skilled masala
Senior Member
- May 2, 2019
- 118
- 160
Masala sayi
08, August 2021
Chuo Kikuu cha Iringa.
Kila ifikapo tarehe 08, August ya kila mwaka Tanzania huadhimisha sikukuu ya wakulima ambapo lengo kuu la sikukuu hiyo ni kuangalia mafanikio ya wakulima, wafugaji na wavuvi kwa mwaka husika, hivyo serikali kupitia wizara ya kilimo huandaa maonesho ya bidhaa za kilimo na ufugaji kwa ngazi ya kanda na taifa, kwa mwaka huu serikali ilitangaza kufuta Maonesho ya nane nane na badala yake pesa zilizokuwa zimepangwa zielekezwe kwenye mafunzo ya Ugani.
Kabla ya mwaka 1993 sikukuu ya wakulima iliadhimishwa kila tarehe 07, Julai ya kila mwaka ikiwa kama wito wa kisiasa wa enzi hizo wa “siasa ni kilimo” mwaka 1992 Tanzania ilipohamia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa sikukuu hiyo ilifutwa na kurejeshwa upya mwaka 1993 huku ikipangwa kuwa tarehe 08, August.
Maadhimisho ya sikukuu ya nane nane ni moja ya siku zinazogusa maisha ya watanzania waliowengi kwani takwimu zinaonesha kuwa sekta hii inatoa fursa za ajira kwa zaidi ya 66.6% ya watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi, kilimo pia kimekuwa kikichangia zaidi ya asilimia 30 ya pato la Taifa kila mwaka ambapo pia mbali na Tanzania kuuza mazao ya kilimo nje ya nchi zaidi ya asilimia 90 ya Chakula kinachotumika nchini kinatokana na uzalishaji wa ndani wa bidhaa za kilimo.
Aidha serikali imekuwa ikijizatiti kuipa kipaumbele sekta ya kilimo ambayo hata hivyo asilimia kubwa ya wakulima wanajihusisha na kilimo cha mazoea na kundi kubwa la vijana kuona kama ni shughuli isiyofaa kuifanya, lakini takwimu na maandiko mengi yanathibitisha kilimo kuwa sekta pekee inayoweza kutatua wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana hasa wanaomaliza elimu ya juu.
Rai yangu kwa serikali pamoja na juhudi ambazo imekuwa ikifanya ili kukuza kilimo ambacho ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa, Naiomba iwekeze maarifa ya kilimo kwa vijana wa elimu ya juu wanachuo ambao idadi yao inakadiriwa kufikia wahitimu 700,000 kwa kila mwaka.
Mapendekezo ya Njia za Kuwekeza Maarifa ya Kilimo na Kuwawezesha Vijana wa Vyuo vikuu Kujihusisha na Kilimo cha kisasa;
Faida za Kuwekeza Maarifa ya Kilimo na Kuwawezesha Vijana wa vyuo vikuu kujihusisha na Kilimo cha kisasa;
Nihitimishe kwa kusema kuwa kwa Mujibu wa jiografia na mazingira ya nchi yetu kilimo bado kinatudai sisi Vijana kama nguvu kazi ya Taifa.
Cc
Masala sayi
Email:masalasayi9@gmail.com
Media handles: skilledmasala

Kuanzisha somo la kilimo cha kisasa kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu ambalo litasomwa kwa lazima na kila mwanafunzi kama ilivyo kwa somo la uraia na masomo mengine kwani vijana wengi wanaomaliza elimu ya juu wanashindwa Kujihusisha na Kilimo kutokana na kukosa maarifa ya ufanyaji bora wa kilimo cha kisasa.
Kutoa mikopo nafuu na kuweka sera rafiki ya ardhi kwa vijana watakaomaliza vyuo na kutaka Kujihusisha na shughuli za kilimo kwani vijana wengi wanaomaliza elimu ya juu wanashindwa Kujihusisha na Kilimo kutokana na kukosa mtaji na nyenzo za kuanzia shughuli hiyo.
Kuanzisha klabu ya kilimo mashuleni na vyuoni ili kuleta hamasa na kuondoa dhana potofu iliyopo kwa vijana kuhusu kilimo kwani vijana wengi wanaomaliza elimu ya juu wanashindwa Kujihusisha na Kilimo kutokana na kukosa hamasa na dhana potofu iliyojengeka kuwa kilimo ni shughuli ya watu waliofeli shule na hii hutokana na vijana wengi kutokea kwenye familia zinazojihusisha na Kilimo cha mazoea.
Faida za Kuwekeza Maarifa ya Kilimo na Kuwawezesha Vijana wa vyuo vikuu kujihusisha na Kilimo cha kisasa;
Kuboresha sekta ya kilimo kwa kuzalisha wakulima wasomi kila mwaka wapatao zaidi ya 700,000 kila mwaka watakaosaidia kuondoa kilimo cha mazoea na kuongeza uzalishaji bora wa mazao ya kilimo yatakayoendana na viwango vya soko la kimataifa.
Kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana hasa wanaomaliza elimu ya juu kila mwaka kwani kilimo kinathibitika kuwa sekta pekee inayoweza kuajiri Kiwango kikubwa cha watu mpaka zaidi ya asilimia 66.6 kwa takwimu za (NBS, 2018).
Kuongeza nguvu kazi ya Taifa kwani vijana wengi watajihusisha na shughuli za uzalishaji na kuachana na kulalamikia ajira na kusubiri kuajiriwa.

Upvote
1