M-Pesa, tiGO-Pesa na Airtel Money Kufa...

Kisendi

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Posts
699
Reaction score
179
Wana jf kuanzishwa kwa kodi kwenye utumaji wa pesa kupitia simu ni kama vile serikali imeona mabenki mengi yamekosa wateja na hatimaye kuanzisha huu mfumo utakaonza july 2013 baada ya bajeti ya mwaka huu kuptishwa.

Makampuni ya simu jipangeni hii ni strategy ya kuhamasisha wananchi waende benki, maana kuna benki zingine sasa zinakufa kwa sababu vijana wengi nao wanaweka hela zao kwenye simu.
 
Hii n I bahati mbaya sana kwani hii ilisaidia kufikisha some form of banking system mpaka vijijini. Serkali imekuwa nauwezo wa kupata taarifa za circulation ya pesa na watu wa vijijini na uwezo wa kutunza pesa zao kiusalama zaidi. Natumai hazitakufa ingawa kuzitoza kodi ni mpango mbovu.
 
Hii ni kodi kwenye commission na wala sio kwenye transaction. Nilivyoelewa mimi, wale agent wa MPESA kwa mfano, commission yao ya mwezi ndio itakata hiyo withholding tax.
 
Mkuu naomba unielekeze kuna aina ngapi za tax. Inaelekea wewe umesomea hayo mambo. Mimi nimesoma mambo ya afya, lakini niko interested sana na mambo ya biashara na uchumi.
 
sio kweli,
kwanza mobile money zimerahisisha huduma za mabenki na wala sio kuyaua..
tazama jinsi kila benki inavyokazana kuwezesha wateja wake kutumia mobile banking,...
pili mara nyingi watu hutumia mitandao kuweka fedha ndogo zisizozidi m 10 mfano..
kwa hivyo pesa nyingi watu watapeleka benki tu..
tatu ni kama alivyosema jamaa hapo..hiyo kodi mpya inachajiwa kwenye comission anayolipwa wakala na kampuni ya simu mwisho wa mwezi..kwa hivyo haiwezi kuathiri biashara ya mobile money namna hiyo..
 
Hii ya MPESA ingelikuwa mbaya kama kila transaction unayofanya serikali ingelikuwa inachukua tax. Ina maana sisi watumaji pesa tungeumia maana pesa zingelikuwa zinakatwa. Lakini hii isingeliweza kuwa asilimia 10 maana hiyo ni pesa nyingi sana.

Kwahiyo nafikiri walichoamua ni hiyo asilimia 10 kwenye commission ya agent. Inaitwa withholding tax kwa maana ya kwamba yule anayekulipa commission kama vile Vodacom, anakata 10% na kuikabidhi yeye mwenye kwa serikali. Njia nyingine ingelikuwa kukulipa pesa zote na kisha kukuambia kalipe mwenyewe kodi. Hii withholding tax ndio inatumika hata kwenye kupanga nyumba au ofisi. Yule mpangaji badala ya kulipa pesa zote anakata 10% na kuifikisha yeye mwenyewe serikalini pamoja na mkataba wa kupanga.

Mkuu naomba unielekeze kuna aina ngapi za tax. Inaelekea wewe umesomea hayo mambo. Mimi nimesoma mambo ya afya, lakini niko interested sana na mambo ya biashara na uchumi.
 
Ahaa leo nimejua jina lako maana comment zako zinafanana na dada mmoja wa Tanuru la Fikra kule FB ambae ni rafiki yangu sana anaitwa Tu..............! ! ! Nae pia amesomea mambo ya Afya.Interesting indeed!
Kijana ningependa nijue ajira yako tafadhali kwa sababu naona ile kazi ya kubeba sumu kila mtu kaishtukia

Unaonaje ukaja kupiga boksi upate mkwanja wa nguvu kuliko kuishia kuwa kibaraka wa mtu?
 
Muathirika ni mtu wa mwisho ambaye ni mtumiaji haya mambo ya comission na agent hakuna anayeathirika, mwisho wa siku mpesa tigopesa airtel money zitakufa coz watumiaji watashindwa gharama zake.
Sasa hivo tu mpesa gharama zimepanda kutuma hela na kupokea je hiyo kodi ikiwekwa?
 
Mkuu naomba unielekeze kuna aina ngapi za tax. Inaelekea wewe umesomea hayo mambo. Mimi nimesoma mambo ya afya, lakini niko interested sana na mambo ya biashara na uchumi.

Kuna withholding tax ambayo makampuni ya cim yanatakiwa kuwakata maagent wanapowalipa commission and then kuna ushuru wa 14% kwa huduma zote ikiwapo hiyo ya money transfer.
 
Hii ni kodi kwenye commission na wala sio kwenye transaction. Nilivyoelewa mimi, wale agent wa MPESA kwa mfano, commission yao ya mwezi ndio itakata hiyo withholding tax.

Tupo pamoja mimi ndivyo nilivyoelewa.
Kwani hawa mawakala wamekuwa wakila mapato ya Bure bila kulipa Kodi, Ilikuwa ni moja ya Biashara zisizo na Kodi.
 
Kuna withholding tax ambayo makampuni ya cim yanatakiwa kuwakata maagent wanapowalipa commission and then kuna ushuru wa 14% kwa huduma zote ikiwapo hiyo ya money transfer.

14% ya Transfer kivipi? Kwani wameambiwa hiyo ni Faida au ni mtu anatuma hela tu. Hiyo Kamisheni yenyewe haifiki 5% itakuwa Tax ?
 
