Lusinde amvaa Amunike kweupe

Lusinde amvaa Amunike kweupe

Tunataka faida ya haraka kwa uwekezaji wa kuhonga leo kesho kimyaaaaa
 
Msitafute mchawi wakati anajulikana! Mpe Pesa mwanao anayekuogopa sana kabla ya kwenda kufanya mtihani na kumwambia "ukifeli huu mtihani pesa zangu utazitapika" uone kama atafaulu!
Wale walio tazama tafrija ile pale Ikulu wakakubaliana nami kuwa wachezaji hawakupata hamasa bali walienda kupata hofu na woga tuu maana sura zao na za viongozi wao zilisawajika kabisa.
Ushindi wa michezo una factors nyingi na moja wapo ni kuuchukulia mchezo kama mchezo sio ugomvi kama kiongozi wetu alivyo taka wachezaji wacheze. Ukileta mentality ya ugomvi unapewa kadi na unapunguza nguvu ya timu.
Mwambieni akadili na korosho zake michezo awaachie wengine.
Timu ya taifa imeanza kuwa njema baada ya kuwa na wachezaji professional wengi wakichanganya ujuzi na wa ndani
 
Tunataka faida ya haraka kwa uwekezaji wa kuhonga leo kesho kimyaaaaa
Wanadhani ushindi wa mpira ni kama uhesabuji wa kura wa NEC unaotangaza kuwa wapiga kura wapo 100 zilizoharibika 10, Chadema 40, CUF 20, na CCM 70.
Uchaguzi ulikuwa huru na haki
 
Mwenye msimamo kundi letu tafadhali atuwekee
_20181120_070550.JPG
 
Kwa mara ya kwanza Lusinde katoa point!! Hongera Mh. Mbunge kuwa mkweli walau kwenye hili.
Katoa pumba tu akili za kuwaza jeshi litatatua kila tatizo. Eti nidhamu watafundishwa jeshini mbona kina jkt sijui prison au pilisi timu zao hata hazifurukutu. Hizi ndio akili za kuamini jeshi litakuza uchumi peke yake.
 
Hata
Ila kweli amunike aeleweki mpaka sasa hana kikosi cha kwanza kila siku timu mpya anachukua wachezaji kutoka timu za chini kabisa kwa msimamo wa ligi
Aende tu anaboa
hata Maximo ililaumiwa hivyohivyo tu mpaka akina Marehemu Mziray walimlaumu kwa kubadilisha sana wachezaji, kwani hilo ni tatizo kubwa?!? katika kubadili huko ndio atapata kikosi anachokitaka. lakini ndiyo AMUNIKE ana makosa yake na wachezaji je?!? wao ndio walikuwa uwanjani watz kabisakabisa kama waliona mbinu za Amunike hazifai si wangetumia mbinu zao binafsi?!? tukashinda, Tizama wale mabeki walikuwa wao wawili tu wakatoa ikawa kona ikazaa goli, hivi Manura kwa nini hakuupiga ule mpira ngumi ukaenda mbali sana?!?, inawezekana hata Gardiolla akijitolea aje kutufundisha bure miaka mi5 atabadilisha sana wachezaji maana inawezekana wasiojulikana ndio wanafaa!
 
Kocha mzuri huanzia alipoishia; kikosi kilichocheza hapa majuzi alitakiwa aanze nacho kile kile - hayupo Samata basi angemwita Ajibu ambaye kaonyesha kiwango kizuri sana!! Kapombe kaumia angeanza na beki wazoefu sijui kwa nini hakumwita Shabalala.
kitendo cha kumwacha Boko; Mkude na Ulimwengu ni dhihaka kwetu washabiki

Atupishe tu jamaa!! Kucheza mpira kimataifa hakukufanyi uwe kocha bora.
 
Hata ukiwauliza viongozi wa nchi hii kama tatizo ni nini hatufanikiwi kisoka naamini hawana hata majibu
Kwa hii mechi laini ya Lethoto sina haja ya kuangalia huko nyuma kulitokea nini. Unapanga walinzi 7 (including kipa) halafu unategemea kushinda? Hata Morinho na mabasi yake hajawahi kupanga mabeki 6 mechi moja.
 
Back
Top Bottom