Dalili za hivi sasa huko kaskazini mashariki mwa Congo DRC sio nzuri hata kidogo-wanao jifanya ni waasi wanapata wapi ujasiri wa kukalia mji/wilaya na kuendesha mambo kama Serikali iliyo uhamishoni na kibaya zaidi wanajitangaza kwamba wao wanaongoza utawala kwa ufanisi zaidi kwenye mji waliouteka kuliko Serikali ya Kinshasa - just imagine!!! Wanayasema haya kwenye nchi ya watu yenye Serikali na Rais aliye chaguliwa na raia kwa njia ya kidemokrasia na sio kwa mtutu wa bunduki.
Narudia kuwambia kwamba dalili zinaonyesha kuna kitu kinasukwa pale, si bure - wala tusishangae ikija kubainika kwamba kuna baadhi ya mataifa ya magharibi yako nyuma yao wakishirikia na baadhi ya viongozi wa Africa!!
Fugisu zote zinazo endelea kaskazini mashariki mwa Taifa la Congo, lengo lake kuu ni kutaka kujenga hoja ya kuigawa CongoDRC kwa madai kwamba Congo is too big a Country/Nation hivyo kuna umuhimu wa kuigawanya na kuwapatia uhuru kabila linalo onekana/dai linanyanyaswa na Serikali ya Kishasa - ulaghai mtupu of course madai hayo yataungwa mkono kwenye Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri Mkuu wa Uingereza BoJo pamoja na Rais J. Biden USA pamoja na baadhi ya nchi za Ulaya specifically NATO members.
Mimi sio mtume wala nabii, lakini naona this is what is coming-kitakacho nusuru Congo kugawanywa ni viongozi wa Afrika kuwa na msimamo mmoja wa kupinga kwa nguvu zao zote kuhusu hila za kuigawanya CongoDRC au Rais wa CongoDRC awaombe Urusi na China kupiga kura ya veto kupinga hila za Mataifa ya magharibi zinazo shirikiana na baadhi ya Viongozi wa Afrka wakiwa na lengo la kuigawa Congo, wahujumu hawa hawataki kuweka wazi kwamba kinacho tafutwa pale ni maliasili za Congo basi na sio uhuru wala nini sijui.