Sisi huku tunaangalia kalio,hips ,weupe na sura,kipaji sio muhimu kwani tutaelekezana mbele ya safari,ila ukiwa navyo hivyo umeshafuzu.Yule Lupita na yule general wa Wakanda wangekuwa bongo wangeambiwa watafute kazi nyingine ya kufanya,kwani vipaji wanavyo ila vile vigezo vya kalio,hips,weupe na sura hawana.Sisi watanzania sehemu nyingi tunaendaga vice versa na ndio maana kuja kumuona mbongo hollywood kwa hivi vigezo vyetu sizani kama tuweza na siku hizi bongo movie upande wa wanaume wanachukua mashombe shombe,wauma lips ,hawaangalii sana vipaji.Ndio maana sanaa ya bongo inakosa ubunifu sababu haina watu wenye vipaji halisi,tutaendelea kumark time tu hapa hapa bongo.Mimi naonaga bora commedy za kibongo zina watu wenye vipaji lkn hizi tamthilia zimekosa mvuto (mfano siri za familia ,mishepu imejaa kibao utafikiri wanatafuta miss bantu).