Mr Chromium
JF-Expert Member
- Aug 20, 2020
- 2,761
- 3,835
- Thread starter
- #21
ni huzuni kwakweli
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ni huzuni kwakweli
Mfumo mzuri ni kuwa nchi ijitosheleze yenyewe kimahitaji yote na sio kuwaza kutegemea kwengineko.Wote hatuwezi kuzalisha kitu kimoja (industrial products) wakati ukanda wetu natural unatufeva kwa kilimo,mifugo,madini na mazao ya majini,pakiwa na usawa wa uuzwaji wa rasilimali zetu.
Nakupa mfano mdgo tuu sisi tunapokea saa (iwe ubora mdgo,imetumika etc) na kwa bei wanayotaka wao.
Ikija upande wetu wanachagua bidhaa bora na nyingi kwa jinsi wanavyotaka wao,hawajali mkulima wao wanajiangalia wao.
Nikimaanisha hakuna usawa au uwiano wa pesa za kuweza kumnufaisha muafrika.
Mfumo wa elimu hauleti tija kwa vijana kuweza kuwa competitive kwenye suala la technically sana sana tutaishia kutoa copy tu baada ya ku assembly vifaa kutoka kwao.Mfumo mzuri ni kuwa nchi ijitosheleze yenyewe kimahitaji yote na sio kuwaza kutegemea kwengineko.
Utawaza kutegemea kwengineko ikiwa tu huna icho kitu.Ardhi ya Afrika haiwezi kuendeleza teknolojia?
Tuboreshe hiyo elimu afu pia wapo fundi makenikia kama fundi gereji bahadhi wapo vizuri tuMfumo wa elimu hauleti tija kwa vijana kuweza kuwa competitive kwenye suala la technically sana sana tutaishia kutoa copy tu baada ya ku assembly vifaa kutoka kwao.
Uzi huu upo kitechnologia zaidi kuliko M23 yenyewe!
Wakati dunia inaamuka kuanza kutumia majeshi binafsi nchi za ulaya na USA ziko miaka 100 mbele yetu wakati huo Nchi za africa ziko karne mbili nyuma bado zinadanganywa na Western democracy, Human right, UN na rule of law,I CJ court.
Kifupi nchi za Africa na Waafrica wenyewe wamelala fofo hawaelewi kinachoendelea na kama wapo wanaoelewa bas kamwe hawatapata nafasi katika serikali wala kufanya maamuzi.
“Ni sawa na mtoto mchanga anaona mambo ya giza lakin hana uwezo wa kusema wala kuzuia lakini mtu mzima Haoni hivo hawezi pambana na asichokiona.”
Private military au Majeshi binafsi yameanza kipindi cha vita baridi na taaratibu yameshika kasi tangu hapo. Miaka ya 2000 katika vita ya Iraq ndipo kushamili na majeshi mashuhuli hapa ni kama PCM na Black water. Yapo mengi kutoka British pia
Nje za nchi za magharibi Russia ime make headline kubwa na kundi lake la Wagner huku likiwa na mchango katika ku annex crimea na katika vita ya Ukraine.
Pia katika mapinduzi mbalimbali katika nchi za Africa kama Mali,bukinafaso, Africa ya kati na kadharika
KWANINI PRIVATE ARMY
- Kuepuka nchi kutuhumiwa na sheria za kivita
- Kuweza kutofautisha kati ya msimamo wa nchi na serikali
- Kukimbia uwajibikaji katika madhambi yanayofanywa na majeshi haya
- Kuficha uwepo wa serikali fulani ya nchi katika migogoro ya vita
M23 Ni kundi linalopigana na DRC. Kwa haraka haraka Utaona jinsi hii project inavoratibiwa hutasikia Nchi zinazohusika zikishutumiwa hata zikishutumiwa inakua ni unafiki kupooza soo! Madai fake yanayotengenezwa kama justification kuua watu zaidi.
Ukweli nchi za maziwa makuu zinaelewa fika Jeshi hili private linamilikiwa na nani? Hivo nyingi zinajiepusha hata kama zinajua Adui anawatafuna taratibu
Nchi za magharibi zinatumia jeshi private au binafsi ili kuepusha mambo kadhaa;
Ni kama uko baa unakata kiuno na umelewa bia na nyumba yako inaungua hata ukiambiwa akili yako haifanyi kazi muda huo ila wewe unaimba amapiano tu.
- Upinzani kutoka kwa waafrica (wangeweka majeshi yake waafrica wangeweza kuungana kupambana)
- Kutengeneza Image kwa Dunia kusema ni vita ya wenyewe kwa wenyewe (Jiulize hao watu wameishi wenyewe kwa zaidi ya miaka 400 wapigane leo, inaingia akilini?).
- UN inatumika kuendelea kufanya mgogoro usiishe
- Vyombo vyao vya ICJ, human right na media zinatumika kufubaza taarifa zisitoke na kuwachanganya waafrica wasifahamu kama nyumba inaungua wao wapo wanacheza mziki wa mzungu!!
- Watu wakiangalia mgogoro huu wanaona DRC na m23 lakini si kweli ni DRC vs Western mercenary. Kilichotokea Ethiopia kina reflect kinachotokea hapa Congo. Nani angeweza dhan jeshi la Tigray nusura liangushe jeshi la Ethiopia na Eritrea pamoja? Ni wenyewe hapana.
