Maadhimisho ya miaka 100 ya Shule ya Sekondari ya Old Moshi. Tukutane Wahandisi tuliosoma hapo

goroko77

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2019
Posts
8,845
Reaction score
13,072
MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA SHULE YA SEKONDARI OLD MOSHI(1922 - 2022).

- Shule ya Sekondari Old Moshi inaenda kutimiza miaka 100 mwezi Oktoba, 2022, tangu kuanzishwa kwake Oktoba, 1922. Shule hii kongwe ya Old Moshi ilianzishwa na serikali ya Waingereza mwaka 1922 ikiwa ni shule ya kwanza ya serikali ya sekondari katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

- Shule ya Sekondari Old Moshi ilianzishwa katika kijiji cha Tsudunyi katika eneo la himaya ya Umangi, Old Moshi na serikali ya Waingereza katika eneo ambalo ndio ulikuwa mji wa Moshi wa zamani. Shule hii ilianza na kutumia baadhi ya majengo yaliyokuwa ya utawala wa serikali ya Wajerumani Kaskazini ya Tanganyika.

- Shule ya Sekondari Old Moshi kutokana na ukongwe wake ni shule ambayo ilisomwa na watu wengi mashuhuri wa zamani ambao walikuja kushika nafasi kubwa za uongozi ndani ya serikali ya wachagga na Tanganyika kwa ujumla. Old Moshi Sekondari ni shule ambayo hata Mangi Petro Itosi Marealle aliyekuja kuwa Mangi wa himaya ya umangi Marangu na baadaye Mangi Mwitori wa jimbo la Vunjo, Uchagga alisoma akiwa Sekondari na baadaye kuja kushika nyadhifa mbalimbali.

- Hata Gavana wa kwanza wa benki kuu ya Tanzania (BOT) Mr. Edwin Mtei ambaye pia ni mwanzilishi na Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameeleza katika kitabu chake cha "From Goatherd To Governor" kwamba alisoma shule hii ya Sekondari Old Moshi wakati ikiwa Tsudunyi. Gavana Mtei aliyewahi pia kuwa waziri wa fedha, katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika mashariki na baadaye kufanya kazi IMF ameeleza kwamba akiwa mwanafunzi Old Moshi, Sekondari alisoma pamoja na waziri mkuu mstaafu Cleopa Msuya, Wilfred Marealle na Mhandisi Mihimili wa mwanzoni Tanganyika Eng. Ainamensa Mbuya.

- Dr. Reginald Mengi pia kwenye kitabu chake cha "I can, I must, I will" ameeleza kwamba shule ya Sekondari alisoma Old Moshi. Hata hivyo ni katika kipindi ambacho Dr. Reginald Mengi alipokuwa anasoma shule ya Sekondari Old Moshi miaka ya mwishoni ya 1950's ndipo shule hii ya mwanzo kabisa Kilimanjaro ilihamishwa kutokea katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi na kuhamishiwa Moshi mjini katika eneo ilipo sasa, karibu na Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.

- Watu wengine wengi sana mbalimbali na wengine ni watu mashuhuri sana wa miaka ya zamani kidogo walisoma katika shule hii.

- Mwaka 1922 shule ya Sekondari Old Moshi ilianzishwa kama shule ya ufundi na mwaka 1927 ndipo ilianza rasmi kufundisha masomo ya sekondari (Ordinary Level Secondary School - O Level). Mwaka 1960 ndipo shule hii ilianza kufundisha masomo ya ngazi ya juu ya Sekondari (Advanced Level Secondary School - A Level) ikiwa ndio shule ya kwanza ya jimbo la Kaskazini lililokuwa linaitwa Northern Province. Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia mwaka 1960 ilianza kutoa masomo ya juu ya Sekondari katika michepuo ya Physics, Chemistry na Mathematics(PCM) na Physics Chemistry na Mathematics(PCB). Hata hivyo tangu mwaka 2009 shule hii iliongeza mchepuo wa sanaa wa History, Geography na Language (HGL).

