fmlyimo
JF-Expert Member
- May 4, 2012
- 330
- 210
Wandugu, kuna shamba nataka ninunue (50 acres) maeneo ya Msanga, Kisarawe Mkoa wa Pwani. Hilo shamba lina udongo mweusi, lipo bondeni. Nimechukua Sample ya Udongo na Maji kutoka katika shamba hilo. Nataka nipeleke Maabara kwa ajili ya vipimo ili nijue hasa ni mazao gani naweza kulima hapo kwa umwagiliaji.
Nia yangu ni kujua hilo shamba litafaa kwa kilimo gani. Kwani nataka kulima Matikiti, Nyanya, Hoho na Vitinguu. Kama hivyo vitu havifai nataka kujua kama naweza kulima Mpunga, Mahindi au Ufuta au kupanda Mananasi au Maembe.
Pia nataka kuchimba na Bwawa la Samaki. Nimejaribu kuchunguza wenyeji nimeona wanalima ndimu, pilipili, mahindi na bilinganya.
Je, ni Maabara gani wanaweza kupima huo Udongo na Maji? na gharama zake zipo vipi? Naombeni mnielekeze. Nipo Dar. Nia yangu nijikite kwenye Kilimo cha Biashara. Sina utaalamu wa Kilimo lakini naimani nitajifunza kupitia kwa wanachama wa JF au sehemu nyingine yoyote na pia nitajifunza zaidi kwa vitendo.