Maadui zetu ni watu wazuri, tuwaombee maisha mazuri

Maadui zetu ni watu wazuri, tuwaombee maisha mazuri

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
MAADUI ZETU NI WATU WAZURI,TUWAOMBEE MAISHA MAREFU.

Leo 13:15hrs 02/07/2022

Maisha yanaanza na kibao cha mgongoni mtoto analia,kila mtu anafurahi ya kwamba mtoto ni mzima,kibao baada ya kuzaliwa kinakupa ukweli wa maisha halisi ya hapa duniani,kumbe maumivu yaani adui yetu ndiye mtu mkweli zaidi ya raha ambaye ni rafiki,rafiki ni raha yaani mpendwa,nae angesema usimpige mtoto na matokeo yake mtoto angepata matatizo katika ukuaji wake,tuna wajibu wa kumshukuru adui kwa kibao chake kilichotupa ukamilifu wa ukuaji katika maisha mapya hapa duniani,mtoto anayepigwa anaweza kuja kuwa rais baadae,kumbe adui yako anaweza kuja kuwa msaada wako baadae,adui yetu ni mwema,tumuombee maisha marefu.

Adui ndiye mtu aliyenifundisha mambo mengi hapa duniani,adui alinifundisha namna bora ya kuishi,alinielekeza katika njia bora ya kuishi na leo nina mafanikio bora ya kujivunia,kama tukitega sikio kwa adui zetu tunapata mafunzo mengi yatakayo tunasaidia mbele ya safari,adui ni adui kwetu tu,anaonyesha tabia yake halisi lakini anakujengea uwezo wa kuishi kati kati ya mbwa mwitu,adui ameumbwa na moyo wa huruma pia,ukitega sikio utagundua ya kwamba anataka ufuate muongozo wake katika kuishi,ukifuatana nae ni hazina kubwa kwako kwa siku za usoni,kwani utajifunza na hapo baadae utakuwa una miongozo mingi itayokupa uchaguzi bora wa namna bora ya muongozo katika maisha yako,

Maisha ya mwanadamu yanaanza na misukosuko,hii inakuandaa na changamoto za duniani,hadi unazaliwa basi wewe mwamba,karibu duniani,zinaendelea hatari katika kukua,unakuja umri wa kupevuka kwa mwanamke na kwa mwanaume,huu ni muda ambao mtu anafanya mambo mengi ya kijinga,ila kwa neema yake Mwenyezi Mungu,gari halikugonga baiskeli zetu tukiendesha barabarani,wala hatukuanguka kwenye ngazi tukicheza kombolela,wala mchele wenye mawe haukutuletea shida tumboni,hata jeshini adui alipokulenga na baada ya vumbi ukaanza kushika mguu wako,mkono na kichwa na kugundua kuwa kumbe bado ni mzima,ndipo unapogundua kumbe yote ni kukuongoza kuishi maisha bora hapo baadae,

Nilipomsoma adui kutafuta udhaifu wake ndipo nilipogundua,nisichokijua yeye alikijua zaidi na ndipo utofauti wetu na kumchukia kulipoanza,sikutega sikio kwa adui nikamdharau nikakosa hata la kujifunza kwake,sikutumia akili yangu kumfikia,ila kwa sasa najua adui ni mtu bora wa kujifunzia,na katika madhaifu yake naweka nguvu yangu ili adui aweze kuwa bora zaidi,kama ilivyoandikwa kwenye 2 Wakorintho 12:9-10 Lakini akaniambia: “Neema yangu inatosha kwa ajili yako; maana uwezo wangu hukamilishwa zaidi katika udhaifu.” Basi, ni radhi kabisa kujivunia udhaifu wangu ili uwezo wake Kristo ukae juu yangu. Kwa hiyo nakubali kwa radhi udhaifu, dharau, taabu, udhalimu na mateso, kwa ajili ya Kristo; maana ninapokuwa dhaifu, ndipo ninapokuwa na nguvu.

Katika dunia ya leo maadui zetu ndio watu wakweli kwetu,kuliko rafiki zetu,maadui ni kweli wanatuchukia,wanatujaribu,wanatusanifu,hawana unafiki,jiwe wanaita jiwe,na koleo wanaita koleo,adui yupo wakati wa shida na raha,adui atakuombea mabaya na wakati wa shida atakucheka,adui ni mkweli muda wote,rafiki atakuwa nawe kwenye raha na wakati wa shida atakukimbia,hapa tunapata funzo katika maisha haya hapa duniani,nimejifunza uvumilivu,heshima,kufikiri mara mbili kabla ya jambo lolote,kushinda changamoto,nimejifunza mimi hasa ni nani,faida na mapungufu yangu,sasa ninajifahamu.

Nimalizie kwa Zaburi 23:5 "Waandaa meza mbele yangu, machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, na kikombe changu kinafurika" ,katika ahadi zote nzuri Mungu anatupa katika Zaburi hii, hii ni moja ya utukufu zaidi. Anasema atatuwekea meza, kueneza chakula cha ajabu juu yake, na kisha kutupatia sikukuu,na anafanya yote haya mbele ya adui zetu,neno la meza katika aya hii linamaanisha "kuenea" - chakula kikubwa, sikukuu kubwa. Na kuna mgeni mmoja tu katika chakula hiki - wewe! Mungu anafanya kazi hii ya ajabu kwa kila mtu anayempenda,kama Mungu anavyoandaa na kukupatia sikukuu yako, huwafanya maadui wako wakiketi kwenye pindo la nje la eneo na kuangalia kila kitu kikifunuliwa,wataona Bwana mwenyewe akieneza meza yako chakula, akiwapeleka kwenye kiti chako na kukusubiri,kisha wanaangalia wakati unapojaza nafsi yako na bei nzuri ya mbinguni.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
hawa watu hawachelewi kukwambia alianza na unyoya sasa hivi ana kuku 277910
 
Back
Top Bottom