Ukabila unatufanya wa Afrika tuendelee kuburuta mkia, China, India, Europe, Amerika zimepiga hatua kwa sababu wameamua kuondoa tofauti zao, wameungana wana faida ya watu, masoko yao ya ndani yanajitosheleza,
Ukija Afrika bado tumefungwa na fikra za utengano, mipaka tuliowekewa na wakoloni inaendelea kututafuna miaka zaidi ya 60, toka Mataifa yetu yapate uhuru.
Idadi ya watu Afrika ni 1.2 billion, tukiamua kuondoa tofauti zetu, tukawa kitu kimoja tutasonga mbele, kwa kutegemea soko la ndani, hata kama mataifa ya magharibi yakiamua kukaa pembeni.
Tanzania si kitu bila Kenya, na Kenya si kitu bila Uganda, nk. Wote tunategemeana, tuondoe fikra tulizofungwa nazo enzi za ukoloni, tuungane tuwe kitu kimoja,
Kama Nyerere aliweza kuunganisha makabila zaidi ya 100 ya Tanzania, hata sisi tukiamua kuweka tofauti zetu za kikabila, kijiografia, tunaweza kuungana kwa mustakabali wa vizazi vyetu vijavyo.
Tukiendelea na fikra za kujiona mimi ni Mtanzania, mimi ni mkenya, mimi ni mganda, tutakuja tutawaliwe tena,
Amerika ilivamia Libya hatukua na cha kumfanya, tungekuwa tumeungana asingeweza kuthubutu kuivamia Libya,
Congo inapitia machafuko miaka nenda miaka rudi, sababu ya utengano wetu, hatuthaminiani, ni rahisi mtu mweusi kumwaga damu ya ndugu yake, tofauti na wenzetu,
Tukiamua kuweka tofauti zetu za kikabila, kijiografia tunaweza kuifanya Afrika ikapiga hatua, na kuondoa dhana ya bara giza.