Eti wachezaji wasitokane na Yanga na Simba!!! Ujuaji mwingine unaleta sana fedheha! Na haya ndiyo matokeo yake.
Sasa si ubadili mfumo kwanza kwa kupeleka vijana wengi wazawa kwenye Academy za Ulaya na pia kuziboresha timu za majeshi na pia zile za mamlaka ili hizo Simba na Yanga zikose nguvu ya kuwa na wachezaji wengi kwenye timu ya Taifa!
Hispania kwenyewe wachezaji wao wengi wa Timu ya Taifa wanatoka Barceloba, Real Madrid na Atletico Madrid! Iweje nongwa kwa Simba na Yanga kutoa wachezaji wengi iwapo wana sifa zinazo stahili?
Huwa nakerwa sana kuwa na kiongozi asiye na mipaka kwa wasaidizi wake. Yaani kila sehemu unaingilia na kuvuruga vuruga tu! Sasa kuna umuhimu gani wa kuwa na wasaidizi au mgawanyo wamadaraka?