M23 inaelekea Bukavu mjini

M23 inaelekea Bukavu mjini

TOKA MAKTABA :

12 February 2025

Bukavu, Sud Kivu

GAVANA AOMBA RAIA : MAHARAGE, UNGA NA DAGAA KWA AJILI YA JESHI LA SERIKALI YA KONGO FARDC

View: https://m.youtube.com/watch?v=dHysQuXyOoI
Gavana mheshimiwa Jean-Jacques Parusi wa Jimbo la Kivu Kusini alipokuwa anaomba raia wawapatie msaada wa unga wa sembe, maharage na dagaa askari wa jeshi la Serikali ya Kongo FARDC ili waweze kupambana na M23

RAIA WASEMA KUWA ASKARI WA SERIKALI WAFANANISHWA NA PANYA RODI / VIBAKA. SABABU ZATAJWA :
Jeshi la serikali ya Congo FARDC wanajeshi wake wanakosa mishahara kwa miezi kibao, vifaa chakavu kama sare na buti za vita, njaa na pia viongozi waliopo makao makuu ya nchi kule Kinshasa kutowapatia rasilimali hizo muhimu ili askari kuwa na morali ya kuipambania serikali ya rais Felix Tshisekedi

Pia upande mwingine maofisa wa Jeshi la FARDC wanaoongoza brigedi, vikosi na kombania waliopo mstari wa mbele wanashiriki katika uporaji wa maliasili kama madini n.k Huku wakilazimisha askari wapiganaji kuwa na nidhamu kwa utawala wa Kinshasa.

Matokeo yake askari wa FARDC wamegeuka kuwa panya rodi na vibaka kwa kuwapora raia ili wajikimu wao na familia zao. Hii imejenga chuki na kutoaminiwa na raia kwa askari wa serikali kukosa nidhamu, hivyo popote FARDC ilipo wananchi wanaishi kwa hofu.

Raia wanasema ukikutana na askari wa serikali ukiwa na simu mobile au cash mfukoni, wakikupora bila kukuua utakuwa na bahati kubwa Mungu anakusimamia, wengi wamepoteza maisha kutokana na kukumbana uso kwa uso na FARDC.

Maeneo yanayokaliwa na M23 kuna utawala wa sheria, askari wa M23 wana nidhamu ya hali ya juu pia morali ya kufika Kinshasa kuchukua nchi ili kubadilisha hali mbaya waliyonayo wakongomani wote.
 
Mwanzo madai ya M23 yalikuwa kwamba jamii ya banyamulenge iliyokuwa ikiishi boma Kwa wingi ilikuwa inaonewa hivo wakaunda kundi Kwa ajili ya kujilinda , ila sasa wanaitaka Congo yote Kwa ujumla Hawa M23 Wana ajenda Yao nyuma ya pazia iweje wasisalie Goma kwanini wanaitaka Congo yote je wao ndo wanazani watakuwa watawala wazuri wa Congo?
Usisahau vita ya Kagera lengo lilikuwa kumfurusha nduli kwenye eneo aliloteka na kujimilikisha eti ni la Uganda. Lakini mtifuano ulikwenda hadi mpakani na Sudan kusini.
 
Kweli ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi
 
Attachments

  • Screenshot_20250214_210637_Gallery.jpg
    Screenshot_20250214_210637_Gallery.jpg
    211.6 KB · Views: 1
12 February 2025

Bukavu, Sud Kivu

GAVANA AOMBA MAHARAGE, UNGA NA DAGAA KWA AJILI YA JESHI LA SERIKALI YA KONGO

View: https://m.youtube.com/watch?v=dHysQuXyOoI
Gavana mheshimiwa Jean-Jacques Parusi wa Jimbo la Kivu Kusini alipokuwa anaomba raia wawapatie msaada wa unga wa sembe, maharage na dagaa askari wa jeshi la Serikali ya Kongo FARDC ili waweze kupambana na M23

Mkuu nakuamini Sana kwenye habari kwa kina 😀
 
TOKA MAKTABA :

