Ma pro wetu wana uwezo wa kawaida kisoka

Ma pro wetu wana uwezo wa kawaida kisoka

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
34,181
Reaction score
41,563
Watanzania,

Bado tuna safari ndefu mno ya kuyafikia mafanikio ya kisoka katika timu yetu ya Taifa. Binafsi naona bado mazonge zonge mengi sana yanaikumba timu yetu. Kikubwa zaidi nachokiona ni hawa ma Pro wetu wanaocheza nje kwa kweli hawana uwezo - hawana uwezo hata wa kubadili mchezo - kifupi ni average players ambao hawapishani sana na hawa wanaocheza humu ndani, kwa hiyo kuwategemea kwamba watatupatia mafanikio ni ndoto - ni lazima tubadili mkakati na kuanza kutemea wachezaji wa ndani ambao mara nyingi wanakuwa wamezoeana.

Sitaki kuwataja kwa majina hawa ma Pro lakini nikisema mtu anitajie hata Pro mmoja ambaye jana alionekana walau kuibeba timu hakuna kabisa, wote wanahangaika tu, Uganda walionekana kucheza ki-mfumo huku sisi tukishindwa kutengeneza nafasi.

Mwalimu kashafika inabidi baada ya haya mshindano avunje timu na yeye mwenyewe apewe nafasi kuangalia ni wachezaji gani atawahitaji kutokana na mfumo anaotaka yeye. Asilazimishwe kuwaita hawa ma pro kama hajaridhika na viwango vyao.

Nahitimisha kwa kusema Ma Pro wetu wana viwango vya kawaida mno kiasi kuwategemea tunazidi kupotea, bora tuwapange wachezaji wetu wa soka na ndani ambao wengi wamekomaa kutokana na ugumu wa ligi yetu kwa sasa.

Mtu unajitahidi kuipenda timu ila haipendeki, sasa mpira kama ule hata kama tukifuzu si tutakwenda kupigwa 8 na wenye mashindao yao.
 
Hii yote inayotusumbua hapa ni siasa tu hamna kitu kingine kwani kwa CCM kila kitu ni siasa hata kuwa mwenyekiti wa TFF lazima uwe na kadi ya CCM na hiyo ndio sifa kuu na ndio maana mwenyekiti wa TFF yule Msomali aliwahi kumkejeli Tundu Lissu kipindi Magufuli alipotaka kumuua wakati Lissu mwenyewe hahusiki kabisa na soka.
 
Ukweli ni kwamba dawa pekee ya kupata timu ya taifa yenye muunganiko mzuri ni kuanza na timu za madogo halafu kwa jinsi wanavyokuwa mnawapandisha madaraja.

Nimecheki timu kama Cameroon imejaa wachezaji ambao naamini wengi wanacheza nje lakini timu haichezi mpira wa kueleweka na wamepigwa 2 na Namibia.

Mechi 2 zilizobaki tuwastaafishe kwa lazima wachezaji wote wazoefu, tuwape nafasi vijana hata kama ni wa Ihefu na Mtibwa. Ingiza Mzize, Israel Mwenda na vijana wengine kadhaa waende wakalipambanie taifa. Tukifungwa fresh tu ila tuanze upya.
 
Back
Top Bottom