Maabara ya Kupima Udongo na Maji kutoka shambani.

fmlyimo

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
330
Reaction score
210
Wandugu, kuna shamba nataka ninunue (50 acres) maeneo ya Msanga, Kisarawe Mkoa wa Pwani. Hilo shamba lina udongo mweusi, lipo bondeni. Nimechukua Sample ya Udongo na Maji kutoka katika shamba hilo. Nataka nipeleke Maabara kwa ajili ya vipimo ili nijue hasa ni mazao gani naweza kulima hapo kwa umwagiliaji.
Nia yangu ni kujua hilo shamba litafaa kwa kilimo gani. Kwani nataka kulima Matikiti, Nyanya, Hoho na Vitinguu. Kama hivyo vitu havifai nataka kujua kama naweza kulima Mpunga, Mahindi au Ufuta au kupanda Mananasi au Maembe.
Pia nataka kuchimba na Bwawa la Samaki. Nimejaribu kuchunguza wenyeji nimeona wanalima ndimu, pilipili, mahindi na bilinganya.
Je, ni Maabara gani wanaweza kupima huo Udongo na Maji? na gharama zake zipo vipi? Naombeni mnielekeze. Nipo Dar. Nia yangu nijikite kwenye Kilimo cha Biashara. Sina utaalamu wa Kilimo lakini naimani nitajifunza kupitia kwa wanachama wa JF au sehemu nyingine yoyote na pia nitajifunza zaidi kwa vitendo.
 
Umejieleza weeeeeee wakati swali lako wala halikuhitaji hayo maelezo

SUA au jamaa wa kilimo pale TAZARA watakusaidia
 
Asante ndugu yangu. Nimetoa maelezo mengi ili kupunguza maswali ambayo ningeulizwa. Nitawatafuta hao wa Tazara. Je, unaweza kukumbuka jina lao? Au hapo Tazara wapo jirani na nani?
 
Wizara ya Kilimo pale TAZARA usihangaike! Pale kama unahitaji ushauri wa zao gani na mahali gani pa kulima wakati gani unaweza kwenda. Vinginvyo ukiacha SUA nenda Mlingano Tanga
 
Wandugu, kuna shamba nataka ninunue (50 acres) maeneo ya Msanga, Kisarawe Mkoa wa Pwani. Hilo shamba lina udongo mweusi, lipo bondeni. Nimechukua Sample ya Udongo na Maji kutoka katika shamba hilo. Nataka nipeleke Maabara kwa ajili ya vipimo ili nijue hasa ni mazao gani naweza kulima hapo kwa umwagiliaji.
Nia yangu ni kujua hilo shamba litafaa kwa kilimo gani. Kwani nataka kulima Matikiti, Nyanya, Hoho na Vitinguu. Kama hivyo vitu havifai nataka kujua kama naweza kulima Mpunga, Mahindi au Ufuta au kupanda Mananasi au Maembe.
Pia nataka kuchimba na Bwawa la Samaki. Nimejaribu kuchunguza wenyeji nimeona wanalima ndimu, pilipili, mahindi na bilinganya.
Je, ni Maabara gani wanaweza kupima huo Udongo na Maji? na gharama zake zipo vipi? Naombeni mnielekeze. Nipo Dar. Nia yangu nijikite kwenye Kilimo cha Biashara. Sina utaalamu wa Kilimo lakini naimani nitajifunza kupitia kwa wanachama wa JF au sehemu nyingine yoyote na pia nitajifunza zaidi kwa vitendo.

Mkuu unaelewa jinsi ya kuchukua sample shambani lakini? Kuna mbinu zake ili upate udongo unaobeba picha halisi ya shamba, vinginevyo utaulizwa jinsi ulivyochukua sample hiyo na kama ulichimba kienyeji tu watakuelekeza urudi ukachukue sample inavyotakiwa, nauli na usumbufu kibao! Elezea hapa jinsi ulivyochukua udongo wako wadau wakukosoe au la kama uko fiti poa! Kwa uliepo Dar kimbilio lako la Karibu ni SUA au la ukiona wanajivuta sana kwingine ni Mlingano Tanga kama alivyokushauri mdau hapo juu! Bei zake kubwa lakini inalipa sana kupima udongo na watakupa ushauri wa uhakika juu ya mazao yatakayofaa kwa aina ya udongo wako!
 
Wizara ya Kilimo pale TAZARA usihangaike! Pale kama unahitaji ushauri wa zao gani na mahali gani pa kulima wakati gani unaweza kwenda. Vinginvyo ukiacha SUA nenda Mlingano Tanga

Asante sana ndugu. Naouna ushauri bado unamiminika. Nitajitahidi kwenda SUA.
 
Mkuu unaelewa jinsi ya kuchukua sample shambani lakini? Kuna mbinu zake ili upate udongo unaobeba picha halisi ya shamba, vinginevyo utaulizwa jinsi ulivyochukua sample hiyo na kama ulichimba kienyeji tu watakuelekeza urudi ukachukue sample inavyotakiwa, nauli na usumbufu kibao! Elezea hapa jinsi ulivyochukua udongo wako wadau wakukosoe au la kama uko fiti poa! Kwa uliepo Dar kimbilio lako la Karibu ni SUA au la ukiona wanajivuta sana kwingine ni Mlingano Tanga kama alivyokushauri mdau hapo juu! Bei zake kubwa lakini inalipa sana kupima udongo na watakupa ushauri wa uhakika juu ya mazao yatakayofaa kwa aina ya udongo wako!

Aisee, nahisi kuwa nilichukua kienyeji. Nilichofanya ni kuchimba kwa panga sehemu kama tatu tofauti. Ya kwanza nilichukua udongo wa juu, ya pili nilichukua udongo wa chini kidogo na ya tatu nilichukua udongo wa chini zaidi. Pia nilichota udongo pembeni ya kisima cha kienyeji kilicho karibu na shamba na kuchota maji kwenye chupa.
Ndugu Kubota, ili kuepuka usumbufu wa nenda rudi, naomba unielekezi jinsi ya kuchukua hizo sample kiutaalamu zaidi na ni kiasi gani hasa kinatakiwa huko maabara. Nimeshaamua kwenda SUA. Pia kama unajua gharama zake na huwa inachukua muda gani naomba uniambie ili nijipange kikamilifu. Asanteni sana.
 
Nilishawahi kwenda SUA kwa ajili hiyo majibu waliyonipa hadi nilikata tamaa ushirikiano wao ni mdogo sana
 
Nenda intertec wapo kurasini kalibia na uhamiaji naaikia haizidi elfu20 kwa sample, udongo chimba pembeni nne na katikati ya shamba changanya huo udongo chukua huo mchanganyiko kama 2kg peleka maabala.
 
Back
Top Bottom