Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwahyo Hali unayoiyona sashv Ni sawa na ya mwaka 1950 mkuuSikuwahi kujua shule ya old Moshi ni kale namna hiyo!
Hata hivyo jamii ya Wachagga wa old Moshi ndio wa zamani kabisa karibu kuliko wachaga wote.
Pamoja na uwepo wa shule tokea mapema lakini naona hakukutoka wasomi wengi old Moshi kama mahali pengine kulie Kilimanjaro.
Pongezi nyingi sana kwa kutimiza miaka 100 ya utoaji wa elimu japo ni miaka mia sasa ya utoaji elimu ila nchi yetu bado ipo chini sana katika fikra kiasi cha kwamba ni kama hakuna elimu ya maana au ya ukombozi inayotolewa.
Sikuwepo mwaka wa 50,60,70 na 80 lakini kwa marejeo mbali mbali huko awali kabla ya hapa kulikuwa na heri kuliko tulipo leo ndugu yangu.Kwahyo Hali unayoiyona sashv Ni sawa na ya mwaka 1950 mkuu
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Hata Mimi nimelala shengena one karibu na laboratory ya biology kutokea getinMy school......
Shengena one ndio bweni langu...tumekula sana pilau kwa kuongoza usafi kila mara
Kumbe kinunda wa zamani hivo...katupigia mathematics 2008-2010 pcm2001-2003
Shengena karibu na Kwa Mr. Kinunda
Lakini Prof. Philemon Sarungi si alisoma hapo pia? Yule bingwa wa mifupa.
Mwalimu wangu Bora kabisa wa Physics PDD (Mr. Msami) Mungu awabariki waalimu na wahudumu wote wa hiyo shule ila ampendelee zaidi PDD.
My young brother pia amepiga Advance pale, amegraduate pale 2005,now yuko Shanghai na Ph'D ya pharmacy anagonga mishe zake, nimemtembelea sana pale miaka hio na kitu ambacho nilikua nacheka kila nikifika pale ni maandish ya ukuta wa getini yaloandikwa OLD MOSHI SECONDARY, ila madogo kwa ununda wao wakaongeza herufi G pale mwanzoni ikawa inasomeka GOLD MOSHI SECONDARY😂😂😂nitamrushia link ili akipenda aje humu achangie chochote.
Nikikutana na Reginald Mengi siku moja akanisalimu,"Habari za siku nyingi.?" Nikabakia kushangaa,kwani tumeonana lini,mpaka nilipofahamu kuwa alisoma Old Moshi kama mimi .
Dr(au Prof?) Massawe,by the way,amesoma Old Moshi. Yule aliyekuwa daktari bingwa wa watoto. Massawe,tulikuwa dormitory moja. He was sleeping on the bed right next to mine.
Wanafunzi wao siku hizi wanabeba mabegi yao na kwenda kusomea chuo cha ushirika ili waonekane ni wanachuo au kung'oa pisi za chuo...wameendekeza uasherati zaid ya masomo
Inachukua wanafunz wenye uhitaj maalumu ila miundombinu wezeshi kwa watoto hao haikidhi mahitaji yao....na hili wakaliangalie
Hawa huwa Mungu anawapa cha ziada na wanakuwa na uwezo mkubwa sanaa...mm nna rafik yangu huwa kaka yake haoni...ila akichukua computer hata mimi nnaeona kwa macho mawili simfikii hata robo...anaendesha ma NGO'S ya nje huko kupitia online....Kuna jamaa ilikua ukiingia tu Kwa sauti za nyayo zako, anakuita jina lako, au ukimshika Mkono anajua Hutu ni flani. Kuna wakati napiga nae stori machozi yananilengalenga, nawaza ambavyo huyu jamaa haoni mnaenda nae kanisani, anasikia tu lakini hajawahi kuona vitu vinafananaje. Mungu amewajalia wale jamaa kwenye utambuzi
Nimekumbuka Bangaluu la KIBO 5MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA SHULE YA SEKONDARI OLD MOSHI(1922 - 2022).
- Shule ya Sekondari Old Moshi inaenda kutimiza miaka 100 mwezi Oktoba, 2022, tangu kuanzishwa kwake Oktoba, 1922. Shule hii kongwe ya Old Moshi ilianzishwa na serikali ya Waingereza mwaka 1922 ikiwa ni shule ya kwanza ya serikali ya sekondari katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
- Shule ya Sekondari Old Moshi ilianzishwa katika kijiji cha Tsudunyi katika eneo la himaya ya Umangi, Old Moshi na serikali ya Waingereza katika eneo ambalo ndio ulikuwa mji wa Moshi wa zamani. Shule hii ilianza na kutumia baadhi ya majengo yaliyokuwa ya utawala wa serikali ya Wajerumani Kaskazini ya Tanganyika.
