Kelly wala sikumbuki nilianzia wapi kuijua. Ila nakumbuka kupata ujumbe tuwe tuanachangia kuweka maneno. Nafikiri kama sikosei ni miaka ya 90 wakati nikiwa member wa Tanzanet forum. Ila naona kwa sasa wana nyimbo nyingi sana. Huwa nikitaka kufika huko naandika wimbo wa Tx Moshi akiwa POLISI JAZZ wa "unalewa bila kipimo". Huu wimbo kwa kweli naupenda sana na hamna sehemu unaweza kusikiliza. Ukiandika kwenye google zinatokea kama site mbili, moja ni humu JF na ya pili ni hiyo.
Inabidi HONGERA zimfikiei Tizedboy na wote waliochangia. Kama ikiwezekana, basi JF waisaidie hii site na kuiwekea LINK moja kwa moja kutoka humu JF. Nafikiri hiyo tumuachie Tizedboy mwenyewe. Vinginevyo JF itaanza kuwa kama Microsoft, ikipita na kuuwa au kununua vikampuni vidogovidogo. Na hii siyo nzuri sana.
Mwanzo niliandika kwa kufikiri jamaa kaweka nyimbo chache tu. Ila nilipoingia MAINPAGE duu, nimekubali. Mod's yale maneno yangu ya kwanza ya kutengeneza sehemu ya Lyrics za Kiswahili, muachane nayo. Ila kibidi kuisaidia hiyo site basi itakuwa vizuri maana ni nzuri na jamaa kajitahidi ila ndiyo haijulikani.