12 February 2025

Bukavu, Sud Kivu

GAVANA AOMBA RAIA : MAHARAGE, UNGA NA DAGAA KWA AJILI YA JESHI LA SERIKALI YA KONGO FARDC

View: https://m.youtube.com/watch?v=dHysQuXyOoI
Gavana mheshimiwa Jean-Jacques Parusi wa Jimbo la Kivu Kusini alipokuwa anaomba raia wawapatie msaada wa unga wa sembe, maharage na dagaa askari wa jeshi la Serikali ya Kongo FARDC ili waweze kupambana na M23

Jeshi la serikali ya Congo FARDC wanajeshi wake wanakosa mishahara kwa miezi kibao, vifaa chakavu kama sare na buti za vita, njaa na pia viongozi waliopo makao makuu ya nchi kule Kinshasa kutowapatia rasilimali hizo muhimu ili askari kuwa na morali ya kuipambania serikali ya rais Felix Tshisekedi

Matokeo yake askari wa FARDC wamegeuka kuwa panya rodi na vibaka kwa kuwapora raia ili wajikimu wao na familia zao. Hii imejenga chuki na kutoamimiwa na raia kwa askari wa serikali kukosa nidhamu, hivyo popote FARDC ilipo wananchi wanaishi kwa hofu.

Kwa sasa anaongelea Bujumbura
 
Uganda, Tanzania, Kenya, Malawi, Rwanda, South Africa, Somalia wote walisisitiza mazungumzo ya maridhiano mezani lakini watawala wa Bujumbura Burundi na Kinshasa DR Congo wao hawakutaka mapendekezo ya nchi hizo 8 wakiamini watashinda kwa risasi na mabomu.

Sasa nchi hizo 8 wameamua wawe watazamaji kuona kama Bujumbura na Kinshasa wataweza kushinda katika uwanja wa mapambano walioutaka.
Kwa hali ilivyo ingekuwa bora kwa sasa M23 wasiitwe tena Waasi wa M23 bali waitwe Jeshi la Ukombozi la M23 au ikipendeza waitwe Jeshi la Kimapinduzi la M23.
Jeshi la Congo DRC na washirika wake inaonekana walikuwa wamejikita kwenye matumizi ya mkongo na sio kuilinda nchi.
 
Mwanzo madai ya M23 yalikuwa kwamba jamii ya banyamulenge iliyokuwa ikiishi boma Kwa wingi ilikuwa inaonewa hivo wakaunda kundi Kwa ajili ya kujilinda , ila sasa wanaitaka Congo yote Kwa ujumla Hawa M23 Wana ajenda Yao nyuma ya pazia iweje wasisalie Goma kwanini wanaitaka Congo yote je wao ndo wanazani watakuwa watawala wazuri wa Congo?
M23 ni sehemu ya muungano wa makundi ya waasi wa Kongo Congo River Alliance kwahiyo wanasaidiana.
 
Jamani, kuna kitu bado hamjaelewa. UN iliposema M23 inazidi jeshi lake uwezo, na kumbuka ndo anajifanya asikali Polisi wa dunia hii, huoni nyuma yake kuna jambo? Kama serikali ilishanyanganywa ardhi yake, hao hao wa UN wakaendelea kuoperate hapo hapo, jiulize ni kwa makubaliano na nani. Hii vita ina unafiki mkubwa sana. Jiulize warundi Elfu 10 waliopelekwa kuhakikisha uwanja wa ndege huo hauanguki, vita hivyo vya kitoto?
Tumeambiwa walitimua vumbi hata wakasahau buti zao pale uwanja wa ndege kutokana na kisago walichopelekewa na M23
 
Afrika inasikitisha sana kwahili la kongo lazima tuonekane wa ajabu sana, anayekufanyia ubaya ndiyo unamuamini hawa watu siyo wazuri kwetu. Leo kwa mwenzio kesho kwako
 
Gavana mheshimiwa Jean-Jacques Parusi wa Jimbo la Kivu Kusini alipokuwa anaomba raia wawapatie msaada wa unga wa sembe, maharage na dagaa askari wa jeshi la Serikali ya Kongo FARDC ili waweze kupambana na M23
Askari ambaye hajala chakula siku mbili hapewi chakula lakini anapewa risasi na mabomu anaweza hata akawauzia waasi risasi na mabomu ili apate chakula.

