Maafa ya mvua Moshi: Watano wafariki Dunia wakiwemo Watoto watatu wa familia moja

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Maafa ya mvua tar 25/04/2024 mkoa wa Kilimanjaro.

Kata ya Kimochi s/m Lyakimbila

VIFO
1. FREDY GAGALA DRS 1
2. ANGEL CHAKI DRS 7
3. EDWARD CHAKI F II KOMAKYA SEC.

KATA YA MBOKOMU

FUKENI SHULE YA MSINGI

Kifo Cha mwanafunzi

Joram Peter kimambo darasa la 5.

Miili yote IPO Mawenzi hospital

Majeruhi ni Baraka Peter kimambo darasa la 5 yupo St.Joseph

----
Watu watano wamefariki dunia wakiwemo Watoto watatu wa familia moja, huku kadhaa wakijeruhiwa, kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Pamoja na vifo hivyo, nyumba kadhaa zimeanguka na nyingine kuzingirwa na maji na kusababisha kaya kadhaa kukosa makazi huku mifugo, vyakula na mali nyingine, vikisombwa na maji hayo ya mafuriko katika Kata za Mji Mpya, Msaranga, Kimochi, Kahe na Mabogini wilayani humo.

Mafuriko hayo ambayo yametoka usiku wa kuamkia leo Aprili 25,2024, yanatokana na mto Rau kujaa maji na kuvunja Kingo za mto huo na kupelekea maji kutapakaa katika maeneo ya makazi ya watu na mashamba na hivyo kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na vifo.

Akizungumza wakati wa uokozi katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hayo, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amesema mafuriko hayo yametokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani hap.

"Vifo vitatu ambavyo ni vya watoto vimetokea kata ya Kimochi baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuangukiwa na kifusi, ambao watu wanne katika familia hiyo wamejeruhiwa na tumewakimbiza katika hospitali ya Mawezi, lakini miili mingine miwili tumeiopoa eneo la Msaranga na msitu wa Rau, ambayo ilikuwa imesombwa na maji," amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Unajuaje hana habari.? Yan Kamati za Ulinzi na Usalama za wilaya na Mkoa wasiwe na Taarifa ila wewe uko nayo. Wakati Mwingine sio sahihi kutoa taarifa ambazo uhakika nazo, Mamlaka za Serikali kutokee vifo vyote hivyo na wananchi wasitoe taarifa ila wewe peke yako ndiyo uwe nazo?.
 
Inna lillah wainna ilaihyi rajiun.
Poleni sana.
Jitahidi kujurisha jeshi la polisi ili taarifa ifike ofisi ya mkoa na kisha Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa kwa msaada zaidi
 
Unajuaje hana habari.? Yan Kamati za Ulinzi na Usalama za wilaya na Mkoa wasiwe na Taarifa ila wewe uko nayo. Wakati Mwingine sio sahihi kutoa taarifa ambazo uhakika nazo, Mamlaka za Serikali kutokee vifo vyote hivyo na wananchi wasitoe taarifa ila wewe peke yako ndiyo uwe nazo?.
Mhhhh! Mkuu, Sasa kama Serikali ya hapo inaonekana kuzubaa yan haitoi Taarifa na wala haijasema chochote sioni ni kwa nini jamaa asichukue hatua kama hiyo ili kuwaamsha waliotegemewa (Serikali) kuzitoa Taarifa hizo kwa wadau wengine? au tuseme huamini hilo ila ni mpaka Serikali...?
 
Maafa ya mvua tar 25/04/2024 mkoa wa Kilimanjaro.

Kata ya Kimochi s/m Lyakimbila

VIFO
1. FREDY GAGALA DRS 1
2. ANGEL CHAKI DRS 7
3. EDWARD CHAKI F II KOMAKYA SEC.

KATA YA MBOKOMU

FUKENI SHULE YA MSINGI

Kifo Cha mwanafunzi

Joram Peter kimambo darasa la 5.

Miili yote IPO Mawenzi hospital

Majeruhi ni Baraka Peter kimambo darasa la 5 yupo St.Joseph

----
Watu watano wamefariki dunia wakiwemo Watoto watatu wa familia moja, huku kadhaa wakijeruhiwa, kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Pamoja na vifo hivyo, nyumba kadhaa zimeanguka na nyingine kuzingirwa na maji na kusababisha kaya kadhaa kukosa makazi huku mifugo, vyakula na mali nyingine, vikisombwa na maji hayo ya mafuriko katika Kata za Mji Mpya, Msaranga, Kimochi, Kahe na Mabogini wilayani humo.

Mafuriko hayo ambayo yametoka usiku wa kuamkia leo Aprili 25,2024, yanatokana na mto Rau kujaa maji na kuvunja Kingo za mto huo na kupelekea maji kutapakaa katika maeneo ya makazi ya watu na mashamba na hivyo kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na vifo.

Akizungumza wakati wa uokozi katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hayo, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amesema mafuriko hayo yametokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani hap.

"Vifo vitatu ambavyo ni vya watoto vimetokea kata ya Kimochi baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuangukiwa na kifusi, ambao watu wanne katika familia hiyo wamejeruhiwa na tumewakimbiza katika hospitali ya Mawezi, lakini miili mingine miwili tumeiopoa eneo la Msaranga na msitu wa Rau, ambayo ilikuwa imesombwa na maji," amesema.

Chanzo: Mwananchi
Tupiamo basi walau kapicha au vid.clip mkuu.
 
Hatari sana maji yanasambaa tope na uchafu vinatapakaa!
 
Back
Top Bottom