M23 ni private mercenaries wa Marekani na Ulaya. Wazungu wako miaka 100 mbele

Maisha yetu tu ya huu umaskin ni shida tupu. Sasa inapotokea Tena vita inakuwa ni jehanamu kabisa. Na

Na hii yote inasababishwa na ujinga na upumbavu wetu wenyewe.. na wakati mwingine tunalaumu viongozi wetu ambao ni zao la watu wajinga na walio na shida. Hawawezi kutatua tatizo Kwa sababu afrika issue ya uongozi hatuiwezi. Narudia Tena sisi wafrika issue ya uongozi hatuiwezi..

Bahati mbaya walishajua sisi ni mambulula wanatumia huo udhaifu kutuadhibu...
 
Kila baya la Mwafrika anapewa Marekani,hao viongozi wanajukumu gani sasa
 
Mfumo mzuri ni kuwa nchi ijitosheleze yenyewe kimahitaji yote na sio kuwaza kutegemea kwengineko.

Utawaza kutegemea kwengineko ikiwa tu huna icho kitu.Ardhi ya Afrika haiwezi kuendeleza teknolojia?
 
Mfumo mzuri ni kuwa nchi ijitosheleze yenyewe kimahitaji yote na sio kuwaza kutegemea kwengineko.

Utawaza kutegemea kwengineko ikiwa tu huna icho kitu.Ardhi ya Afrika haiwezi kuendeleza teknolojia?
Mfumo wa elimu hauleti tija kwa vijana kuweza kuwa competitive kwenye suala la technically sana sana tutaishia kutoa copy tu baada ya ku assembly vifaa kutoka kwao.
 
Mfumo wa elimu hauleti tija kwa vijana kuweza kuwa competitive kwenye suala la technically sana sana tutaishia kutoa copy tu baada ya ku assembly vifaa kutoka kwao.
Tuboreshe hiyo elimu afu pia wapo fundi makenikia kama fundi gereji bahadhi wapo vizuri tu
Na sio mbaya Bora tuanze na hizo kopy huku tukibadili formula kidogo kama china Ili isiwe mizozo.

Mi nadhani tukianza nahili tutahamsha hali ya ufikiriaji wa mambo ya kisayansi na kuboresha na ata huko mbeleni tugundua kitu ila kwasasa kuanza tu na kugundua vitu vyetu ni ngumu maana wapo waliotutangulia kimandeleo na wamegundua vitu muhimu katika nyanja hizo
 
 
Makapuni ya marekani ,china na ulaya yanauza silaha
Eu na marekani wanapatanisha
Africa wanalaumiana
Wanaharakati wa ulaya na marekani wanalaumu na kushitaki Serikali za kiafrica
China analaumu Marekani na ulaya kwa kuuza silaha Africa
Marekani na ulaya wanalaumu China na urusi kwa kuuza silaha Africa
Umoja wa Mataifa wasuluhisha
Afrikaaaaaaaaaaa
 
Nafurahi sana kuona watu kama mleta mada kwamba bado tupo baadhi ya waafrika tunaoelewa na kufuatilia siasa za kimataifa na kuzielewa.

Kilichobaki tujiulize nini cha kufanya
 
Hata kama utakataa lakini ukweli ni kwamba Afrika na waafrika tumelaaniwa. Mifano hai ipo mingi tu hata hapo ulipo ipo.
 
Mleka mada umetumia Google kutafsiri andiko maana u aż Unguja sana na unarudi palepale na kwa taarifa mali na Burkina Faso hakuna wagner ni propaganda
 
Umeanza vizuri ila ulipofika hapo kwenye mtoto mdogo kuona mambo ya giza umeharibu.

Mambo ya Kongo yana historia ndefu.

Shida ilianza pale wareno walipofika ngambo ya maji ya mto Kongo upande wa bahari ya Atlantic na wakongoman wenyewe kuanza kuwindana kuuza watumwa kwa wareno hao na wengineo.

