Luteni Ian Kagame

Luteni Ian Kagame

Mjukuuu kashaulaa kablaaa ajasomaa aisee wenye nyota zaooo tuendelee kupanga tuwarithishe watoto jinsi ya kulipa kodi on tym kwa wenye house zao na tusiwasumbue wasije aibika
 
Mtoto wa kike wa Gisa aliyezaa na mkewe mnyarwanda anaitwa Teta alipelekwa kusoma nje na PK na aliporudi akapewa kazi huko Wizara ya Mambo ya nje ya Rwanda na hata kwny harusi yake PK,mkewe na watoto wake walikuwepo.Pia mke wa Rwigyema na mama mzazi wa Rwigyema wote wanaishi Kigali wakihudumiwa na Serikali ya PK.

kwa akili ya mafundisho ya kilokole kutoka mchungaji mwamposa, unaweza dhani kwa kufanya hivyo, PK ana roho ya upendo na moyo wa huruma sana.

ila kwa sisi tuliosoma cuba ya buza magengeni,hapo PK kaiweka hiyo familia kwenye circle yake ili iwe rahisi kuidhibiti, ku monitor idealogy yao, agenda zao na mienendo yao.ni mbinu nzuri ya kudeal na warithi wa adui yako ambaye ulishiriki kuondoa uhai wake.
 
Rwanda hakuna umoja ni propaganda tu na wala hakuna mhutu anaemkubali PK kinachoitwa umoja Rwanda ni watu kunyamazishwa kibabe kujadili matatizo yanayowakabili ila hakuna umoja, cake ya taifa yote inaliwa na watutsi huku wahutu wakiwa wametupwa huko mashambani vijijini hali yao mbaya kwelkwel wakati watutsi wakiwa wanajivinjari Mjini Kigali.
Watutsi wanapendelewa kupita kawaida hadi imefikia nje ya Rwanda mfano huku Tz watu woote wanajua ukisema wanyarwanda unamaanisha watutsi, yaan nje ya Rwanda mtutsi wa Burundi akisema yeye ni mnyarwanda watu wote wataamini ila mhutu wa Rwanda akisema yeye ni mnyarwanda watu watakataa na swali litakuwa ni moja tu mbona haufanani na wanyarwanda? (wakimaanisha watutsi) afu watamwambia unaonekana kama mrundi (wakimaanisha mhutu).
Hahahaaa, dah bongo kweli mnawadharau warundi na kuwatukuza wanyarwanda, ila uhalisia hauko hivyo
 
Nchi za kifalme hizo

Wanajua bila kuwa mwanajeshi huwezi kuzitawala.

Ndio maana watoto wanapelekwa jeshini kwanza then wanarithi nchi

..Husseni Mwinyi alipomaliza form 6 hakujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria.

..lakini ameshakuwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa, raisi wa Zanzibar, na kuna mipango ya kumfanya raisi wa muungano.
 
Kuna nchi wakati mwingine kutawaliwa na madikteta au krithishana ni afadhali kuliko kuacha demokrasia ichukue mkondo wake. Rwanda, Uganda ni nchi ambazo demokrasia yao ni mtutu wa bunduki.
Kagame yuko hapo ili kuweka mtengamano wa kisiasa nchini rwanda. Vinginevyo angeshtakiwa kwa kutungua ile ndege mwaka 1994.
Acha watawale, na watoto wao na wajukuu wao. Kinyume chake ni mtutu wa bunduki kutawala
Nani mwenye ushahidi kama aliitungua yeye?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pale kulikua na beef kati ya kagame na fred gisa rwegyema, kama ulivosema kagame alipoenda mafunzoni the issue ilikua Museveni alimpenda sana fred so ilikua zuga kwa kagame, ili jamaa akapindue kule ashike nchi, kagame ilimuuma na ukumbuke ni mwanzilishi wa RPF ndio maana wale founder wote wa RPF kagame aliwala vichwa maana walikua wanaona jamaa kadakia mchongo juu kwa juu, na Rwigyema ni mzaliwa wa Rwanda lakini akachanja mbuga kwenda Uganda ndio alikua moja ya makamanda hatari wa museveni, basi umafia wa PK kwa wenzake haujaanza leo kwenye vilima vya matimba akiwa na miaka 33 akauliwa na kuzikwa Remera, hadi hapo kagame akawa hana mpinzani wa maana tena, kwa ufupi ilikua hivo
Hii sio Kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom