Aisee kuendesha biashara bongo ukiachana na TRA sisi wenyewe tunaharibiana. Yani mtz akiingia kazini ukiwa umempa ajira plan yake ni kutafuta namna akuibie. Hajali hasara unayopata. Unamwajiri mtu famasi, kumbe anakuja na dawa zake ndizo anauza wewe unashangaa hakuna mauzo. Kazi yako kumpa mshahara na kulipia fremu lakini kumbe yeye anauza dawa zake.