- Mpaka sasa shule ya Sekondari Old Moshi ina wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato sita ikiwa na jumla ya wanafunzi 717 ambapo kati ya wanafunzi 268 ni wa kidato cha kwanza mpaka cha sita na wanafunzi 449 ni wa kidato cha tano na sita.

- Wakati shule ya Sekondari Old Moshi inakwenda kutimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake na serikali ya Waingereza, ikiwa imeandaa sherehe za maadhimisho hayo siku ya tarehe 20/Oktoba/2022 tunaomba mchango wako wa mawazo juu ya;

1. Unafahamu nini kuhusu shule ya Sekondari Old Moshi?

2. Je, wewe umesoma shule ya Sekondari Old Moshi? Umesoma mwaka gani?

3. Una ndugu jamaa au rafiki aliyesoma shule ya Sekondari Old Moshi?, Alisoma mwaka gani?

4. Mtu gani mwingine maarufu unayemfahamu alisoma shule ya Sekondari Old Moshi?

5. Una maoni au Ushauri au Mapendekezo gani juu ya shule ya Sekondari Old Moshi ilipofika mpaka sasa inapotimiza miaka 100?

Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kuwasiliana na Ms. Leyla Shangali, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Ya Maadhimisho ya Miaka 100 Ya Shule Ya Sekondari Old Moshi.

Karibu kwa Mchango wa Mawazo.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Nikikutana na Reginald Mengi siku moja akanisalimu,"Habari za siku nyingi.?" Nikabakia kushangaa, kwani tumeonana lini, mpaka nilipofahamu kuwa alisoma Old Moshi kama mimi.

Dr(au Prof?) Massawe, by the way, amesoma Old Moshi. Yule aliyekuwa daktari bingwa wa watoto. Massawe, tulikuwa dormitory moja. He was sleeping on the bed right next to mine.
 
Nikikutana na Reginald Mengi siku moja akanisalimu,"Habari za siku nyingi.?" Nikabakia kushangaa,kwani tumeonana lini,mpaka nilipofahamu kuwa alisoma Old Moshi kama mimi .
Dr(au Prof?) Massawe,by the way,amesoma Old Moshi. Yule aliyekuwa daktari bingwa wa watoto. Massawe,tulikuwa dormitory moja. He was sleeping on the bed right next to mine.
Shikamooo
 
MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA SHULE YA SEKONDARI OLD MOSHI(1922 - 2022).

- Shule ya Sekondari Old Moshi inaenda kutimiza miaka 100 mwezi Oktoba, 2022, tangu kuanzishwa kwake Oktoba, 1922. Shule hii kongwe ya Old Moshi ilianzishwa na serikali ya Waingereza mwaka 1922 ikiwa ni shule ya kwanza ya serikali ya sekondari katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

- Shule ya Sekondari Old Moshi ilianzishwa katika kijiji cha Tsudunyi katika eneo la himaya ya Umangi, Old Moshi na serikali ya Waingereza katika eneo ambalo ndio ulikuwa mji wa Moshi wa zamani. Shule hii ilianza na kutumia baadhi ya majengo yaliyokuwa ya utawala wa serikali ya Wajerumani Kaskazini ya Tanganyika.

- Shule ya Sekondari Old Moshi kutokana na ukongwe wake ni shule ambayo ilisomwa na watu wengi mashuhuri wa zamani ambao walikuja kushika nafasi kubwa za uongozi ndani ya serikali ya wachagga na Tanganyika kwa ujumla. Old Moshi Sekondari ni shule ambayo hata Mangi Petro Itosi Marealle aliyekuja kuwa Mangi wa himaya ya umangi Marangu na baadaye Mangi Mwitori wa jimbo la Vunjo, Uchagga alisoma akiwa Sekondari na baadaye kuja kushika nyadhifa mbalimbali.

- Hata Gavana wa kwanza wa benki kuu ya Tanzania (BOT) Mr. Edwin Mtei ambaye pia ni mwanzilishi na Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameeleza katika kitabu chake cha "From Goatherd To Governor" kwamba alisoma shule hii ya Sekondari Old Moshi wakati ikiwa Tsudunyi. Gavana Mtei aliyewahi pia kuwa waziri wa fedha, katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika mashariki na baadaye kufanya kazi IMF ameeleza kwamba akiwa mwanafunzi Old Moshi, Sekondari alisoma pamoja na waziri mkuu mstaafu Cleopa Msuya, Wilfred Marealle na Mhandisi Mihimili wa mwanzoni Tanganyika Eng. Ainamensa Mbuya.

