Augustine Genius
JF-Expert Member
- Apr 14, 2016
- 1,216
- 1,486
Hata ROMA MZIMBABWE alipita OLD MOSHI
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo ni babu yakoShikamoo Baba
Sio Baharia Iddy kweli huyu? Anyway Mawenzi 10 karibu na Kibo 11 ndio lilikuwa bweni languKuna jamaa ilikua ukiingia tu Kwa sauti za nyayo zako, anakuita jina lako, au ukimshika Mkono anajua Hutu ni flani. Kuna wakati napiga nae stori machozi yananilengalenga, nawaza ambavyo huyu jamaa haoni mnaenda nae kanisani, anasikia tu lakini hajawahi kuona vitu vinafananaje. Mungu amewajalia wale jamaa kwenye utambuzi
Mama Recho na chapati zake na mandazi, Halafu kuna mama Deborah naye alikuwa mke wa jamaa wa Gs Mzee Maganga.... Dah Good old daysMama Semiono, Kinunda, Kimaro mbao, ToD, Mama recho du kitambo sana
Tufahamiane kwa majina yetu halisi au hizihizi USER ID za JamiiForums?MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA SHULE YA SEKONDARI OLD MOSHI(1922 - 2022).
- Shule ya Sekondari Old Moshi inaenda kutimiza miaka 100 mwezi Oktoba, 2022, tangu kuanzishwa kwake Oktoba, 1922. Shule hii kongwe ya Old Moshi ilianzishwa na serikali ya Waingereza mwaka 1922 ikiwa ni shule ya kwanza ya serikali ya sekondari katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
- Shule ya Sekondari Old Moshi ilianzishwa katika kijiji cha Tsudunyi katika eneo la himaya ya Umangi, Old Moshi na serikali ya Waingereza katika eneo ambalo ndio ulikuwa mji wa Moshi wa zamani. Shule hii ilianza na kutumia baadhi ya majengo yaliyokuwa ya utawala wa serikali ya Wajerumani Kaskazini ya Tanganyika.
- Shule ya Sekondari Old Moshi kutokana na ukongwe wake ni shule ambayo ilisomwa na watu wengi mashuhuri wa zamani ambao walikuja kushika nafasi kubwa za uongozi ndani ya serikali ya wachagga na Tanganyika kwa ujumla. Old Moshi Sekondari ni shule ambayo hata Mangi Petro Itosi Marealle aliyekuja kuwa Mangi wa himaya ya umangi Marangu na baadaye Mangi Mwitori wa jimbo la Vunjo, Uchagga alisoma akiwa Sekondari na baadaye kuja kushika nyadhifa mbalimbali.
- Hata Gavana wa kwanza wa benki kuu ya Tanzania (BOT) Mr. Edwin Mtei ambaye pia ni mwanzilishi na Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameeleza katika kitabu chake cha "From Goatherd To Governor" kwamba alisoma shule hii ya Sekondari Old Moshi wakati ikiwa Tsudunyi. Gavana Mtei aliyewahi pia kuwa waziri wa fedha, katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika mashariki na baadaye kufanya kazi IMF ameeleza kwamba akiwa mwanafunzi Old Moshi, Sekondari alisoma pamoja na waziri mkuu mstaafu Cleopa Msuya, Wilfred Marealle na Mhandisi Mihimili wa mwanzoni Tanganyika Eng. Ainamensa Mbuya.
- Dr. Reginald Mengi pia kwenye kitabu chake cha "I can, I must, I will" ameeleza kwamba shule ya Sekondari alisoma Old Moshi. Hata hivyo ni katika kipindi ambacho Dr. Reginald Mengi alipokuwa anasoma shule ya Sekondari Old Moshi miaka ya mwishoni ya 1950's ndipo shule hii ya mwanzo kabisa Kilimanjaro ilihamishwa kutokea katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi na kuhamishiwa Moshi mjini katika eneo ilipo sasa, karibu na Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
- Watu wengine wengi sana mbalimbali na wengine ni watu mashuhuri sana wa miaka ya zamani kidogo walisoma katika shule hii.
- Mwaka 1922 shule ya Sekondari Old Moshi ilianzishwa kama shule ya ufundi na mwaka 1927 ndipo ilianza rasmi kufundisha masomo ya sekondari (Ordinary Level Secondary School - O Level). Mwaka 1960 ndipo shule hii ilianza kufundisha masomo ya ngazi ya juu ya Sekondari (Advanced Level Secondary School - A Level) ikiwa ndio shule ya kwanza ya jimbo la Kaskazini lililokuwa linaitwa Northern Province. Shule ya Sekondari Old Moshi kuanzia mwaka 1960 ilianza kutoa masomo ya juu ya Sekondari katika michepuo ya Physics, Chemistry na Mathematics(PCM) na Physics Chemistry na Mathematics(PCB). Hata hivyo tangu mwaka 2009 shule hii iliongeza mchepuo wa sanaa wa History, Geography na Language (HGL).
- Mpaka sasa shule ya Sekondari Old Moshi ina wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato sita ikiwa na jumla ya wanafunzi 717 ambapo kati ya wanafunzi 268 ni wa kidato cha kwanza mpaka cha sita na wanafunzi 449 ni wa kidato cha tano na sita.
