Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Serikali kupitia Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Dkt Jim James Yonazi ametoa akaunti maalum ya Serikali ambayo Watanzania wataitumia ili kutuma fedha kwa ajili ya kuwachangia waliopata maafa Kariakoo.
Jina la Akaunti
National Relief Fund
Namba ya Akaunti
9921159801
Pia, Soma: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Watu 7 wengine waokolewa
Misaada kwa ajili ya waathirika wa kuporomoka kwa jengo Kariakoo itolewe kwenye akaunti moja- Dkt. Yonazi
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema msaada wa kifedha kwa ajili ya kusaidia walioathirika na kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo Jijini Dar es Salaam unatolewa kwa akaunti maalum ya maafa ya 9921159801 ambayo ipo Benki Kuu ya Tanzania na kushughulikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Dkt. Yonazi ameyasema hayo leo Novemba 18, 2024 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hali inayoendelea katika zoezi la uokoaji.
Amesema akaunti hiyo ni pekee nchini ambayo inakusanya misaada ya kifedha kwa ajili ya maafa.
"Kuna watu wana nia njema kabisa ya kuwasaidia Watanzania, lakini naomba tujizuie kabisa kukusanya michango ya kifedha kutoka kwa mtu yeyote bila kupitia akaunti hii". Amesema Dkt. Yonazi.
Aidha amesema akaunti hiyo ni maalumu imethibitishwa na serikali ili kuweza kuhakikisha misaada inawafikia walengwa na inatimiza malengo ya kutoa misaada hiyo.
Amesema kwa sasa operesheni inaendelea mpaka pale watakapokamilisha zoezi la kuokoa baadhi ya watu ambao bado hawajaokolewa.