Lusinde amvaa Amunike kweupe

Lusinde amvaa Amunike kweupe

Mbunge wa Mtera(CCM),Livingstone Lusinde ameitaka TFF kuandaa barua ya kumfuta kazi kocha was Taifa Stars,Emmanuel Amunike ili akishuka tu uwanja wa ndege akabidhiwe.

Lusinde ametoa kauli hiyo kufuatia Taifa Stars kulala bao 1-0 dhidi ya Lesotho mjini Maseru na kujiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu Afcon 2019 kule nchini Cameroo.

"Hii serikali ina mawaziri wanaotumbuliwa wakikosea kidogo tu,sasa huyu kocha anazoa wachezaji na kuwapanga anavyotaka yeye halafu tumwache.Namwomba Waziri Mwakyembe awaandikie TFF akiwa huko ili wavunje mkataba haraka" amedai Lusinde.

Lusinde alidai pia sifa ya Amunike ni nidhamu ambayo wachezaji wanaweza wakafundishwa jeshini lakini sio suala LA soka kwani limeshamshinda.

Lusinde pia amedai Amunike amekuwa na upendeleo katika upangaji wa kikosi na badala yake anapanga watu kwa kuangalia matakwa ya wapenzi na sio kitàalamu.
Kuna kitu sisi Watz huwa hatukisemi nacho ni umri wa wachezaji wetu wengi wamedanganya wameshazeeka ndo maana uwanjani wanawahi kuchoka, kupiteza maarifa na mpira wanakabia macho.
 
Kwenye hiyo mechi waziri Mwakiembe alikua anonesha kukataa tamaa... yani ili mradi mpira uishe aende zake...

Ila performance yetu ilikua mbovu sana... hata hilo bao moja ni la kizembe sana...


Cc: mahondaw
 
Hiv kumbe kuna watu walitegemea jana tungevuna magoli kule Lesotho duh.. Kwa team hiihii tuliyonayo...
 
Tumpe nafasi
Kusema kweli kocha na timu wametuangusha. Mimi nilikuwa naamini kwa dhati kabisa kwamba tunawapiga Lesotho na tunaingia fainalini! Million 50 wamepewa, wamekaa South siku kumi, wanawakilisha watanzania 55million; tunafungwa na timu ya kitongoji kama Bonyokwa!! Mimi ni miongoni mwa watu ambao wameumia sana na kufungwa huku. Nafasi yetu hadi tuombe wengine washinde nasi tushinde wakati jana tulikuwa na mechi moja tu ya kumaliza kazi, hiyo mechi ambayo tunaitegemea inakuwa kama kupiga ramli. Hakuna cha kupewa nafasi hapa
 
Tumpatie muda huyu kocha, pamoja na kufungwa lakini mpira walicheza kwa kuwango kizuri toka nijue taifa star, nina uhakika tunaweza fanya vizuri game ijayo, huyu jamaa anaweza kutujengea team nzuri kwa uzoefu wake.
 
Hivi mnadhani kuyafundisha Yale machoko ni kazi rahisi??.. tuyapeleke kwa konki master tuu
 
Mbunge wa Mtera(CCM),Livingstone Lusinde ameitaka TFF kuandaa barua ya kumfuta kazi kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike ili akishuka tu uwanja wa ndege akabidhiwe.Lusinde ametoa kauli hiyo kufuatia Taifa Stars kulala bao 1-0 dhidi ya Lesotho mjini Maseru na kujiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu Afcon 2019 nchini Cameroon.
"Hii serikali INA mawaziri wanaotumbuliwa wakikosea tu kidogo,sasa huyu kocha anazoa wachezaji na kuwapanga anavyotaka yeye halafu tumwache.Namwomba Waziri Mwakyembe awaandikie TFF akiwa huko ili wavunje nae mkataba haraka" amedai Lusinde.
Lusinde alidai pia sifa ya Amunike in nidhamu ambayo wachezaji wanaweza wakafundishwa hata jeshini lakini sio suala la soka ambalo amedai limemshinda.
Lusinde pia amedai kuwa Amunike amekuwa na upendeleo katika upangaji wa kikosi na badala yake anapanga watu kwa kuangalia matakwa ya wapenzi na sio kitaalamu
Huyu Lusinde sijui hizi bangi anazovuta anazitoa wapi serikali ya CCM imeshindwa kutuondoa kwenye list ya nchi maskini zaidi duniani kwa miaka hamsini anataka Amunike atimuliwe baada ya kukaa na team miezi miwili tu ?
Hawezi kuwa sahihi kwa hili
 
Mbunge wa Mtera(CCM),Livingstone Lusinde ameitaka TFF kuandaa barua ya kumfuta kazi kocha was Taifa Stars,Emmanuel Amunike ili akishuka tu uwanja wa ndege akabidhiwe.