Mfalme wa kongo Afonso aliona shida hii lakini alikosea kuamini kuwa yeye kufata matakwa ya wageni itamsaidia na hata alipotuma ujumbe wake kwa mfalme wa Ureno (ujumbe huu uliundwa na familia ya Afonso). Ujumbe huo haukufika mpaka leo hii.

Henry Morton Stanley na mikataba yake ya hadaa kwa viongozi wa kabila za Kongo iliandaa kutawaliwa na mfalme Leopold.

Kwa miaka mingi ukoloni ulitawala mpaka wabelgiji wanaondoka. Patrice Lumumba kuuwawa kinyama na Mobutu kulihakikisha kuwa Kongo itakua ya aina gani.

Ukabila na uingiliwaji na mataifa mengine kumeifanya Kongo iwe ilivyo mpaka sasa

Safari bado ni ndefu kupata suluhisho!
 
Hii taarifa yako haionyeshi chanzo na muendelezo wa shida ya Kivu
 
Hii taarifa yako haionyeshi chanzo na muendelezo wa shida ya Kivu
Chanzo ni ukabila na uchu wa madaraka.

Hao M23 ni watusi wa Kongo. Kivu ina utajiri wa madini yanayotengeneza hizi malighafi za vifaa vya elektroniki pamoja na aina zingine za madini.

Wakongoman kwa maana ya wabantu hawataki kuwatambua watusi hawa kama wakongo toka enzi za Mobutu. Hawahesabiwi kama wananchi wa Kongo. Wanahitajika kurudi kwao Rwanda.

Ilihali watusi hawa toka miaka ya zamani kabla ya ukoloni waliishi humo Kongo. Mipaka ilivochorwa na wakoloni wakatenganishwa.

Ilipotokea mauaji ya Kimbari Rwanda 1994 wakimbizi baadhi walikimbilia Kongo na wakati wa kurudi hawa wa Kivu waliokua wakikaa humo toka enzi walitakiwa nao warudi ndo waliitwa Banyamulenge.

Matokeo yake ni vita vya silaha vilianza

Baada ya Kagame (mtusi,) kushinda walianza kuwasapoti hao watusi wa Kongo pamoja na misaada ya nje pia

Angola, Zimbabwe ya Mugabe, Uganda ya Museveni nao walimega keki kubwa sana huko Kongo na ndio walimsapoti Laurent Kabila na kusimika serikali yake.

Rwanda akiwa kinara. Na hata jeshi la Kongo lilifunzwa na Rwanda na viongozi wake wengi walikua watusi nk.

Wakati huo miaka ya 90 ilikua ni kwa ajili ya ulinzi kwani majeshi yaliyotekeleza mauaji ya Rwanda yalikimbilia Kongo wakati huo Mobutu akiwalinda. Baadae majeshi haya haya yaliingizwa kwenye mfumo wa jeshi la Kongo ikiwamo na hao watusi

Baadae ilikua ni unyonyaji wa madini. Coltan iliyochotwa huko kinyemela ni nyingi hadi sio poa.

Waliposhindwana ndio kujitenga na vita kuanza moja.

Itoshe kusema kuwa suluhi ya Kongo itapatikana na wakongoman wenyewe.

Vidonda vya mauji ya kila mara mpaka sasa watu karibu milioni 5 washafariki juu ya hivi vita. Sijajua wataviponyaje.

Ila wanabidi wakae mezani na kutatua tofauti zao. Pia kuepuka muingiliano wa nje katika suluhu hizi
 
Historia ya wakimbizi toka sehemu hiyo ni ndefu Sana hata kabla Tanzania au Congo hazijapata Uhuru. Kulikuwa na hao wakimbizi Tabora na Sumbawanga na wengine wakaolewa au kuoa na kupata watoto,vijukuu na vilembwe. Muongezeko wa hao wakimbizi au watusi, wengine ni juhudi za kimkakati za kuimega DRC na hizo maliasili. Dawa yao ni kuwahisha wasiishi hapo mpakani wapelekwe magharibi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…