Makamanda kama kweli itatokea mtaanza kupokea pesa huko Majimboni kwenu kutoka kwa Freeman Mbowe basi ondoeni mashaka kabisa kuwa Mwenyekiti wenu tayari ni mtu wa Serikali na nirafiki wa watesi wenu lazima aogopwe kama ukoma.
Freeman Mbowe amekuwa akilalamika uongozi huu ni mgumu na hauna manufaa yoyote iweje leo atoe pesa kununua matatizo anayoyapata kwenye Uenyekiti kama ambavyo amekuwa akituaminisha hivyo kwa muda mrefu?!!
Nyie mnafahamu, Magari ya chama karibu yote yamepaki kwani hakuna pesa za matengezo, haya mapesa yanaletwa leo huyu ndugu yetu ni kwanini leo?
Nakwanini yasiende kutengeneza magari yetu?
Lakini pia zipo tetesi hizi hapa chini,
👇👇👇
TAMKO LA WAJUMBE KUELEKEA UCHAGUZI WA MWENYEKITI CHADEMA 21 January 2025
Team Mbowe wamejifungia nyumbani kwa Mbowe na nyumbani kwa Boni Yai tangu Mbowe aliporudisha Fomu.
Mpaka SASA timu hii imefanya tathimini kubaini mikoa ambayo wajumbe wake hawamuungi mkono Tajiri wa Chama Mbowe, tathimini hiyo imesema hata kama Mbowe angeungwa mkono na mikoa mitano kwa kura zote za mikoa hiyo bado atapigwa kwa zaidi ya kura mia saba mbele.
Kwahiyo wameazimia kutenga bajeti Billion 1.4 kwajili ya kununua wajumbe 700 wanaomuunga mkono LISU Wakati huo wanaomuunga mkono Mbowe bajeti yao ni 1,500 000 hadi Million 2 inategemea aina ya kila mjumbe.
Faida ya utajiri wa Mbowe ndani ya chadema ni kununua wajumbe?. SASA timu Mbowe inaelekea mikoani kufanya biashara ya wajumbe, karibuni niko hapa nasubiria Million 2 Mimi mpiga kura wa mbangaizaji mwenzangu Tundu LISU (kumbe kuwa upande wa LISU ni dili) Jamani kuwa Lisu sitoki ng'ooo!
Wajumbe wabangaizaji wenzangu tunao mpigia kura Tundu Lissu, hakikisha unapewa Million 2, hizo ni pesa zetu ambazo Mbowe amekuwa akipora toka kwenye ruzuku ya chama kwa kudai CHADEMA madeni hewa!
Ni lazima tuchukue hiyo pesa na kura zote tunapiga kwa Mwenyekiti Tundu Lissu ili tuweze kuokoa chama chetu toka kwa wala rushwa sugu! Wabangaizaji wenzangu mmeshuhudia jinsi tulivyo teswa na ma JOC, ZOC, WOC, Van Guards kwenye chaguzi za ndani, hatukuwa na mawakala wala wagombea,
Hakuna pesa ila wao wanatoka makao makuu na kuja majimboni wakiwa wanajilipa mishahara na posho kubwa, ni wakati wa Tundu Lissu kuongoza chama ili viongozi wa majimbo hadi misingi waweze kupata posho kama viongozi wa kamati kuu wanavyo jilipa! Viongozi wote tunajitolea kufanya kujenga chama, kwa nini Mbowe akijitolea inakuwa ni deni la CHADEMA?
Wabangaizaji tukidai jasho letu tunalo jitolea tunalipwa na nani? Azimio ni moja tu, kila mjumbe anaeletewa pesa ya tajiri Mbowe, ambayo tunajua amefadhiliwa na Abdul na Mama yake lazima tuichukue, lazima kila mjumbe apokee Million 2 na kura tunapiga kwa Tundu Lissu.
Bila kuchukua maamuzi haya magumu Mbowe hawezi kuelewa ni jinsi gani ameihujumu CHADEMA kwa maslahi yake binafsi na CCM