Mbunge wa Mtera(CCM),Livingstone Lusinde ameitaka TFF kuandaa barua ya kumfuta kazi kocha was Taifa Stars,Emmanuel Amunike ili akishuka tu uwanja wa ndege akabidhiwe.
Lusinde ametoa kauli hiyo kufuatia Taifa Stars kulala bao 1-0 dhidi ya Lesotho mjini Maseru na kujiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu Afcon 2019 kule nchini Cameroo.
"Hii serikali ina mawaziri wanaotumbuliwa wakikosea kidogo tu,sasa huyu kocha anazoa wachezaji na kuwapanga anavyotaka yeye halafu tumwache.Namwomba Waziri Mwakyembe awaandikie TFF akiwa huko ili wavunje mkataba haraka" amedai Lusinde.
Lusinde alidai pia sifa ya Amunike ni nidhamu ambayo wachezaji wanaweza wakafundishwa jeshini lakini sio suala LA soka kwani limeshamshinda.
Lusinde pia amedai Amunike amekuwa na upendeleo katika upangaji wa kikosi na badala yake anapanga watu kwa kuangalia matakwa ya wapenzi na sio kitàalamu.
Ukishaanza kutafuta namna ya kumaliza matatizo yako(na kujiongezea umaarufu) inakuwa shida sana. Tatizo la Tanzania kwa sasa ni mifumo zaidi. Mpira wa miguu ni kielelezo kingine tu. Kocha umemtoa nje ya nchi unategemea atapata wapi wachezaji? Ataanglia mifumo yetu ya ndani ya mpira wa miguu, sasa kama imekufa yeye awatoe hao wachezaji wapi? "Mars" au?
Taifa Stars(wakati huo) ndo timu ya taifa ya mwisho kushiriki fainali za "AFCON" mwaka 1980(bao la Peter Tino) mpaka leo ni ziro. Lakini ukiangalia wakati wa Mwalimu JKN kulikuwa na mifumo lukuki ya kuendeleza michezo, Umiseta, Umishumta nk, leo iko wapi hii, imekufa(ama inaendeshwa kinadharia tuuuu).
Hakukuwa na wadhamini kama leo, hata kocha wa kumwajiri kwa mapesa mengi au Raisi wa kuahidi mapesa mengi kwa wachezaji kama leo (Waliambiwa tu kweni wazalendo), na bado ndo timu pekee ya taifa iliyofanya vizuri zaidi kuliko timu yoyote mpaka leo(na si kazi tutayaona kwa miaka mingine ijayo).
Angalia sasa Mh. Rais anavyofanya, ni kama vile mifumo yote ya ki-inchi imekufa, mfano kwenye secta ya uchumi imetokea matatizo ya kiuchumi leo unatatua kwa matamko(na kutumia bunge ama jeshi kama mhuri tu) na iko mifano mingi kwa sasa hivi siwezi kusema yote leo(hahahah itabidi mada mpya hapa JF), miaka yake 5(10) ikiisha akaja mwingine na style yake tuanze kumlaumu(na wengine kumsifu).... na mwingine akija kwa mtiririko huo huo kwa miaka 5(10) tuendelee hivyo hivyo tena na tena...
USHAURI WANGU.
Mifumo yetu mingi(except JKN angalau alikuwa na mfumo anaotaka kuufuata na uliokuwa unaeleweka japo baadhi alifeli) ina aanguka sababu ya mambo ya kisiasa zaidi(nakubali mifumo ya kisiasa ndo inayoamua mustakabali wa nchi zote duniani), labda ni muda sasa kama kweli tuna mfumo(tuuboreshe SANA!) au tutengeneze mfumo mpya bora zaidi(sio bora mfumo wa kupiga makofi na kutoa pongezi)
Love you my country Tanzania
Wish God gives you My President you a better Wisdom.