The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mbunge wa Jimbo la Mvumi, Livingstone Lusinde, amempongeza na kumuhimiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi, kuendelea kutenda haki bila woga wala upendeleo, licha ya vitisho anavyopokea kutoka kwa watu wanaodhulumu wananchi.
Akichangia bungeni leo, Mei 29, 2025, wakati wa kujadili Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha ujao, Mhe. Lusinde amesema taifa lina watu waliobobea katika dhuluma, hasa kwenye sekta ya ardhi, na kwamba baadhi yao wamekuwa wakituma jumbe za vitisho kwa Waziri ili asiwaguse.
"Kuna watu ni wadhulumati kwenye nchi hii. Wanadhulumu ardhi za watu wa chini. Waziri endelea kuwa na roho hiyo hiyo na sura ya kibandidu," amesema Lusinde.