Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera, Faris Buruhani ametoa wito kwa viongozi wa vijana mkoani humo kusimama imara katika kulinda maslahi ya vijana wenzao hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, huku akiwakumbusha kwamba kazi waliyochaguliwa kuifanya ni kuwasimamia vijana ndani na nje ya vikao na si kupiga makofi tu vikaoni.
Wito huo umetolewa na ndugu Faris alipokuwa akizungumza na Baraza la Vijana wa CCM wilaya ya Bukoba mjini katika mwendelezo wa Kampeni maalum ya Kamati ya Utekelezaji mkoa ya kutafuta kura mpya za Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyopewa jina la "SANEVO" ambayo inaendelea mkoani Kagera.
Aidha, Faris amesisitiza kwa sauti kubwa kwamba vijana wa CCM mkoa wa Kagera wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi za Udiwani na Ubunge pale muda utakapofika huku akiwakumbusha kwamba wakati wa vijana ni sasa hivyo wasipumbazwe na maneno yaliyopitwa na wakati ya kuamini kesho ni bora kuliko leo.
Kampeni hii ya SAMIA NEW VOTERS inaendelea na inatarajiwa kukamilika April 29 katika wilaya ya Missenyi ambayo itakuwa wilaya ya mwisho.