Muathirika ni mtu wa mwisho ambaye ni mtumiaji haya mambo ya comission na agent hakuna anayeathirika, mwisho wa siku mpesa tigopesa airtel money zitakufa coz watumiaji watashindwa gharama zake.
Sasa hivo tu mpesa gharama zimepanda kutuma hela na kupokea je hiyo kodi ikiwekwa?

baada ya voda kuongeza gharama za kutuma na kutoa pesa m-pesa zimepungua na baada ya airtelmoney kuanza kutoza gharama airtelmoney imekufa hivo vi benk navyo nowdayz vimekuwa uyoga hiv huduma za nmb unategemea watu bado waipende bank!
 
Tupo pamoja mimi ndivyo nilivyoelewa.
Kwani hawa mawakala wamekuwa wakila mapato ya Bure bila kulipa Kodi, Ilikuwa ni moja ya Biashara zisizo na Kodi.

mmh mkuu una uhakika na unachokisema hapo kwa red? mkuu biashara ya mpesa sijui tigopesa si stand-alone business, ndo maana kama huna biashara nyingine inayo-operate (yenye biashara) hawakupi uwakala. Kwangu mimi kuwakata kodi ni kuwaonea na ni double standard kwa sababu hawa watu tayari wanalipa kodi TRA kwa biashara anayoifanya, so utamkataje tena kodi mara mbili?

Ni sawa na mtu ana duka lake analipa TRA halafu bado unamkata ten kodi kwa kila item anayouza, that's crazy!!
 
Kama wanalipa kodi kwenye hizo biashara sanjari haimaanishi wasilipe kwenye hii ya kutuma pesa. Ikumbukwe pia kwamba kodi hii ni copy paste ya nchi jirani ikiwemo Uganda. Na vile vile naamini upo uwezekano mkubwa wa makampuni kuongeza viwango vya ada ili kulinda faida zao. Hii ina maana kodi hii itaishia kulipwa na mtumiaji. Na kwa Bahati mbaya wanaotumia huduma hizi ni wananchi wa kipato cha kati na zaidi cha chini. matajiri na pesa zao nyingi bado wako na mabenki.

Mtoa mada ana wajibu wa kuweka ushahidi wa namba kwamba viwango vipya vya ada vitazidi viwango vya mabenki na hivyo kusababisha kufa kwa huduma hizi.
 
sio kweli,
kwanza mobile money zimerahisisha huduma za mabenki na wala sio kuyaua..
tazama jinsi kila benki inavyokazana kuwezesha wateja wake kutumia mobile banking,...
pili mara nyingi watu hutumia mitandao kuweka fedha ndogo zisizozidi m 10 mfano..
kwa hivyo pesa nyingi watu watapeleka benki tu..
tatu ni kama alivyosema jamaa hapo..hiyo kodi mpya inachajiwa kwenye comission anayolipwa wakala na kampuni ya simu mwisho wa mwezi..kwa hivyo haiwezi kuathiri biashara ya mobile money namna hiyo..

Kweli kabisa maana haya ni ma-gap ambayo serikali inmekuwa ikiyaachia kama vile zamani kwenye mpira wa miguu walivyokuwa hawalipi PAYE mwisho siku wafanyakazi ndio wanaumia kwa kukatwa ela kubwa wakati kuna watu wanaingiza mamilioni ya hela kwa mwezi more than 10 m alafu ukute analipa kodi 30,000 (alfu thelasini) wakati huo huo mfanyakazi mshahara let say million anakuja kulipa karibu laki 3 kodi
 
Kama wanalipa kodi kwenye hizo biashara sanjari haimaanishi wasilipe kwenye hii ya kutuma pesa. Ikumbukwe pia kwamba kodi hii ni copy paste ya nchi jirani ikiwemo Uganda. Na vile vile naamini upo uwezekano mkubwa wa makampuni kuongeza viwango vya ada ili kulinda faida zao. Hii ina maana kodi hii itaishia kulipwa na mtumiaji. Na kwa Bahati mbaya wanaotumia huduma hizi ni wananchi wa kipato cha kati na zaidi cha chini. matajiri na pesa zao nyingi bado wako na mabenki.

Mtoa mada ana wajibu wa kuweka ushahidi wa namba kwamba viwango vipya vya ada vitazidi viwango vya mabenki na hivyo kusababisha kufa kwa huduma hizi.

Mkuu umepambanua vizuri ila hapo kwa red inaweza kuwa kinyume chake. Unajua haya makampuni yana ushindani sana ktk hizi huduma zao, vile vile wana ushindani toka kwenye mabenki. Kwa mtazamo huu wanaweza wasiongeze viwango vya ada kwa kuhofia kupoteza wateja, badala yake mawakala ndo wakaishia kulipa hiyo kodi.

Nasema hivi kwa sababu kwa uzoefu wangu mdogo nimegundua haya makampuni yanaburuza sana mawakala, partly kwasababu mawakala wenyewe wako disorganized, hawana umoja wa kuwasemea so hawana ubavu wa kugomea hizo rates, pia wengi wao hawana option na wanategemea hii biashara kwa mulo wao wa siku. Kama umeishawahi kufanya hii biashara utaelewa ninachomaanisha au ukiongea na mawakala wenyewe ndo utasikia malalamiko yako khs commission kiduchu wanazopewa, sometimes wanakatwa bila maelezo na hawana pa kusemea! akienda ofisini kulalamika anaambiwa ukitaka acha biashara, mwingine apewe hiyo laini, na hivi customer care ni zere, it's so crazy!!
 
Kijana ningependa nijue ajira yako tafadhali kwa sababu naona ile kazi ya kubeba sumu kila mtu kaishtukia

Unaonaje ukaja kupiga boksi upate mkwanja wa nguvu kuliko kuishia kuwa kibaraka wa mtu?
Mind your own business!!
 
Back
Top Bottom