe *****
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
EmamaUsitutishe *****
Hiyo sehemu ulotaja timu zetu kubwa uchawi ndo wanatoaga hapo, mmoja aliwahi kamatwa hapo boda,/akaeleza jinsi alivyotumwa na alikuwa hana kibali cha kuingia kule Mozambique (c) baadae akaja kuachiwa akapita
Bora Yako...Niliambulia nyumba tu, ipo chamanzi mfenesini. Pesa nyingine nililia bata.
Vipi Huko Mwatizi wale Magaidi wa Cabo Del Gado Hawajatimba?!!!Mkuu mimi sio mganga wa kienyeji.
Mimi ni mchimbaji, na mpaka hapa ninapo andika niko zangu Mwatizi, wilaya ya Mwatizi, mkoa wa Tete ,Mocambique, bado naendelea na kulisaka jiwe.
😂😂😂Mshana hajui uchawi, ila anazijua story za kichawi tu. Watu tunachezea uchawi kila siku.
Kama nakuongopea muulize, keshawahi kufukua maiti iliyo zikwa miezi mitatu iliyo pita?
Wengine tusha pagawa na haya maisha, mtuache tu.
Lupatu jina la mkoa wa Tanga
MozambikHili neno tunalitamkaje mbona limenishimda "Mocambique"
.....afrika hii..Hahaha!
Wabongo kwa kupenda Ulozi
😂😂😂Niazime hicho kibao mara moja mkuu...nina kazi nacho
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Fureshiii mwanalupatu.
We tupe season iyo Wala ata usiwazeMama alikitazama kile kibao muda kama dakika 5 hivi, mpaka nikajistukia na kumuuliza mama, mbona anakiangalia sana?
"Mwanangu hichi kitu ni kikubwa wewe bado ni mtoto, kitupe kitakuletea madhara"
"Hiki ndicho kilicho waua dada yangu na kaka yangu"
Mama aliendelea kuongea huku machozi yakimtoka, mpaka mimi mwenyewe nikashikwa na wenge.
Aliendelea kuniambia, mpaka Kule kijijini watu wamesha jua kua ni mimi ndie nilie sababisha vifo vya Mama mkubwa na mjomba.
Hata watoto wa mjomba wamechukizwa na kitu hicho.
Basi mama akiniomba nikitupe kile kibao.
Mama hakukaa akaondoka kwake, huku nyuma akiniacha na mawazo kibao kichwani.
Kwa kweli nilikaa kama wiki mbili tu lakini nikawa tayari nisha sababisha vifo zaidi ya saba.
Maana ukiachilia kifo cha mama mkubwa pamoja na mjomba, pia hapa mtaani kuna vifo vitatu vya majirani, na vyote vina fanana.
Maana wote kabla ya kufa hutokwa na damu sehumu zote za siri, na wote wamenitaja kwamba chanzo cha kifo Chao ni mimi.
Siku moja nilitulia sehem peke yangu nikajiuliza maswali, nikaona ngoja niende kwa rafiki yangu Yombo dovya (huyu jamaa tume maliza wote yombo dovya primary school)
Nilivyo fika kwake, sikumficha, nimamweleza mkasa mzima, chakushangaza na yeye akaniambia hata hapo kwao kuna vifo vya wazee wawili viliongozana kipindi nilipo peleka begi langu kwao.
Nikarudi home, nakukata shauri kwamba lazima hiki kibao (kinga) nikitupe.
Siku moja, mtaani hapo kulikua na kigodoro, nikala mtungii nikasema leo lazima nikitupe hiki kibao.
Mala baada ya kukubali mtungi nikaongoza mpaka lelini, nikakitoa kile kibao nakukirusha kwa mbali.
Nikarudi zangu home na kujilaza kitandani na usingizi ukanipitia.
Asubuhi nilipo amka, nishaoga maji yangu nikatoa suruali nyingine nikavaa, nikaitoa ile suruali niliyo ivaa jana nakuanza kutoa vitu muhimu.
Nikazama mfuko wa kwanza nikatoa simu, mfuko mwengine nikatoa waleti, sasa nikawa nacheki mifuko ya nyuma ili nicheki kama kuna chenji chenji, katika angaika angaika zangu nakitoa tena kile kibao (ile kinga niliyo itupa jana yake kwenye kigodoro) kwanza nilipagawa nusu ya kudata.
Nakumbuka hiyo siku, nilipanga na mtu (dalali) niende nikaangalie kiwanja Mbande, lakini kutokana na tukio hilo ilinibidi nimpigie jamaa simu nakumuomba aniwie radhi kwa siku hiyo, kwani nilishindwa hata kutoka nje kwa siku hiyo.
MUENDELEE KUNI SAMEHE, MAMBO NI MENGI MUDA NI MDOGO. HATA KESHO NAWEZA NIKAMALIZIA. NITARUDI.
Utapataje madini bila ushirikina???je wajua majini ndio walioficha hayo madini huko chiniWachimbaji washirikina sana
Kuna wachawi hapo balaaHapo Bungu nilimzika my best friend Said Ndaruke: RIP SAID
Uliwaona wakati wakiyaficha?Utapataje madini bila ushirikina???je wajua majini ndio walioficha hayo madini huko chini
Nyuma ya paziaUliwaona wakati wakiyaficha?