M23 yaua wanajeshi 3 wa Tanzania huko Goma DRC

Hutaki hiyo tafasiri.
Tafasiri yako ichukuliwe kwa Tahadhari-sio kwamba siitaki, nakataaje maoni yako?
Jana PK kaulizwa kama anaunga mkono M23 akajibu haoni sababu ya kutowaunga mkono.

Thats means anawaunga mkono.

Hivyo tafasiri ni kutokana na maneno ya PK.

Kama M23 ni nduguzo waambie waache kuuwa raia wa DRC. Africa tumechoka vita za Watutsi.

Tangu na tangu kila vita lazima mshiriki mnauwa maras na marais. Zama na zama

Sent from my A002SH using JamiiForums mobile app
Mkuu suala hili ni very complex na naamini unajua hilo, Fika.

Tatizo langu ni hizi lugha za Uchonganishi na Kwanini Watanzania waingizwe kwenye Vita hii. Hypothetically, Watanzania watatu wamekufa(God rest their soul) Tunaingia Kumchapa Kagame-then what? Mitafaruku ya Congo inaisha? au za Tutsi na Hutu? Sidhani.
 
Kwahiyo ni nani analipa hizi Familia za Wanajeshi wetu? SADC? DRC? au Chama cha Tishekedi?

Vijana wetu wanafia nini kwenye Foreign Wars?

Maswali ni mengi sana na Wajinga ni wengi.

Hii habari nimeiona kwenye BBC Kiswahili TV.
 
Rahisi kuandika kwa smartphone!
 
Kwahiyo ni nani analipa hizi Familia za Wanajeshi wetu? SADC? DRC? au Chama cha Tishekedi?
Nadhani inategemea hao M23 wamo kwenye makundi gani ya Mitafaruku kwa "Wenye Interest zao" huko. Mfano kama wanajulikana kama "Magaidi" na State Department au UN basi ni Wazungu. Bila ya kusahau, na biashara haramu ya Dhahabu na Madini mengine ya thamani-Wanunuzi ikiwa ni Waarabu, Wahindi, Wazungu n.k Ama?
Vijana wetu wanafia nini kwenye Foreign Wars?
Umoja ni nguvu?
Maswali ni mengi sana na Wajinga ni wengi.
Umo kwenye kundi gani?
Hii habari nimeiona kwenye BBC Kiswahili TV.
🤔
 
Kibarango kweli kibarango kama jina lako, Kwanza story zako siku zote ni za uchonganishi hususa ni kwenye Suala lolote linalohusu Rwanda na Kagame, I am sure una sababu zako binafsi na wala sio huruma uliyo nayo kwa Raia wa Congo. Kwa taarifa yako hata hao M23 ni Raia wa Congo lakini najua wewe hilo hulitaki, wanapigania nini? Baba zao na Mama zao wako kwenya kambi za wakimbizi kwa muda wa miaka 25 sasa, wengi wao wako Uganda, Rwanda na Kenya. Kwanini wako ukimbizini miaka yote hiyo, wamefukuzwa huko kwao na jeshi la serikali kwa kushirikiana na FDLR.
Statement ya Kagame jana hukumuelewa hata kidogo labda kwa uwezo wako mdogo wa kuelewa ni kitu gani amesema au ni kujishaua tu kwa sababu zako za siku zote. Amekufafanulia kwa nini hate wewe usiwaunge mkono hawa raia wa Congo waliofukuzwa kwenye ardhi ya mababu zao kwa sababu tu rugha wanayo tumia ni Kinyarwanda rejerea historia kwanini hawa watu wanapatikana kwenye hili eneo la mashariki ya Congo? Jibu lake Mwl. Nyerere alizungumzia hili, Thabo Mbeki alifafanua hili na watu wengine wengi tu.
 
Kwa Ufupi Majeshi ya SADC kwa kushirikiana na majeshi ya DRC ni kwamba wanashirikiana moja kwa moja na FDLR, hawa FDLR ndio hao waliofanya Genocide Rwanda ndio hao waliowafukuza Raia wa Congo waliojazana kwenya makambi ya wakimbizi ndani ya Uganda, Rwanda, Kenya na sehemu nyingine Duniani ambao ndio wazazi wa hawa vijana wa M23. Kwa taarifa hawa wakimbizi ndio source/supply ya vijana wanokwenda vitani. Hawana kazi nyingine kwenye makambi so ni rahisi sana kujiunga na vita, mbaya zaidi wana sababu na nia imara kabisa kwani wana nyanyasika wakati wana ardhi yao nzuri tu amayo wamyenyanganywa na kufukuzwa na Serikali yao. Kwa hiyo hata ukiwamaliza hawa m23 wote leo kesho watakuja wengine. Kwani hawa wakimbizi mpaka leo wako 500k Uganda, 150k Rwanda, 50k Kenya na zaid ya 300k sehemu mbalimbali duniani, wengine wako hata kwenye national service ya USA na Canada. So wanaopeleka majeshi kupambana na M23 wawe tayari kwani hawa vijana wako kwao and they have nothing to lose
 
Hey
 

Attachments

  • Screenshot_2024-04-08-22-58-10-452_com.facebook.katana.jpg
    577.9 KB · Views: 11
Ni uzembe wa mobutu kuwaacha banyamulenge waliokimbia vita kipindi cha habyarimana free ndio maana leo hii na wao wanajiita wacongo lkn ni kimaslahi tu huku wakijua warwanda wakimbizi kama wakimbizi wengine tu,benaco pale kuna wakimbjzi wamezaliwa pale na hadi kutaka kupata wajukuu wakiwa pale pale ila bado wanajijua si wa TZ
 
Amani haitapatikana DRC kwa makombora, wakae chini wayamalize kama ilivyofanyika Sudan Kusini, leo hii kule wanaishi kwa amani na kuiboresha nchi yao. Pande zote zilisikilizwa na kuingizwa serikalini wakawa kimoja.
DRC makombora yamepigwa kwa miaka mingi tu, na bado ni mtifuano maporini.
 
Hii vita haituhusu sisi,Congolese wameamua kuuwana wenyewe tuwaache,hivi ukiwauliza simple question why wanapigana vita sidhani kama wana jibu,rudisha wanajeshi wetu waje walinde hizi porous borders zetu,Mozambique border kuna shida na jeshi la SADC linaondoka,naona RAF wana ichukua vita hii,sisi to hold line yetu ili hii vita isienee kwetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…