Lusinde ametoa kauli hiyo kufuatia Taifa Stars kulala bao 1-0 dhidi ya Lesotho mjini Maseru na kujiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu Afcon 2019 kule nchini Cameroo.

"Hii serikali ina mawaziri wanaotumbuliwa wakikosea kidogo tu,sasa huyu kocha anazoa wachezaji na kuwapanga anavyotaka yeye halafu tumwache.Namwomba Waziri Mwakyembe awaandikie TFF akiwa huko ili wavunje mkataba haraka" amedai Lusinde.

Lusinde alidai pia sifa ya Amunike ni nidhamu ambayo wachezaji wanaweza wakafundishwa jeshini lakini sio suala LA soka kwani limeshamshinda.

Lusinde pia amedai Amunike amekuwa na upendeleo katika upangaji wa kikosi na badala yake anapanga watu kwa kuangalia matakwa ya wapenzi na sio kitàalamu.

Ukishaanza kutafuta namna ya kumaliza matatizo yako(na kujiongezea umaarufu) inakuwa shida sana. Tatizo la Tanzania kwa sasa ni mifumo zaidi. Mpira wa miguu ni kielelezo kingine tu. Kocha umemtoa nje ya nchi unategemea atapata wapi wachezaji? Ataanglia mifumo yetu ya ndani ya mpira wa miguu, sasa kama imekufa yeye awatoe hao wachezaji wapi? "Mars" au?

Taifa Stars(wakati huo) ndo timu ya taifa ya mwisho kushiriki fainali za "AFCON" mwaka 1980(bao la Peter Tino) mpaka leo ni ziro. Lakini ukiangalia wakati wa Mwalimu JKN kulikuwa na mifumo lukuki ya kuendeleza michezo, Umiseta, Umishumta nk, leo iko wapi hii, imekufa(ama inaendeshwa kinadharia tuuuu).

Hakukuwa na wadhamini kama leo, hata kocha wa kumwajiri kwa mapesa mengi au Raisi wa kuahidi mapesa mengi kwa wachezaji kama leo (Waliambiwa tu kweni wazalendo), na bado ndo timu pekee ya taifa iliyofanya vizuri zaidi kuliko timu yoyote mpaka leo(na si kazi tutayaona kwa miaka mingine ijayo).

Angalia sasa Mh. Rais anavyofanya, ni kama vile mifumo yote ya ki-inchi imekufa, mfano kwenye secta ya uchumi imetokea matatizo ya kiuchumi leo unatatua kwa matamko(na kutumia bunge ama jeshi kama mhuri tu) na iko mifano mingi kwa sasa hivi siwezi kusema yote leo(hahahah itabidi mada mpya hapa JF), miaka yake 5(10) ikiisha akaja mwingine na style yake tuanze kumlaumu(na wengine kumsifu).... na mwingine akija kwa mtiririko huo huo kwa miaka 5(10) tuendelee hivyo hivyo tena na tena...

USHAURI WANGU.
Mifumo yetu mingi(except JKN angalau alikuwa na mfumo anaotaka kuufuata na uliokuwa unaeleweka japo baadhi alifeli) ina aanguka sababu ya mambo ya kisiasa zaidi(nakubali mifumo ya kisiasa ndo inayoamua mustakabali wa nchi zote duniani), labda ni muda sasa kama kweli tuna mfumo(tuuboreshe SANA!) au tutengeneze mfumo mpya bora zaidi(sio bora mfumo wa kupiga makofi na kutoa pongezi)

Love you my country Tanzania
Wish God gives you My President you a better Wisdom.
 
Kwa mara ya kwanza Lusinde katoa point!! Hongera Mh. Mbunge kuwa mkweli walau kwenye hili.
Hamna kitu hapo. Anajaribu kuusoma upepo wa mkulu. Anajaribu kumfurahisha aliyetoa million 50.
 
hatuna soccer academy hata moja halafu unategemea miujiza kwenye soka
hivi tuna mpira gani hadi tuwafunge lesotho kwao!!!
acheni bange

Ushindi hauji kwa kuomba dua tu na maneno mareeefu. Don't politicise mpira please. Tunahitaji kuwekeza sana na tusitake mafanikio ya haraka. Pamoja stars msivunjike moyo na wanasiasa msiwavunje moyo vijana. Mpira sio maneno+ blabla
 
Chadema na upinzani wataungana kumtetea amunike

Kitu kikitajwa na wanasisiem wao ni kupinga tu
 
Chadema na upinzani wataungana kumtetea amunike

Kitu kikitajwa na wanasisiem wao ni kupinga tu
Ila kweli amunike aeleweki mpaka sasa hana kikosi cha kwanza kila siku timu mpya anachukua wachezaji kutoka timu za chini kabisa kwa msimamo wa ligi
Aende tu anaboa
 
Back
Top Bottom