Lusinde amvaa Amunike kweupe

Lusinde amvaa Amunike kweupe

PURT50

Member
Joined
Oct 20, 2018
Posts
43
Reaction score
36
Mbunge wa Mtera(CCM),Livingstone Lusinde ameitaka TFF kuandaa barua ya kumfuta kazi kocha was Taifa Stars,Emmanuel Amunike ili akishuka tu uwanja wa ndege akabidhiwe.

Lusinde ametoa kauli hiyo kufuatia Taifa Stars kulala bao 1-0 dhidi ya Lesotho mjini Maseru na kujiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu Afcon 2019 kule nchini Cameroo.

"Hii serikali ina mawaziri wanaotumbuliwa wakikosea kidogo tu,sasa huyu kocha anazoa wachezaji na kuwapanga anavyotaka yeye halafu tumwache.Namwomba Waziri Mwakyembe awaandikie TFF akiwa huko ili wavunje mkataba haraka" amedai Lusinde.

Lusinde alidai pia sifa ya Amunike ni nidhamu ambayo wachezaji wanaweza wakafundishwa jeshini lakini sio suala LA soka kwani limeshamshinda.

Lusinde pia amedai Amunike amekuwa na upendeleo katika upangaji wa kikosi na badala yake anapanga watu kwa kuangalia matakwa ya wapenzi na sio kitàalamu.
 
Mbunge wa Mtera(CCM),Livingstone Lusinde ameitaka TFF kuandaa barua ya kumfuta kazi kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike ili akishuka tu uwanja wa ndege akabidhiwe.Lusinde ametoa kauli hiyo kufuatia Taifa Stars kulala bao 1-0 dhidi ya Lesotho mjini Maseru na kujiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu Afcon 2019 nchini Cameroon.
"Hii serikali INA mawaziri wanaotumbuliwa wakikosea tu kidogo,sasa huyu kocha anazoa wachezaji na kuwapanga anavyotaka yeye halafu tumwache.Namwomba Waziri Mwakyembe awaandikie TFF akiwa huko ili wavunje nae mkataba haraka" amedai Lusinde.
Lusinde alidai pia sifa ya Amunike in nidhamu ambayo wachezaji wanaweza wakafundishwa hata jeshini lakini sio suala la soka ambalo amedai limemshinda.
Lusinde pia amedai kuwa Amunike amekuwa na upendeleo katika upangaji wa kikosi na badala yake anapanga watu kwa kuangalia matakwa ya wapenzi na sio kitaalamu
 
Kwa mara ya kwanza Lusinde katoa point!! Hongera Mh. Mbunge kuwa mkweli walau kwenye hili.

Huwa anatoa point au hoja za msingi mara nyingi tu ila kwa kuwa huwa unakuwa siyo upande wake huwa unazichukulia hoja zake kuwa hazina lolote
 
Hapa ndio utazijua Akili za Wabongo!

Wakishinda mwalimu anafaa wakifungwa Mara moja tu mwalimu aondoke!

Yale Yale enzi za Maximo
 
Mbunge wa Mtera(CCM),Livingstone Lusinde ameitaka TFF kuandaa barua ya kumfuta kazi kocha was Taifa Stars,Emmanuel Amunike ili akishuka tu uwanja wa ndege akabidhiwe.Lusinde ametoa kauli hiyo kufuatia Taifa Stars kulala bao 1-0 dhidi ya Lesotho mjini Maseru na kujiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu Afcon 2019 kule nchini Cameroo. "Hii serikali ina mawaziri wanaotumbuliwa wakikosea kidogo tu,sasa huyu kocha anazoa wachezaji na kuwapanga anavyotaka yeye halafu tumwache.Namwomba Waziri Mwakyembe awaandikie TFF akiwa huko ili wavunje mkataba haraka" amedai Lusinde.
Lusinde alidai pia sifa ya Amunike ni nidhamu ambayo wachezaji wanaweza wakafundishwa jeshini lakini sio suala LA soka kwani limeshamshinda
Lusinde pia amedai Amunike amekuwa na upendeleo katika upangaji wa kikosi na badala yake anapanga watu kwa kuangalia matakwa ya wapenzi na sio kitàalamu.
Kwenye michezo atulie huyo mbunge atowe sauti yake juu ya yule mkwepa kodi au lile nijambo dogo kwake?
 
Back
Top Bottom