- Shule ya Sekondari Old Moshi kutokana na ukongwe wake ni shule ambayo ilisomwa na watu wengi mashuhuri wa zamani ambao walikuja kushika nafasi kubwa za uongozi ndani ya serikali ya wachagga na Tanganyika kwa ujumla. Old Moshi Sekondari ni shule ambayo hata Mangi Petro Itosi Marealle aliyekuja kuwa Mangi wa himaya ya umangi Marangu na baadaye Mangi Mwitori wa jimbo la Vunjo, Uchagga alisoma akiwa Sekondari na baadaye kuja kushika nyadhifa mbalimbali.
- Hata Gavana wa kwanza wa benki kuu ya Tanzania (BOT) Mr. Edwin Mtei ambaye pia ni mwanzilishi na Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameeleza katika kitabu chake cha "From Goatherd To Governor" kwamba alisoma shule hii ya Sekondari Old Moshi wakati ikiwa Tsudunyi. Gavana Mtei aliyewahi pia kuwa waziri wa fedha, katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika mashariki na baadaye kufanya kazi IMF ameeleza kwamba akiwa mwanafunzi Old Moshi, Sekondari alisoma pamoja na waziri mkuu mstaafu Cleopa Msuya, Wilfred Marealle na Mhandisi Mihimili wa mwanzoni Tanganyika Eng. Ainamensa Mbuya.
- Dr. Reginald Mengi pia kwenye kitabu chake cha "I can, I must, I will" ameeleza kwamba shule ya Sekondari alisoma Old Moshi. Hata hivyo ni katika kipindi ambacho Dr. Reginald Mengi alipokuwa anasoma shule ya Sekondari Old Moshi miaka ya mwishoni ya 1950's ndipo shule hii ya mwanzo kabisa Kilimanjaro ilihamishwa kutokea katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi na kuhamishiwa Moshi mjini katika eneo ilipo sasa, karibu na Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
- Watu wengine wengi sana mbalimbali na wengine ni watu mashuhuri sana wa miaka ya zamani kidogo walisoma katika shule hii.
- Mwaka 1922 shule ya Sekondari Old Moshi ilianzishwa kama shule ya ufundi na mwaka 1927 ndipo ilianza rasmi kufundisha masomo ya sekondari (Ordinary Level Secondary School - O Level). Mwaka 1960 ndipo shule hii ilianza kufundisha masomo ya ngazi ya juu ya Sekondari (Advanced Level Secondary School - A Level) ikiwa ndio shule ya kwanza ya jimbo la Kaskazini lililokuwa linaitwa Northern Province. Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia mwaka 1960 ilianza kutoa masomo ya juu ya Sekondari katika michepuo ya Physics, Chemistry na Mathematics(PCM) na Physics Chemistry na Mathematics(PCB). Hata hivyo tangu mwaka 2009 shule hii iliongeza mchepuo wa sanaa wa History, Geography na Language (HGL).
- Mpaka sasa shule ya Sekondari Old Moshi ina wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato sita ikiwa na jumla ya wanafunzi 717 ambapo kati ya wanafunzi 268 ni wa kidato cha kwanza mpaka cha sita na wanafunzi 449 ni wa kidato cha tano na sita.
- Wakati shule ya Sekondari Old Moshi inakwenda kutimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake na serikali ya Waingereza, ikiwa imeandaa sherehe za maadhimisho hayo siku ya tarehe 20/Oktoba/2022 tunaomba mchango wako wa mawazo juu ya;
1. Unafahamu nini kuhusu shule ya Sekondari Old Moshi?
2. Je, wewe umesoma shule ya Sekondari Old Moshi? Umesoma mwaka gani?
3. Una ndugu jamaa au rafiki aliyesoma shule ya Sekondari Old Moshi?, Alisoma mwaka gani?
4. Mtu gani mwingine maarufu unayemfahamu alisoma shule ya Sekondari Old Moshi?
5. Una maoni au Ushauri au Mapendekezo gani juu ya shule ya Sekondari Old Moshi ilipofika mpaka sasa inapotimiza miaka 100?
Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kuwasiliana na Ms. Leyla Shangali, Mwenyekiti wa Kamati Ya Maandalizi Ya Maadhimisho Ya Miaka 100 Ya Shule Ya Sekondari Old Moshi.
Karibu kwa Mchango wa Mawazo.
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Sawa Mainjinia mmesaidia vp kuboresha mfumo wa elimu??MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA SHULE YA SEKONDARI OLD MOSHI(1922 - 2022).

Yule mama wa Chemistry sijawahi kujua jina lake halisi zaidi ya "Madam Quantum"😀😀Nimesoma hapo nikalala Mawenzi 10.
Namkumbuka Mr Msami (PDidy) mkali sana wa Physics...mpole sana na anajua. Sijui yuko wapi.
Alikuwepo babu mmoja mkali wa Pure Maths, mama mmoja mkali wa Chemistry.
Mwl mmoja akiitwa Lisapita.
Old Moshi My School