- Dr. Reginald Mengi pia kwenye kitabu chake cha "I can, I must, I will" ameeleza kwamba shule ya Sekondari alisoma Old Moshi. Hata hivyo ni katika kipindi ambacho Dr. Reginald Mengi alipokuwa anasoma shule ya Sekondari Old Moshi miaka ya mwishoni ya 1950's ndipo shule hii ya mwanzo kabisa Kilimanjaro ilihamishwa kutokea katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi na kuhamishiwa Moshi mjini katika eneo ilipo sasa, karibu na Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.

- Watu wengine wengi sana mbalimbali na wengine ni watu mashuhuri sana wa miaka ya zamani kidogo walisoma katika shule hii.

- Mwaka 1922 shule ya Sekondari Old Moshi ilianzishwa kama shule ya ufundi na mwaka 1927 ndipo ilianza rasmi kufundisha masomo ya sekondari (Ordinary Level Secondary School - O Level). Mwaka 1960 ndipo shule hii ilianza kufundisha masomo ya ngazi ya juu ya Sekondari (Advanced Level Secondary School - A Level) ikiwa ndio shule ya kwanza ya jimbo la Kaskazini lililokuwa linaitwa Northern Province. Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia mwaka 1960 ilianza kutoa masomo ya juu ya Sekondari katika michepuo ya Physics, Chemistry na Mathematics(PCM) na Physics Chemistry na Mathematics(PCB). Hata hivyo tangu mwaka 2009 shule hii iliongeza mchepuo wa sanaa wa History, Geography na Language (HGL).

- Mpaka sasa shule ya Sekondari Old Moshi ina wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato sita ikiwa na jumla ya wanafunzi 717 ambapo kati ya wanafunzi 268 ni wa kidato cha kwanza mpaka cha sita na wanafunzi 449 ni wa kidato cha tano na sita.

- Wakati shule ya Sekondari Old Moshi inakwenda kutimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake na serikali ya Waingereza, ikiwa imeandaa sherehe za maadhimisho hayo siku ya tarehe 20/Oktoba/2022 tunaomba mchango wako wa mawazo juu ya;

1. Unafahamu nini kuhusu shule ya Sekondari Old Moshi?
2. Je, wewe umesoma shule ya Sekondari Old Moshi? Umesoma mwaka gani?
3. Una ndugu jamaa au rafiki aliyesoma shule ya Sekondari Old Moshi?, Alisoma mwaka gani?
4. Mtu gani mwingine maarufu unayemfahamu alisoma shule ya Sekondari Old Moshi?
5. Una maoni au Ushauri au Mapendekezo gani juu ya shule ya Sekondari Old Moshi ilipofika mpaka sasa inapotimiza miaka 100?

Nakuja
 
Sikuwahi kujua shule ya old Moshi ni kale namna hiyo!

Hata hivyo jamii ya Wachagga wa old Moshi ndio wa zamani kabisa karibu kuliko wachaga wote.

Pamoja na uwepo wa shule tokea mapema lakini naona hakukutoka wasomi wengi old Moshi kama mahali pengine kulie Kilimanjaro.

Pongezi nyingi sana kwa kutimiza miaka 100 ya utoaji wa elimu japo ni miaka mia sasa ya utoaji elimu ila nchi yetu bado ipo chini sana katika fikra kiasi cha kwamba ni kama hakuna elimu ya maana au ya ukombozi inayotolewa.
 
2001-2003 PCM
Shengena karibu na Kwa Mr. Kinunda

Lakini Prof. Philemon Sarungi si alisoma hapo pia? Yule bingwa wa mifupa.

Mwalimu wangu Bora kabisa wa Physics PDD (Mr. Msami) Mungu awabariki waalimu na wahudumu wote wa hiyo shule ila ampendelee zaidi PDD.
 
Back
Top Bottom