Hakuna adui mbaya kama njaa.
 
M23 ni sehemu ya muungano wa makundi ya waasi wa Kongo Congo River Alliance kwahiyo wanasaidiana.
Mbona wanaitwa waasi ilhali wanao huo umoja wao? Kwa nini wasiitwe Wapiganaji wa Vuguvugu la kuikomboa Congo DRC kwani majeshi ya Congo DRC yameshatepeta mazima.
 
Afrika inasikitisha sana kwahili la kongo lazima tuonekane wa ajabu sana, anayekufanyia ubaya ndiyo unamuamini hawa watu siyo wazuri kwetu. Leo kwa mwenzio kesho kwako

Viongozi wakubwa wa nchi ni walafi, wanatumia kodi za wananchi kujinunulia magari ya kifahari, rushwa, ufisadi huku umma mkubwa wakiishi katika umasikini wa kutisha na wanaona maisha ya viongozi wao wa kiserikali yalivyo ya kifahari.
 
God bless M23.

M23 sio wahasi, ni wakombozi wa nchi ya DRC
 
Mbona wanaitwa waasi ilhali wanao huo umoja wao? Kwa nini wasiitwe Wapiganaji wa Vuguvugu la kuikomboa Congo DRC kwani majeshi ya Congo DRC yameshatepeta mazima.
Wengi wao walikuwa ni Wanajeshi wa Kongo kabla ya kuasi ndio maana wanaitwa Waasi.

Tishekedi aache kiburi akae nao chini wayajenge vita iishe asisubiri mpaka wafike Uvira Kalemie Moba Lubumbashi wakifika huko wanaweza kuongeza masharti.
 
Wengi wao walikuwa ni Wanajeshi wa Kongo kabla ya kuasi ndio maana wanaitwa Waasi.

Tishekedi aache kiburi akae nao chini wayajenge vita iishe asisubiri mpaka wafike Uvira Kalemie Moba wakifika huko wanaweza kuongeza masharti.
Muda umekwisha, Tishekedi imebakia siku za kukimbia DRC
 
Askari ambaye hajala chakula siku mbili hapewi chakula lakini anapewa risasi na mabomu anaweza hata akawauzia waasi risasi na mabomu ili apate chakula.

Hakuna adui mbaya kama njaa.
Duh! M23 wameigundua dosari hiyo na wamewabana kwenye udhaifu huo na kweli wamenyong'onyea - wameishiwa kabisa morali hadi nguvu iliyobakia kwao ni ya kukimbia ili kujiokoa na sio kupambana tena.
 
Viongozi wakubwa wa nchi ni walafi, wanatumia kodi za wananchi kujinunulia magari ya kifahari, rushwa, ufisadi huku umma mkubwa wakiishi katika umasikini wa kutisha na wanaona maisha ya viongozi wao wa kiserikali yalivyo ya kifahari.
Hapa ndo wanakuja kuyaacha na kukimbia na familia zao. Walianza kama waasi,wanapigiwa mwano, leo hii wanasubiliwa kwa hamu na kukaribishwa kwa shangwe. Si raia wanajua M23 haina shida na raia!!! Ikiendelea hivo mbona mzee big atakoma. We jiulize watu wanaitwa kuendelea na kazi, kwa mikataba yao ile ile,mishahara yao,ile ile, nani atageuka!
 
Duh! M23 wameigundua dosari hiyo na wamewabana kwenye udhaifu huo na kweli wamenyong'onyea - wameishiwa kabisa morali hadi nguvu iliyobakia kwao ni ya kukimbia ili kujiokoa na sio kupambana tena.
M23 inawambia nyie ni raia wenzetu, tatizo ni uongozi wala msijali. Wanapokelewa, bila kujali wameua wenzao, wanapewa chakula,wanalala,mishahara yao bado iko pale pale watalipwa, unadhani nani afurukute!
 
Back
Top Bottom