Ni pombe itapoisha ndipo utajua huna hata kwa kwenda nyumba ilishaisha,vitu vyote hamna tena, familia yako imefia huko naww umebaki mkimbizi!
Uhalisia uliopo Congo hata Hitler asingeweza kufanya hivo wala King leopard wa Congo hafiki.
“Wakati kwene Vita ya pili ya dunia shetani alituma Majeshi yake kuangamiza ila CONGO SHETANI AMESHUKA KABISA.“
Kweli hawa jamaa wanamaslahi yao DRCKweli pale kunawazunguma wako nyuma ya M23, ndo mana hata kiongozi wa M23 akenda ughaibuni akamatwi kwa uharifu wa kivita .
Hii taarifa yako haionyeshi chanzo na muendelezo wa shida ya KivuUmeanza vizuri ila ulipofika hapo kwenye mtoto mdogo kuona mambo ya giza umeharibu.
Mambo ya Kongo yana historia ndefu.
Shida ilianza pale wareno walipofika ngambo ya maji ya mto Kongo upande wa bahari ya Atlantic na wakongoman wenyewe kuanza kuwindana kuuza watumwa kwa wareno hao na wengineo.
Mfalme wa kongo Afonso aliona shida hii lakini alikosea kuamini kuwa yeye kufata matakwa ya wageni itamsaidia na hata alipotuma ujumbe wake kwa mfalme wa Ureno (ujumbe huu uliundwa na familia ya Afonso). Ujumbe huo haukufika mpaka leo hii.
Henry Morton Stanley na mikataba yake ya hadaa kwa viongozi wa kabila za Kongo iliandaa kutawaliwa na mfalme Leopold.
Kwa miaka mingi ukoloni ulitawala mpaka wabelgiji wanaondoka. Patrice Lumumba kuuwawa kinyama na Mobutu kulihakikisha kuwa Kongo itakua ya aina gani.
Ukabila na uingiliwaji na mataifa mengine kumeifanya Kongo iwe ilivyo mpaka sasa
Safari bado ni ndefu kupata suluhisho!
Chanzo ni ukabila na uchu wa madaraka.Hii taarifa yako haionyeshi chanzo na muendelezo wa shida ya Kivu
Laana hii inatoka wapi. Tafadhali elezea kinagaubaga. Karibu...Hata kama utakataa lakini ukweli ni kwamba Afrika na waafrika tumelaaniwa. Mifano hai ipo mingi tu hata hapo ulipo ipo.
Historia ya wakimbizi toka sehemu hiyo ni ndefu Sana hata kabla Tanzania au Congo hazijapata Uhuru. Kulikuwa na hao wakimbizi Tabora na Sumbawanga na wengine wakaolewa au kuoa na kupata watoto,vijukuu na vilembwe. Muongezeko wa hao wakimbizi au watusi, wengine ni juhudi za kimkakati za kuimega DRC na hizo maliasili. Dawa yao ni kuwahisha wasiishi hapo mpakani wapelekwe magharibiChanzo ni ukabila na uchu wa madaraka.
Hao M23 ni watusi wa Kongo. Kivu ina utajiri wa madini yanayotengeneza hizi malighafi za vifaa vya elektroniki pamoja na aina zingine za madini.
Wakongoman kwa maana ya wabantu hawataki kuwatambua watusi hawa kama wakongo toka enzi za Mobutu. Hawahesabiwi kama wananchi wa Kongo. Wanahitajika kurudi kwao Rwanda.
Ilihali watusi hawa toka miaka ya zamani kabla ya ukoloni waliishi humo Kongo. Mipaka ilivochorwa na wakoloni wakatenganishwa.
Ilipotokea mauaji ya Kimbari Rwanda 1994 wakimbizi baadhi walikimbilia Kongo na wakati wa kurudi hawa wa Kivu waliokua wakikaa humo toka enzi walitakiwa nao warudi ndo waliitwa Banyamulenge.
Matokeo yake ni vita vya silaha vilianza
Baada ya Kagame (mtusi,) kushinda walianza kuwasapoti hao watusi wa Kongo pamoja na misaada ya nje pia
Angola, Zimbabwe ya Mugabe, Uganda ya Museveni nao walimega keki kubwa sana huko Kongo na ndio walimsapoti Laurent Kabila na kusimika serikali yake.
Rwanda akiwa kinara. Na hata jeshi la Kongo lilifunzwa na Rwanda na viongozi wake wengi walikua watusi nk.
Wakati huo miaka ya 90 ilikua ni kwa ajili ya ulinzi kwani majeshi yaliyotekeleza mauaji ya Rwanda yalikimbilia Kongo wakati huo Mobutu akiwalinda. Baadae majeshi haya haya yaliingizwa kwenye mfumo wa jeshi la Kongo ikiwamo na hao watusi
Baadae ilikua ni unyonyaji wa madini. Coltan iliyochotwa huko kinyemela ni nyingi hadi sio poa.
Waliposhindwana ndio kujitenga na vita kuanza moja.
Itoshe kusema kuwa suluhi ya Kongo itapatikana na wakongoman wenyewe.
Vidonda vya mauji ya kila mara mpaka sasa watu karibu milioni 5 washafariki juu ya hivi vita. Sijajua wataviponyaje.
Ila wanabidi wakae mezani na kutatua tofauti zao. Pia kuepuka muingiliano wa nje katika suluhu hizi