Lwandamina ashusha tuhuma kwa kigogo yanga, ataja mambo 6 yaliyomuondoa Yanga

Lwandamina ashusha tuhuma kwa kigogo yanga, ataja mambo 6 yaliyomuondoa Yanga

kuteuliwa kwa mkwasa kulimfanya hadi julio kutamani ukatibu mkuu simba,akaanza kujileta karibu,afadhali hawakumpa maaana ningekuwa balaa kubwa zaidi ya mkwasa
 
Kati ya kosa waliofanya Yanga ni kumpa utendaji wa timu mtu ambaye aliwahi kuwa kocha kwenye timu hiyo na ku prove failure. Yeye atakuwa anaamini bado ni kocha bora na kusahau kuwa nu kiongozi na kuendelea kumkosoa , kutokumkubali, kutokumpa ushirikiano ama kutengeneza makundi ya hujuma kibongobongo miongoni mwa wachezaji.
Nakuunga mkono Mkuu
Hili Yanga Fc walilofanya ni kosa la kiufundi kwa hakika na kwa asili ya sisi Watz sio rahisi kwa Mkwasa kutoa ushirikiano kwa 100% au kumkubali kocha yoyote atakaekuja kuifundisha Yanga fc.

Vilevile kweli Lwandamina katoa hoja zenye mashiko na kuonyesha utofauti wa 'professional coach' na 'unprofessional coach'. Jambo alilonifurahisha ni hili la kuwafanyia wachezaji 'perfomance appraisal' kwani haya yanaonekana ktk kazi za mikataba. Mtu huzalishi vya kutosha lazima ukae pembeni

Anyway, ngoja tusikie na upande wa pili kama hoja zitajibiwa kwa hoja au vioja
 
huyu jamaa hakwepeshi maneno, suala la ngoma litakuja igawa timu jamaa hana msaada wowote sasa ivi yeye kila siku ni kuumwa tu na ndo tunasikia akipona analeta nyodo kucheza pumbavu sana.

mkwasa nae na tabia za kiswahili
 
Njaa ikizidi Kila Mtu atakimbia Akatafute Kulipo na Kula
 
huyu jamaa hakwepeshi maneno, suala la ngoma litakuja igawa timu jamaa hana msaada wowote sasa ivi yeye kila siku ni kuumwa tu na ndo tunasikia akipona analeta nyodo kucheza pumbavu sana.

mkwasa nae na tabia za kiswahili
Sa atakuwaje na tabia za kizungu!
 
Nimependa hapo Mkwassa anaenda kambini, anaahidi malipo afu hatekelezi. Kama wanasiasa wetu. Safi sana
 
Soka la bongo haliishi figisu,tatizo waliopewa dhamani ya kuendeleza soka wako pale Kwa maslahi yao..ilipaswa wabadilishe mifumo iliyopo kuendena na hali ya sasa..lakini bado tuna ule mpira wa kizamani.
 
Hili swala la kurekebisha mikataba ni la msingi sana hapa bongo, kuna wachezaji wanajiona wakimataifa hawa dawa yao ndio hiyo. Lwandamila umeongea point sana japokuwa mimi sio Yanga
 
Niliwahi kurushiwa clip moja watsup mashabiki wa Yanga wakimzonga Mkwassa na Mkwassa kuamua kuwapuuzia, kaingia kwenye gari na kuondoka.

Ile ilikuwa ni jeuri kubwa sana, na baada ya kusoma huu uzi nimeanza kuelewa kweli Mkwassa ni shida.
 
Lwandamina Amemaliza yake
Bado Mkwasa ili Tujue nani Bundi pale Jangwani.
 
Labda Mkwassa anataka arudishiwe timu yeye kama Kocha Mkuu
 
Labda Mkwassa anataka arudishiwe timu yeye kama Kocha Mkuu
Nakumbuka alishawahi kuwa kocha mkuu wa Yanga.
Sielewi aliifanikisha timu kwa kiwango gani.
Ila angekuwa kocha mwenye mafanikio angebaki kuwa kocha mkuu hadi sasa.
Poleni Watani
 
Nakumbuka alishawahi kuwa kocha mkuu wa Yanga.
Sielewi aliifanikisha timu kwa kiwango gani.
Ila angekuwa kocha mwenye mafanikio angebaki kuwa kocha mkuu hadi sasa.
Poleni Watani
Lini alikuwa kocha mkuu?
 
Back
Top Bottom