PURT50
Member
- Oct 20, 2018
- 43
- 36
Mbunge wa Mtera(CCM),Livingstone Lusinde ameitaka TFF kuandaa barua ya kumfuta kazi kocha was Taifa Stars,Emmanuel Amunike ili akishuka tu uwanja wa ndege akabidhiwe.
Lusinde ametoa kauli hiyo kufuatia Taifa Stars kulala bao 1-0 dhidi ya Lesotho mjini Maseru na kujiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu Afcon 2019 kule nchini Cameroo.
"Hii serikali ina mawaziri wanaotumbuliwa wakikosea kidogo tu,sasa huyu kocha anazoa wachezaji na kuwapanga anavyotaka yeye halafu tumwache.Namwomba Waziri Mwakyembe awaandikie TFF akiwa huko ili wavunje mkataba haraka" amedai Lusinde.
Lusinde alidai pia sifa ya Amunike ni nidhamu ambayo wachezaji wanaweza wakafundishwa jeshini lakini sio suala LA soka kwani limeshamshinda.
Lusinde pia amedai Amunike amekuwa na upendeleo katika upangaji wa kikosi na badala yake anapanga watu kwa kuangalia matakwa ya wapenzi na sio kitàalamu.