- Wakati shule ya Sekondari Old Moshi inakwenda kutimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake na serikali ya Waingereza, ikiwa imeandaa sherehe za maadhimisho hayo siku ya tarehe 20/Oktoba/2022 tunaomba mchango wako wa mawazo juu ya;
1. Unafahamu nini kuhusu shule ya Sekondari Old Moshi?
2. Je, wewe umesoma shule ya Sekondari Old Moshi? Umesoma mwaka gani?
3. Una ndugu jamaa au rafiki aliyesoma shule ya Sekondari Old Moshi?, Alisoma mwaka gani?
4. Mtu gani mwingine maarufu unayemfahamu alisoma shule ya Sekondari Old Moshi?
5. Una maoni au Ushauri au Mapendekezo gani juu ya shule ya Sekondari Old Moshi ilipofika mpaka sasa inapotimiza miaka 100?
Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kuwasiliana na Ms. Leyla Shangali, Mwenyekiti wa Kamati Ya Maandalizi Ya Maadhimisho Ya Miaka 100 Ya Shule Ya Sekondari Old Moshi.
Karibu kwa Mchango wa Mawazo.
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Bila shaka itakua ni cube ya kwanza mkono wa kushoto ukiwa unatokea MAWENZI 10Old school tumepiga sana hapo na kina Contour, Chura, Billo boy, Macgun, Shofu, kipindi hicho tunacheza mechi na polisi wa hapo ccp na kuwachapa magoli na virungu juu tulikuwa watukutu kweli mabweni yote kuanzia Shengena,Meru, Hanang, Kibo na Mawenzi tunalala ilikuwa full shangwe. By then niliishi Kibo 5 na kwenye bed langu juu kulikiwa na tobo la kuingia darini incase ya soo nazama na kuchemsha maji kwa direct heater misumari ila tulikuwa mapopo balaa tukatoboa Bro wangu nae tulikuwa nae now Dr. Somewhere Dar, mimi naendelea kupambana na hali yangu sehemu fulani sikuwa mjinga na nilipata ka BA. kanani push kwenye maisha kitaa
Bweni langu hili.. Sijui ulikuwa mwaka gani maana intake yetu kilitokea kisa cha jamaa yetu mmoja alikuwa na miadi na demu wake kutoka shule ya wasichana ya Ashira kama sikosei(ambao siku 2 zilizopita walikuja shuleni kwetu kwenye disco na jamaa akaopoa. Sasa kwa vile kipindi kile disco [emoji1739] likiisha wasichana wanaitwa rokoo mmoja mmoja kuingia kwenye Bus kurudi shuleni kwao, ilikuwa ukiopoa mnapanga siku demu anakuja mjini ndiyo mnakutana kubanduana) hivyo siku ya ahadi jamaa akaenda mjini pale stend ya ma Bus kuna wasambaa walikuwa wanauza Viagra ya kienyeji iliyokuwa inaitwa MKUYATI ambayo ilikuwa ni balaa. Jamaa skainunua, akaenda pale Shangazi Hotel akanunua chai ya rangi na kuweka ile dawa (ni ya unga) na kunywa. Kwa bahati mbaya demu siku hiyo hakuja alinyimwa ruhusa shuleni, bwanaaa weweee jamaa yetu wa Shengena aliteseka maana ile erection ya mashine ilikuwa siyo ya kitoto, kuanzia asubuhi mpaka jioni mashine iko wima tuu. Akapewa kila aina ya ushauri mpaka kupiga nyeto, akapiga 2 rounds but baada ya muda kidogo ngoma imesimama daaah.. [emoji23] [emoji23]My school......
Shengena one ndio bweni langu...tumekula sana pilau kwa kuongoza usafi kila mara
Sahihi..Nasikia alitaga
Enzi zetu Physics tulifundishwa na walimu kutoka Urusi. Yaani yule mwalimu alikuwa ni full engineer na alifufua mpaka Lori la shule, na baadae tukaletewa mtambo wa sinema kutoka Urusi, na sinema maarufu iliitwa KUKARACHA.. [emoji23] [emoji23]2001-2003 PCM
Shengena karibu na Kwa Mr. Kinunda
Lakini Prof. Philemon Sarungi si alisoma hapo pia? Yule bingwa wa mifupa.
Mwalimu wangu Bora kabisa wa Physics PDD (Mr. Msami) Mungu awabariki waalimu na wahudumu wote wa hiyo shule ila ampendelee zaidi PDD.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Umenikumbusha NDAMA... Nilikuwa na ndama wangu msambaa tulielewana sanaa mpaka nikamuachia godoro na blanket nilipomaliza..Kuna wakati ukienda Muhimbili wote wametoka Old Moshi (PCB) na COET ni kutoka Old Moshi (PCM). Kilichokuwa kinasaidia ni KUBUNDI na ndama kumletea Uji na chakula ng'ombe! Hiyo ni miaka ya 1973! Moshi Sec we acha tu
Mama Tara pia alikuwepoMama Recho na chapati zake na mandazi, Halafu kuna mama Deborah naye alikuwa mke wa jamaa wa Gs Mzee Maganga.... Dah Good old days
Wewe jamaa una ramli balaaaaa mpaka nimeogopa du!! Ulitoka mwaka gani pale Old tuanzie hapo maana umepatia 💯✓Bila shaka itakua ni cube ya kwanza mkono wa kushoto ukiwa unatokea MAWENZI 10
Shule ilishakarabatiwa mwaka janaKwenye majadiliano hayo zungumzia suala la ukarabati maana shule imechoka miundombinu hasa kipindi cha mvua na matope. Nimesoma jirani ila Old Moshi nimeenda sana
Hz hz mkuu za hapahapaTufahamiane kwa majina yetu halisi au hizihizi USER ID za JamiiForums?